Ukiwa unaenda kuhamia nyumba mpya nini huwa unachunguza na kuzingatia?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,085
1,768
Wakuu,

Tupeane maujuzi hapa ya mambo ya kufanya na kutokufanya

Ukiahamia chumba kipya au nyumba mpya uzingatie nini?

Sasa msije mkasema "Uingie na boksa kinyume nyume"🤣🤣🤣🤣maana nimewahi kusikia kuna watu nishasikia lazima waweke kwanza vitu vyao kuua chochote kilichoachwa na aliyetoka sehemu hio! Balaa linakuja unachoweka kimezidiwa nguvu na mtangulizi🤣🤣

Twende kazi...

nyumba ya kupanga.jpg

Pia soma: Tabia ya kutembeza wageni kwenye nyumba mpya!
 
Majirani ni wakuwa nao makini sana, penda kuobserve/kumsoma mtu kwanza kuliko kusikiliza ya wanaokuzoea haraka, wengi huwa ndio wabaya wasambaza chuki.
 
Kwanza naomba nikupongeze kwa hatua kubwa ulio fikia.
Zaidi nikushauri uzingatie security, jitahidi kujua watoto wako wanacheza na watoto wa akina nani, jitahidi watoto wako wasipende kutoka/kucheza nje ya uzio wako.
Zingatia mambo ya kijamii inayo kuzunguka, ila usipende kupendwa na jirani zako hadi pale utakapo wajua vizuri tabia zao.
Nyumba mpya inaraha zake mkuu, ila ukisha hamia ndipo utaanza kuona kasoro zake na hapo ndipo utaanza kukosoa kwamba hapa na pale fundi alikosea na pengine ingekua hivi.
Ukihamia kwenye nyumba mpya, jitahidi pia fanya mpango uwe na usafiri wako mkuu.
Kwaleo naomba niishie hapa.
 
Back
Top Bottom