Ukiweza kudhibiti matumizi ya sukari katika familia yako utaiokoa sana

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1641105117710.jpeg

Sukari tunayoihitaji mwilini tunaipata katika vyakula tunavyokula. Chapati, majimbi, viazi, mkate vyote hivi vinatupa sukari. Unaweza kabisa kunywa chai bila sukari.

Wana historia wanasema kabla ya kugundulika kwa sukari, ingawa afya ya meno haikuwa bora kama ilivyo sasa lakini matatizo ya meno hayakuwa makubwa kama tuliyonayo leo.

Unapokunywa chai yenye sukari, inapitia mdomoni, huelewi tu madhara unayopatia meno yako. Chai bila sukari ni salama kwa meno na afya ya mwili kwa ujumla.

Fikiria pia pesa utakayo okoa utakapoacha matumizi ya sukari. Ukitembelewa na mgeni unamfahamisha kabisa mila na desturi ya nyumba yako, unaweza kuwa unatoa ushauri nasaha wa afya bila kujijua.
 
Back
Top Bottom