Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
MKJJ
Swali zuri lakini turudi kule ambako wengi humu ndani twapenda kufuata referece ni KATIBA ...halafu kuna suala zima la balance of power ambako kwetu hilo ni HARAM lakini having said that najua kuwa BLAIR ni lawyer halikadhalika CLINTON naye alikuwa ni lawyer sasa itabidid tuangalie hilo
DrWho, lakini Blair kwa muda aliokuwa waziri mkuu ni lini alienda mahakamani kupractice law? Hata Clinton analipia kila mwaka ada yake ya uanasheria lakini sijui mara ya mwisho ilikuwa lini yeye kupractice law. Tatizo langu siyo kuwa mwanasheria na mbunge. Tatizo langu ni kuwa mbunge mwenye kuendelea na sheria. Natumaini chama fulani cha wanasheria kinaweza kupinga kitendo cha Mkono kuwa sehemu ya mawakili wakati yeye ni mtunga sheria inayoweza kumuadhibu Dito.
Hivi Mkono akileta mswada bungeni unaosema fundamentally, kuwa sheria ya makosa ya jinai ibadilishwe kitu ambacho kinaweza kuathiri matokeo ya kesi hii nani atamzuia? Naomba Rais kama anasikia amuombe Nimrod awaache wanasheria wengine waishughulikie hii kesi!!