Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mzee ES,

asante sana kwa information , mimi siku zote huwa niadmire sana politics za bongo ni kama movie ...yaani watu wameshaenda mbali mpaka kupanga ni gereza gani huyu bwana hatafungwa ! Na msamaha autapata kivipi ? Everything is possible in bongoland
 
sasa si unaona tayari taarifa zinasema bastola haionekani,sasa bila ya silaha kuwepo kesi inakuwa weakened. He will go to jail for manslaughter and he will be out in 5 years or even less.Yote haya ya kuandika barua ya kujiuzulu na nini,ni late effort za kuonyesha humility.
 
Kama kesi imeshapangwa na kuamuliwa aina ya hatia na wapi afungwe, hapo tutasema kuna mfumo wa sheria na utawala bora. If it is going to happen as put by Mzee ES it'll a big shame on our judicial and governance system.
 
There is no such a thing like "big shame on..." that is a vocabulary in bongoland.

Thats how we do things. Umesahahu tupo kwenye siasa ya ujamaa?. mwenzetu, ndugu yetu au kama wasemavyo wa russi comrade. Bro ditto ni mwenzetu, bahati mbaya tu alipatwa na wazimu wa muda. tusamehane mara sabini u sabini.

FD
 
ya'll underestimate Mahakama Kuu ya Tanzania! waache wapambe waseme wanachosema.. but our courts are one of the most independent on the continent... and I'll tell you this... kitu pekee kitachokuja kumuokoa ni huo msamaha wa Rais, ambao nina uhakika hauwezi kuwa ndani ya miaka mitano ya mwanzo ya JK so at most atatumikia angalau miaka tisa jela.. but... Mahakama Kuu itampa kama si maisha basi angalau 30 years!!!!!
 
Nina imani na mahakam kuu, tatizo liko upande wa prosecution. DPP anaweza kuamua kupeleka kesi isiyokuwa na uzito wowote, kwa hiyo mahakama inaamua kulingana na jinsi kesi ilivyopelekwa.

Kwa vyovyote vile kama kesi hii ikigeuzwa kuwa manslaughter na jamaa akatumikia kifungo kifupi nadhani vurugu litazuka hapa nchini kwa mara ya kwanza hasa kwa vile bado watu wana kumbukumbu jinsi Nguza na familia yake walivyofungwa maisha kimchezomchezo tu. Itakuwa imeonyesha kuwa makabwera wanaweza kuswekwa jela maisha wakati wakubwa wanaachiwa kuyeya.

Vipi kesi ya mtoto wa Mungai imefikia wapi jamani?
 
Msihofu vijana!
viongozi wa Tanzania waoga!!
au niseme baadhi yao!! he- he -This is funny!!

Tufuatiliane pole pole taratibu..kwa uakika..Labda Mzuzuri alikua ana Marelia!!
au bangi!? au nini?...au hiyo ndio ili kua tabia yake kwa miaka yote kama kiongozi!?

Hii kesi iendeshwe kisanii.. kwasababu hii mplya imewafikia wengi kwa haraka!..
Tumsikilize ana jiteteaje...Tumpende ikiwezekana tumsamehe!

Huuu - muda umeisha - see you soon..
 
Maoni yangu knowing siasa za bongo,

(1). Ditopile, ni rafiki wa karibu wa Jk tena sana kuliko hata watu wanavyofikiri, toka JK apate habari hizi amekosa amani, he is a friend, je tunawakimbia marafiki wakiwa kwenye matatizo?

(2). Akizungumza na kina Mtandao, RA, EL, na the rest watamwambia muache afungwe, unajua hiii itakuharibia sana sifa zako na kazi yako! Na huyu bwana ni mjeuri siku zote huyu!, lakini EL atamvuta pembeni na kumwambia Jakaya, hebu muulize JM kwanza usiende kama mjinga bro!

(3). Ditopile, pamoja na kwamba ni mmoja wa maadui wakubwa wa JM wa bila sababu, atamwambia Jk, Jakaya huwa hatuwakimbiii marafiki wakiwa na shida, ndio maana hata mimi rafiki yangu Vernon Mwaanga, alipokamatwa na madawa ya kulevya kule Zambia nilienda kumuombea kwa Kaunda akamsamehe kifungo cha miaka 30, sasa itakuwa wewe?

Halafu kumbuka huyu Ditopile ni mwenzetu huyu, sasa kama you have to save him ni lazima iwe kabla ya uchaguzi au baada ya uchaguzi, unajua tutawapa upinzani hoja ya kutusumbua kwenye election, lakini lazima umuokoe,

(4). Jk itabidi aende huko Pwani kwanza kuonana na wazee na kuwaambia kuwa wazee mwenzetu ni lazima aende jela kidogo kwa hiyo mtanisamehe lakini nitamtoa baadaye, Mzee Dito atapigwa miaka kumi ya manslaughter, baada ya uchaguzi wa 2010, atatoka msamaha wa rais,

Hapa decision has to be made kati ya Jakaya Kikwete, Said Mwema, na Rashid Othman, with baraka toka kwa JM, that is all,

Mahakama ipi bongo itakayompa miaka 30? Jaji gani huyo asiyejitaka? Atapelekwa pale Morogoro ambako, tofauti ni kwamba huwezi tu kwenda nyumbani lakini all is good kama boarding school, tena ni njiani kwa hiyo ni guaranteed viognozi wakuu watakuwa wakimpitia kila wakati wakiwa wanaenda Dodoma, with in time atatoka hasa kwa hoja ya ugonjwa,

Lakini hatarudi tena kwenye siasa, ataingia upinzani maana yule jama ni jeuri sana!

Mtoto wa Mungai, haendi kokote ataachiwa tu very soon!

Haya ni maoni yangu knowing siasa ya bongo!
 
Kijana hapo umeshusha vitu ile inavyo takiwa..
imenifanya nienedelee kushusha mambo!!

kama ni hivyo Basi JK anakazi nzito..Kwanini kazi kama hiyo iwe ya Kikwete..
Kuna mahakama ya Tanzania..Hapo ata ukicheza usanii lakini uongo hautakiwi...

hebu apewe muda wa kujitetea kwenye media..kwa viki nzima tumuone!!
Waafrica wapewe moyo wa kusamehe...moyo wa kuamua...Tukiwa tunapoteza hizi timing!! tutachelewa sana..

hay nafikiri ni mambo- Ya state craft!! he-he this SAD...Not funny at all..
he- this is funny...oooh he!
 
Naweza akasamehewa huyo Brother Ditto na Yule Justin Nyari wa arusha. nimenotice hichi kitu kwa msamaha wa RAIS.
 
quarz.. mke wa marehemu alishakufa... sasa ni babu na bibi tu.. jamani kama kuna mtu ana details za watu hawa naomba nipatiwe....
 
Mzee Mwanakijiji,

Nimepeleka salaam Bongo nadhani tutazipata habari kamili kupitia wana blog kama wewe ambao wamejitolea kulifuatilia. Najaribu pia kupata mhusika wa hawa watoto maanake kuna habari kuwa marehemu alikuwa na mke mwingine ambaye ndiye mlezi....Kisha tutajaribu kukuunganisha...mambo yote nadhani bora uwasiliane na Michuziline kwa sasa naona kalivalia njuga.
Kibongobongo ndugu watakapo sikia michango hiyo tena ngoma nyingine!... Mawakili, mnatakiwa kazi hii bila malipo Mpoooo!
 
Mawakili hapa watakuwa na kazi gan?Hii ni kesi ya State vs Dito,labda kum-sue Dito for wrongfull killing,na hio ni mpaka kesi hii iishe,au wiunganishe na serikali,lakini sioni hilo litawezekana kivipi,maana Dito hakuwa sehemu yake ya kazi na alitoroka,maana mabosi wake walikuwa hawana taarifa kuwa yupo town.Sasa wanaweza kum-sue Dito kwa kumuua bread winner wa familia,sina uhakika,i'm just speculating
 
Kitendo cha JK kumpa pole Dito hakijakaa sawa,mtu wa kupewa pole na rais ni mfiwa na sio muuaji...ni mtazamo wangu tu
 
@ Zanaki
Hapo Ndipo sanaa inapoanzia- Kitendo cha kumpa pole Ni-ujumbe tosha kwamba 'we are sorry'...!! Lakini -take care- no way out!!

Kwahiyo Jk Yupo sahihi...!!Hat kama Nini wewe lzima umuonee huruma mtu yeyete anapokua kwenye matatizo....
 
Mawakili Mapande na Ringos naona wamekuja juu na kutaka kututisha kuhusu kuzungumzia kesi ya Mzee Ditopile.

Tafadhali naomba Mawakili hawa watuache na wafanye shughuli yao ya kumtetea Ditopile (ambayo wazi itaongeza credibility zao).Sisi mitizamo yetu haitopindisha ukweli wa sheria, na naona si vibaya kumjadili Dito kwa kuwa alikuwa Kiongozi wetu na Mtanzania mwenzetu, kitendo cha kututisha kutokana na nguvu zao wanasheria hawa, kisheria ni kuingilia haki yetu ya kimsingi ya "kueleza/kujadiliana" tunachokielewa.
 
Back
Top Bottom