Ukiwa na sifa hizi unaweza kuchaguliwa kiongozi wa serikali muda wowote

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
1. Uwe ni mtu mnafiki ambaye ukiomba pesa serikalini,mfano milioni 100 ,kwa ajili ya kuendesha taasisi au position uliyonayo, uko radhi kupewa 5% of that na kuridhika huku ukishukuru sana bila kulalamika au kutishia kujiuzuru nafasi hiyo kwa kigezo cha kutoweza kufanya kazi kwa fedha kiduchu!
2. Uwe mtu ambaye unaweza kutengeneza dili za pesa( kwa wizi au ubadhilifu) na kuzificha kwenye akaunti ya nje ilmradi bosi wako akigundua uwe radhi kumpunguzia kidogo ili kumtuliza.
3. Uwe mtu ambaye uko tayari kufa kuliko kujiuzuru nafasi yako kwa sababu yoyote iwe ya kweli au ya uongo
4. Uwe tayari kutetea uozo wa namna yoyote ilmradi uwe umefanywa na bosi wako au yeyote aliye juu yako
5. Uwe tayari kuwashughulikia watu wote kwa vyovyote vile,hata ikibidi kuwaua, wanaohatarisha kudondoka kwa mkate wako au wa bosi wako
Nawasilisha!
 
uwatoe nje wabunge wa upinzani
uombe mwongozo,utaratibu,ufafanuzi unaowaumiza wapinzani
uibe trlioni 3
upende kupanda ndege
 
Leo nimekuwa kama mtu aliyepata msiba mkubwa sana.
Hii hali huwa najisikia mara chache sana. Mara ya mwisho ilinitokea mwaka1999 wakati Mwalimu Nyerere alipo fariki dunia.
Leo imenitokea tena baada ya kusoma thread za kusikitisha kuhusu viongozi wa Taifa hili changa, lenye rasilimali nyingi lakini wananchi wake ni masikini huku viongozi ni matajiri wa kutupwa.
 
uwatoe nje wabunge wa upinzani
uombe mwongozo,utaratibu,ufafanuzi unaowaumiza wapinzani
uibe trlioni 3
upende kupanda ndege
ujue kulala bungeni, ujue kujikomba,ujifanye mjinga km waziri wa uchukuzi anajifanya kuwa pesa ulizopewa kwa wizara nyeti kiasi hiki
 
uzuri ni kwamba sa ivi wanajitaja wenyewe! tutafika tu hata kama ni taratibu
 
Back
Top Bottom