Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Haya ni maneno ya mwisho ya Mzee Tibaigana, on the issue!

".............gari la Mtuhumiwa halikupata hasara yoyote ile, lakini mtuhumiwa alitoka na kwenda kumfuata dereva wa basi, huku akimuamuru atoke nje kwa kutumia bastola, kitu kilichomjengea hofu dereva huyo na kuamua kufunga madirisha ya basi na milango, na kuona hivyo mtuhumiwa aliendelea kugonga dirisha la basi kwa kutmia bastola hiyo, hatimaye bastola hiyo ilifyatua risasi mbili, moja ikamuuwa marehemu kwa kumpasua kichwa na kutoa ubongo wote nje na damu nyingi zikimwagika............."

Sasa guys I am finally getting karibu na ukweli wa hii kesi, leo nimeongea na wasure mbali mbali, wanasema mahakimu wa bongo hawaipendi CCM na serikali yake, kwa hiyo wanasema hayo maneno ya Tibaigana ni balaa kwa Blaza Dito, wakaniambia subiri uone jinsi mvua itakavyomnyeshea!, Hiii ninaipa 80%, kutokana na watu niliongea nao, lakini bado nina-reserve 20%

(a). Pia baada ya kuongea na wananchi wengi huku bongo, sasa I am convinced 60%, kuwa Mzee JK kutoa mfao kwa familia ya marehemu ilikuwa ni kwa nia njema kabisaaa, kwa hiyo Mzee Moshi, you were almost right kwenye hili, lakini bado nina-reserve the other 40%,

(b). Lakini hakuna aliyenishawishi kuhusu viongozi kwenda kujipanga kwa ndugu wa marehemu, ilikuwa tu ni ile ile tabia ya kujikomba baada ya kusikia kuwa rais ametoa mfao,

(c). Kuhusu Blaza Dito kuwa Rumande, hiyo sasa nimehakikisha kuwa ni kweli yuko huko lupango, tena Keko upande unaoitwa unaoitwa general population, yaani kwa mahabusu wote mpaka wezi wa kuku na mbuzi!

To be continued...............kila zitakapopatikana habari mpya!
 
Quarz,
mshikaji umeniacha hoi!...Nimechokaaa!
Yaani kwa sababu watu wengi hufa kwa kugongwa na haya madaladala basi Mbonde anachukua hukumu zao wote?...
Kama ungekuwa na ushahidi ama kesi hata moja ya huyo Mbonde kuua watu ningekuelewa unachojaribu kutufahamisha. sioni kabisa uhusiano wa kifo cha Mbonde na watu wanaogongwa na madaladala.
Hakuna root ya tatizo hili ila wafanya dhana kuipamba. Dito sii mtembea kwa miguu yote yanayotupata huko mitaani na hayo ma daladala yeye huyasikia ktk bomba.
 
mkandara, ni wapi nimeongea hiyo statement uliyoandika,
ni wazi kuwa hujanielewa.
nimekuambia isu hii ni moja ya dalili tu ya mambo mengi yaliyojificha katika suala zima la usafiri dar es salaam, madaladala ni kero namba moja ya usafiri dar,soma pia hiyo post ya mwanakijiji kuhusu mkuu wa mkoa wa dodoma ameongelea kero hizo na pia
ningekushauri ufanye utafiti kwa mwaka mzima tangu uanze ni watu wangapi wamepoiteza maisha kutokana na jali zinazosababishwa na watu wadaladala.
 
quarz said:
mkandara, ni wapi nimeongea hiyo statement uliyoandika,
ni wazi kuwa hujanielewa.
nimekuambia isu hii ni moja ya dalili tu ya mambo mengi yaliyojificha katika suala zima la usafiri dar es salaam, madaladala ni kero namba moja ya usafiri dar,soma pia hiyo post ya mwanakijiji kuhusu mkuu wa mkoa wa dodoma ameongelea kero hizo na pia
ningekushauri ufanye utafiti kwa mwaka mzima tangu uanze ni watu wangapi wamepoiteza maisha kutokana na jali zinazosababishwa na watu wadaladala.
Kwa hiyo basically Ditopile ametupunguzia threat level ya hawa daladala kwa kutuondolea mmoja ambaye (why lie) had the potential ya kuua?
 
