Ukiwa wewe Rais kipi kipaumbele chako

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,752
5,973
Mwl Nyerere aliwahi kuhoji jiulize umelifanyia au utalifania nini Taifa lako. Kama ungepewa nafasi ya Urais kipaumbele chako kitakuwa nini!

Hili ndilo swali tunapaswa kuwahoji au kusikia kutoka kwa wagombea Urais.

Nikianza mimi mwenyewe, kama ningepewa nafasi hiyo nitatekeleza kwa vitendo miiko ya uongozi ili kurejesha maadili na uwajibikaji.
 

mjinga

JF-Expert Member
May 11, 2008
328
129
1.Nitasimamia kupata katiba safi
2.Nitawaweka ndani wezi wote wa Escrow waliojificha ktk benki ya Stanbic, wezi wa Epa,Meremeta, Lada,
3 viongozi wote waliohujumu uchumi na kutia hasara nchi hii,
4.Nitaiipitia mikataba yote mikubwa mikubwa,
5.Makampuni yote ya nje kutofaidika na kodi za free….nitawapa wafanya biashara wa ndani free kodi na sio wawekezaji wa nje
6
7
 

fikikungetaa

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
331
79
6. Ningesimamia kwa umakini mkubwa sector zinazochangia pato la taifa kukua
7. Ningehakikisha miradi yote ya ndani ya nchi inafanikiwa km proposal isemavyo ndani ya muda uliowekwa
8. Mtu Yeyote atakae jaribu kuhujumu uchumi wa nchi atadhibitiwa chini ya sheria kali za nchi ama kufukuzwa nchini kabisa.
9. Nitaunda katiba ambayo itagusa kila eneo na yenye kunufaisha maendeleo nchini
 

Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,614
18,437
Ninge hakikisha vijana wote ma Billioner mali zao zote zinataifishwa na kuswekwa ndani!!

-Elimu
-Afya
-Nishati
-Miundo mbinu
-

-60% ya bajeti inaenda moja kwa moja jeshini!


Ningehakikisha mikataba yote ya ki mbwa na ya ki Cadaver naifutilia mbali!
 

Humilis

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
758
743
Kwangu ingekua ni Elimu...elimu imebeba mambo mengi sana na ndio msingi wa maendeleo...

Kwa aliyesema...
1.Elimu
2.Elimu
3.Elimu
Yupo sahihi kabisa...
Elimu kwanza jaman
 

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
2,257
1,668
1.Nitasimamia kupata katiba safi
2.Nitawaweka ndani wezi wote wa Escrow waliojificha ktk benki ya Stanbic, wezi wa Epa,Meremeta, Lada,
3 viongozi wote waliohujumu uchumi na kutia hasara nchi hii,
4.Nitaiipitia mikataba yote mikubwa mikubwa,
5.Makampuni yote ya nje kutofaidika na kodi za free….nitawapa wafanya biashara wa ndani free kodi na sio wawekezaji wa nje
6
7


TANZANIA HAMNA MAFISADI WALA UFISADI,sababu wote unaowahisi mafisadi wangekuwa wamepelekwa mahakamani na kuthibitishwa kuwa ni mafisadi.
 

Mr. Mangi

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,515
759
Mi ningefanya mengi sana kwa vitendo na kwa uaminifu mkubwa na hamna sekta yoyote ningeipa kipaumbele namba 2 zote ningeanza nazo maana zote zimeoza

Labda nieleze kwa uchache
1. Elimu, ningehakikisha masomo yote yasiyo na mashiko kwa mwanafunzi na taifa yanafutwa na ningehakikisha kuna elimu ya ufundi stadi na kwa vitendo, pia kuanzia kidato cha kwanza mtoto angesoma masomo machache na anayoyahitaji (specialization) kuyafanyia kazi ktk maisha yake pia walimu na watumishi waliopo ktk mazingira magumu wangelipwa nusu mshahara kila trh 15


1. Afya. Hili ningeanza na usafi wa mazingira wa lazima kila wikend pia kuhusu Tiba ningehimiza tafiti za kina ktk dawa za asili pamoja na lishe Tiba na vingepewa kipaumbele kabla ya madawa ya kizungu pia vyakula vya aina yoyote Ingekuwa marufuku kuingizwa nchini toka nje

1. Uchumi. Uzalishaji nchini ungeongezeka kwa kujenga na kufufua viwanda na ingeambatana sambamba na uboreshaji wa hali ya juu wa kilimo cha umwagiliaji ikiwemo kwa kusafirisha maji toka kwenye vyanzo lukuki tulivyonavyo kwani kwa nchi zetu maendeleo ya viwanda hutegemea maendeleo ya kilimo pia sherehe zote za kitaifa zingesimama kwa muda na zingefanyika kila baada ya miaka 10 kama vile sherehe za mwenge wa Uhuru, muungano n.K kwa kufanyaje hivi tungejipatia fedha nyingi za akiba na tungeweza maliza Deni la taifa pia utalii, madini, gesi, wanyama pori ningevisimamia vilivyo

1. Ulinzi na usalama. Ningehakikisha jeshi hasa la wananchi linakuwa ki technology na sio kwa idadi ya askar waenda kwa miguu (infantry) pia jeshi la polisi ningehakikisha wanafanya kazi kwa weledi na sio kutumia nguvu na darasa la 7 wala kidato cha nne hasingeruhusiwa kujiunga na jeshi lolote

1. Utawala bora. Hapa haki na usawa vingekuwa mstari wa mbele na upande wa siasa Ingekuwa si ajira ila ni wito wa kuwatumikia wengineo hivyo kwa kuanzia na raisi mshahara na marupurupu vingepunguzwa kwa asilimia 50 kisha wabunge wafuatie n.k usawa wa jinsia ktk uongozi wala ulemavu usingekuwepo kwani yoyote angekuwa kiongozi kwa kukidhi vigezo na sio kwa jinsia yake ama ulemavu

1. Sheria na Katiba. Utawala wa sheria ungezingatiwa na upande wa Katiba tungebadili na ktk uchaguzi kura ya kidato cha 6 na kuendelea isingekuwa na thamani sawa na ya mtu mwingine asiye na elimu hiyo na kuendeleza na kiongozi yeypte ubadhilifu angewajibishwa kwa kurudishwa alichokiiba n.k

Yapo mengi ila kwa Leo tosha
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom