Ukiwa mwanasiasa hakikisha unatenga muda wa kusoma na kuwaelewa wana falsafa wa enzi. Ni hitaji muhimu la maamuzi utakayofanya

Taifa letu lina ombwe la maarifa ndio maana unaweza kuona mtu amevaa suti na kunyoa vizuri ila akizungumza kichwani ni debe tupu.
Huwezi kuona wachangiaji wengi hapa,but trust me umeongea moja ya jambo la maana Sana ambalo mwalimu Nyerere alilipigania Sana wakati anang'atuka madarakani na wakati wa ustaafu wake.
Maarifa mengi yamefichwa vitabuni,chochote ambacho unamkwamo nacho,ukitafuta vitabu vinavyoendana na ishu yako utapata ufumbuzi.
Tusome vitabu,tusiamini sana vyeti vya ngazi mbalimbali za elimu.
 
Kabisa.. 48 laws of power ni kama mkisanyiko wa masomo mbali mbali ya philosophers wa zamani..
Yes kitabu kina madini mengi sana na ingawa stories nyingi za zamani ila Zina reflect Hali halisi ya dunia ya Leo. Na humu duniani hamna jipya yote ni marudio tu ya kale ila with modified technology ila watu ni wale wale tu
 
Huwezi kuona wachangiaji wengi hapa,but trust me umeongea moja ya jambo la maana Sana ambalo mwalimu Nyerere alilipigania Sana wakati anang'atuka madarakani na wakati wa ustaafu wake.
Maarifa mengi yamefichwa vitabuni,chochote ambacho unamkwamo nacho,ukitafuta vitabu vinavyoendana na ishu yako utapata ufumbuzi.
Tusome vitabu,tusiamini sana vyeti vya ngazi mbalimbali za elimu.
Ni sahihi mkuu mimi nimeanza kusoma Bible , najitahidi sana kuwa kwenye Utulivu wa kusoma ili nitoke na kitu na nafanya mazoezi ya kile nilichokisoma, nasoma habari za wafalme na Maisha kwa ujumla lengo nahitaji kuwa kiongozi bora.
 
Ndo mana nikasema asilimia kubwa... nikimaanisha kuna ambavyo vipo sasa havikuwepo zamani..

lakini lazima uelewe hata hii artificial intelligence unayoiona sasa ni zao la wana falsafa wa zamani, watu kama akina Tesla, Newton, Shrodinger, Edison, Da Vinci etc.. bila kazi zao usingeona huu ugunduzi wa sasa
Ni kweli kabisa tunaita "ukuaji wa Teknolojia" huu mchakato umeanza siku nyingi.
 
Suala la kusoma falsafa ni la kila mtu aliyehai na anayejua kusoma na kuandika. Mimi natamani hata mitaala ya degree mwaka wa kwanza wote watu wasome falsafa halafu mwaka wa pili na watatu waendelee na mambo yao. Falsafa ni msingi wa Maisha.
 
Nantombe Mushi, kama mtu anataka kuwa msomaji mzuri na aelewe anachosoma unamshauri afanye nini?
Google majina ya wanafalsafa wa zamani.. halafu katika kila mmoja, tafuta kitabu chake halafu anza taratibu kusoma baadhi ya vitabu vyake.

Kuna wanafalsafa wa kwenye siasa, uchumi, literature, hesabu, sayansi, dini, etc.. ni wewe mwenyewe tu kuchagua unaguswa na nini
 
Suala la kusoma falsafa ni la kila mtu aliyehai na anayejua kusoma na kuandika. Mimi natamani hata mitaala ya degree mwaka wa kwanza wote watu wasome falsafa halafu mwaka wa pili na watatu waendelee na mambo yao. Falsafa ni msingi wa Maisha.
Ndo mana hata mtu kuwa padri lazima asome falsafa.. ni muhimu mno aisee.. sema basi tu.. ikiwa watu wangekuwa wanasoma maandiko ya wana falsafa maisha yetu yangekuwa ya tofauti sana... hata demokrasia yetu ingekuwa sana na watu wangekuwa na uwezo mkubwa wa ku reason mambo
 
Back
Top Bottom