Quarz,

Ngoja nitoke nje kdiogo ya mada nikujibu swala la tabia za maderava wa daladala na ajali za barabarani.

Ajali za barabarani hapa Dar-es-Salaam si kosa la madereva wa daladala tu ingawa hata mimi huya wanainiudhi; ni kosa la serikali kwa kiasi kikubwa kutokana na kushindwa kusimamia sheria ipsavyo. Kama umeendesha kwenye mitaa ya miji mingi marekani utakuwa umegundua kuwa wamarekani wengi hawataki kumfuata mtu kwa nyuma, kila mtu anataka awe mbele hata kama kufanya hivyo hakumpunguzii muda wa kusafi na kunaweza kuhatarisha maisha yake. Ile usimamizi wa sheria huwa unawabana kiasi kuwa wanapovunja sheria huwa wako makini wasishikwe. Hii ni tabia ya maderava wengi hasa wanapokuwa wana haraka fulani; kwa vile madereva wa daladala wako kwenye haraka kila wakati ni lazima tabia hiyo wawe nayo kama binadamu wengine.

Tatizo liko kwenye barabara zetu na usimamizi wa sheriaza barabarani. Baada ya ukosefu wa sheria kwa muda mrefu, madereva wengi wamezoea kujifanyia mambo kama watakavyo ingawa wanajua kuwa kufanya hivyo ni makosa. Pamoja na ajali nyingi za hapo Dar es Salaam, utakubaliana nami kuwa hakuna hata dereva mmoja aliewahi kufungwa au kuhukumiwa adhabu ya kutisha. In fact maderava wabovu siyo wale wa daladala tu; unawajua wao kwa vile wako wengi barabarani. Ukifuatilia kwa makini utagundua utakuwa madereva wengi pale Tanzania hawafuati sheria kabisa za barabarani kwa vile ni kama hazipo.
 
quarz,

kuua ni kuua, Dito ameua NA ALAANIWE full stop. Madereva wa daladala ndio ni wakorofi lakini huwezi kujustfy KOSA kwa kutumia KOSA.
Wananchi pia wanakufa na wanaendelea kufa kwa kuwa Viongozi wengine wametuingiza kwenye MIKATABA BOMU, huyo DITO et al wako unaowatetea akiwemo huyo LUKUVI ni KERO SANA KWA WANANCHI lakini haimaanishi leo quarz ukachukue bastola na kwenda kumuua Mr DITO AU LUKUVI eti kwa kuwa walituingiza Mikataba Bomu, Sera Mbovu na matokeo yake hadi leo tunashindwa kudhibiti hata na Malaria na watu wanakufa vilevile

Quarz, wee waangalie tu hao viongozi, they are no longer killing us softly (Mikataba Feki, Rushwa, embazzlement nk), they are now killing us HARD with bullets, Umeme nk.

Quarz umeshawahi kumsikia KINJE? RUPIA? KILONTSI (sasa hivi mwakilishi wetu EU pale Brussels)? na yule Kamishna wa polisi (I think Aziz......correct me if im wrong) aliyeua na baadaye kupelekwa Canada, Hawa wote wamekuwa ni kero na wanapeta mitaani wakati madereva wa daladala walioua wanasota keko, sasa hapo sijui akina "Mbonde" (walalahoi) nao wachukue bastola na kuwa-shoot hao?
 
Quarz,
Ndugu yangu hatubishani ila kama unayo Tafsiri tofauti na maneno haya nambie, tena basi Ogah kakupa safi sana.
Umeandika hivi hapo juu:-
katika hii isu ya ditopile intetion yangu ni kuangalia mambo kwa upana wake,ningependa tuende mbele zaidi kuangalia the root courses of the problems ambazo hilo tatizo moja la ditopile ni dalili ya matatizo mengi yaliyojificha ndani yake.
Kisha ukaendelea na maelezo mengine uliyoandika hapo juu..
Sasa ebu chukulia kuwa marehemu alikuwa na drivers record safi kabisa, hajawahi pata ajali wala kugonga mtu acha kuua... Je, ni haki kutumia issue ya Dito kumhukumu ndugu yetu ambaye sii mmoja kati ya madereva wauaji ati tuone root?..au mwenzetu unazo data zaidi kuhusu marehemu kuwa kazoea kugonga na kuua watu.
Nachopinga hapa ni ku waweka madereva wote ktk chungu kimoja hali wapo ambao wana record nzuri.
Ninge kuelewa tu ikiwa Marehemu aliwahi kukonga mtu na kuua kama mmoja wa hao uliowatolea mfano. Na wala sii daladala peke yake magari yote Dar huua watu kila siku lakini hatuwezi kuwahukumu madereva wote wenye magari.
Ebu fikiria na jiweke katika hali ambayo hata wewe inakuhusu. Mathlan, ndugu yako kapigwa risasi huko Marekani na mzungu bila kosa kisha anatokea mzungu mwingine na kusema - "unajua hawa watu weusi ni majambazi sana wanaua kila siku, kwa hiyo tutazame root course ya problem."
Quarz, sidhani kama utamwelewa huyu mtu kwani kosa la majambazi ya mtu mweusi na ndugu yako ambaye sii jambazi hazihusiani kabisa.
Dito kachemsha ndugu yangu hakuna zaidi na kama marehemu angekuwa kamgonga mtu na kumuua kisha Dito akachukua hatua hiyo -LABDA tungeweza kuona upande wako kwa mapana yake.
 
Ogah said:
quarz,

kuua ni kuua, Dito ameua NA ALAANIWE full stop. Madereva wa daladala ndio ni wakorofi lakini huwezi kujustfy KOSA kwa kutumia KOSA.
Wananchi pia wanakufa na wanaendelea kufa kwa kuwa Viongozi wengine wametuingiza kwenye MIKATABA BOMU, huyo DITO et al wako unaowatetea akiwemo huyo LUKUVI ni KERO SANA KWA WANANCHI lakini haimaanishi leo quarz ukachukue bastola na kwenda kumuua Mr DITO AU LUKUVI eti kwa kuwa walituingiza Mikataba Bomu, Sera Mbovu na matokeo yake hadi leo tunashindwa kudhibiti hata na Malaria na watu wanakufa vilevile

Quarz, wee waangalie tu hao viongozi, they are no longer killing us softly (Mikataba Feki, Rushwa, embazzlement nk), they are now killing us HARD with bullets, Umeme nk.

Quarz umeshawahi kumsikia KINJE? RUPIA? KILONTSI (sasa hivi mwakilishi wetu EU pale Brussels)? na yule Kamishna wa polisi (I think Aziz......correct me if im wrong) aliyeua na baadaye kupelekwa Canada, Hawa wote wamekuwa ni kero na wanapeta mitaani wakati madereva wa daladala walioua wanasota keko, sasa hapo sijui akina "Mbonde" (walalahoi) nao wachukue bastola na kuwa-shoot hao?
i agree kabisa, it was cold blooded murder, 2 shots...
he must pay for this crime...mtu mzima hata hajui ku file insurance claim ya prado hiyo?
 
mkandara,
mimi mtazamo wangu mara nyingi naangalia root course of the problems badala ya kuangalia the apparently problem or symptoms.
kwasababu utakapotatua root course of the problems you will end up solving the problem itself completely.

mfano.
kuna sheria ya balabalani inasema mnapokuwa kwenye msafara kila gari inatakiwa liache umbali fulani kutoka gari jingine,
hii inasaidia mfano kwenye congestion na gari moja mbele lika punguza mwendo kwa ghafla, lile la nyuma liweze kumanage speed yake bila ya kusababisha ajali.
sasa utaweza kuona kama dreva yule wa daladala alifuata sheria hii sidhani kama haya yote yangetokea,
kwahiyo root course of the problem ni kutofuatwa kwa sheria za barabarani na matokeo yake waathirika ni wote wasafiri na madereva wenyewe.

sasa hivi watu tunalia tu na ditopile, okay.
lakini ujue tukisahau kutatua tatizo hili,keshokutwa litatokea jingine linalofanana ni hilohilo.

mfano mngine ni isu hii ya majambazi, unaona kila mtu analia ujambazi,
lakini je wameshawahi kukaa chini na kujiuliza hasa nini kinasababisha ujambazi nchini,
kama una asilimia zaidi ya 80 ya vijana hawana ajira, wala ujuzi wa kujiajiri unategemea watafanya nini? au watakula nini?
suluhisho ni kuwa na comprehesive strategy ya kutatua tatizo hili.
 
What a contradiction, hebu angalia hii statement ya quarz

…………………………….kwahiyo siku ya tukio kama siku nyingine ditopile alikuwa na silaha na wala hakunuwia kuwa siku hiyo anaenda kuua mtu. tena unaona ilikuwa ni majira ya saa mbili pengine ndio alikuwa arudi kupumzika. sasa pale imetokea ajali.(prado yake mpya imegongwa) hivi nani kati yenu prado yake imegongwa na ataanza kucheka au kumbembeleza mtu aliye gonga prado lake?
lazima pale jamaa alikasirika sana, sasa baada ya hapo anaamua kushuka na kwenda kukabiliana na dreva wa daladala, unategemea aiche silaha yake ya ulinzi (take into consideration the behaviour of daladalas youngmen who smoke marijuwana?)..............


very funny, mzee quarz hapo juu unahalalisha/unasupport Dito kuua kwa sababu/matatizo unayotaja kuhusu madereva wa dala dala


Now, here you come again quarz

………………………..mimi mtazamo wangu mara nyingi naangalia root course of the problems badala ya kuangalia the apparently problem or symptoms.
kwasababu utakapotatua root course of the problems you will end up solving the problem itself completely..............


very funny indeed, yaani nikiunganisha maelezo yako napata picha ya kwamba, ili quarz asolve problem , ana-deal na root course in quarz sense/fashion of thinking, ni kuua!!!! duuhh


Absolutely ridiculous!!
 
quart acha upuzi wako we!
sis tumepotelewa na ndugu yetu wewe unakuja na msalahi ya kipuuzi.

Tunathamini gari kuliko maisha ya mtu!

Pia sheria zipo kama serkali yenyewe imeshindwa kuwabana madreva wakorofi na wahuni, ni nani wa kulaumiwa kutokana na ajari ni serikali kushindwa kazi au madreva!!!

Stop upuuzi wako huo. Kama angekuwa ndugu yako ungesema hivyo!
Ni kweli madreva wanasababisha ajali lakini unafiriki serikali iko makini kuwabana?

Mbona nchi nyingine madreva waoga na wanajua sheria zipo na zinatekelezwa!

serikali ya tanzania badala ya kuwabana mdreva mara wanakuja na uhuni kama wa Sumaye eti speed Governer etc. Huku kote ni kushindwa kuendesha nchi!

Stop that nonsense argument.
 
Sheria za barabari hazifuatwi kwa sababu wamiliki wengi ni viongozi! Iliwahi kusemekana wenye daladala wengi ni viongozi hata hasa awamu iliyopita.
Mdreva wanakuwa na kiburi kwa sababu anajua kwa mfano gari ni la RPC, au la waziri wa sheria kwa mfano!

serikali iwe makini na iwabane waendesha magari makubwa na madogo kupunguza vifo barabarani. Na siyo mtu mmoja mmoja aamue kutumia PISTOL kwa kuwa gari lake limegongwa na huhu yeye ni mkuu wa mkoa!!
 
sasa ndugu yangu holga,
labda nianze kukueleza kisayansi utaweza kunielewa.
kwenye sayansi wanasema "there are some ACTIONS/EVENTS which may trigger another ACTION or EVENTS to occur with either NO,LITTLE or MUXIMUM Consequences.

>>>>>>>>>>>>>>HAS TRIGGER<<<<<<<<<<<<<<<<<
[EVENT A]--------------------------------->[EVENT B]

Examples1
>>>>>>>>>>>>>>>>>triggered<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
[EVENT A]--------------------------------->[EVENT B]
(ajari ya gari)*********************** (reaction ya mwenye gari)
**********************************killing a driver
example 2
>>>>>>>>>>>>>>>triggered<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
[EVENT A]--------------------------------->[EVENT B]
(earthquake)*************************(Tsunami)-kilings thouthands


example 3
>>>>>>>>>>>>>>>triggerd<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
[EVENT A]--------------------------------->[EVENT B]
(kunywa maji*****************************(kuugua kipindupindu
yasiyochemswa)*************************na mamia kupotezamaisha)

sasa sisi wanasayansi tunapotaka kutatua tatizo "we are not much concerned with EVENT B, we are much focused on EVENT A which causes EVENT B,
because EVENT B wouldnt have happened if EVENT A wouldnt at the first place.

ili kuzuia kipindupindu(kinachasababisha mamia kupoteza maisha) tunahitaji kuadress suala la watu kunywa maji safi na usafi wa mazingira.

ili kuokoa watu na janga la tsunami, we need to focus on the earthquake wich triggered the TSUNAMI.

ili kuzuia vifo kwa ajali za barabarani tunahitaji kufuatilia sheria za barabarani.

TOFAUTI YANGU NA WEWE NI KUWA WEWE UMESHIKILIA EVENT B,MIMI NAJARIBU KUANGALIA NI JINSI GANI TUNAWEZA KUZUIA EVENT A KUTOKEA.
NAFIKIRI UMENIPATA.
 
Dereva kagonga gari la ditopile - Kosa
Dereva akakimbia - kosa
Mbele akasimama - Safi
Dito akasimama kuuliza dereva - safi
Dereva akafanya uhuni kutoshuka na kuangalia uaribifu aliofanya - Kosa
Dito akatoa bastola amtishie dereva - Kosa
Dito akamdito dereva -kosa.

Dito angemuacha na kumdharau tu huyo dereva, wengi wanaboa saaaana jamani, yaani anaweza hata kusimama katikati ya barabara na kupakia au kushusha abiria. na ukiwauliza lugha wanayotoa huwa ni mbaya au ananyamaza kimya, yaani hata msamaha hawaombi.

Dito ange muacha mshikaji na kujaza bima kesho yake, Labda bro Dito has been away for too long!! ahaha alipotoka daladala wala hazikua nyingi sasa amerudi town anajifanya ni mjanja kumbe mji umebadilika.

Asanteni
 
mkuyuga said:
quart acha upuzi wako we!
sis tumepotelewa na ndugu yetu wewe unakuja na msalahi ya kipuuzi.

Tunathamini gari kuliko maisha ya mtu!

Pia sheria zipo kama serkali yenyewe imeshindwa kuwabana madreva wakorofi na wahuni, ni nani wa kulaumiwa kutokana na ajari ni serikali kushindwa kazi au madreva!!!

Stop upuuzi wako huo. Kama angekuwa ndugu yako ungesema hivyo!
Ni kweli madreva wanasababisha ajali lakini unafiriki serikali iko makini kuwabana?

Mbona nchi nyingine madreva waoga na wanajua sheria zipo na zinatekelezwa!

serikali ya tanzania badala ya kuwabana mdreva mara wanakuja na uhuni kama wa Sumaye eti speed Governer etc. Huku kote ni kushindwa kuendesha nchi!

Stop that nonsense argument.

mpuuzi utakuwa ni wewe ndugu yangu,
hata kama magari ni ya viongozi ni nani anayaendesha?
na unavyo ongea utafikiri kuwa hakuna sheria za barabarani, sheria zipo ila hazifuatwi,
YAANI HATA KUFUTA SHERIA WA KULALAMIKIWA NI KIONGOZI?
HUO SASA NDIO UPUUZI WENYEWE,KWAHIYO UNATAKA KIONGOZI AKUFATE NA KUKWAMBIA KUWA SASA SIMAMA KUNA ZEBRA,
ZEBRA IMEWEKWA ILI MADEREVA WAIFUATE, LAKINI ANGALIA MADREVA WANGAPI HASA WA DALADALA WANASIMAMA KWENYE ZEBRA?
KWAHIYO HAPO UNAMLAUMU MWENYE BASI AMBAYE YUKO OFFISISNI KWAKE AU UNAMLAUMU YULE DREVE AMBAYE HAFUATI SHERIA?
 
Back
Top Bottom