Ukiwa mpinzani Tanzania ina maana kuwa unapinga kila serikali iliyoko madarakani?

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Kuna aina fulani ya uchangiaji ambayo imeonekana kupotosha wasomaji katika media mbalimbali kuwa kila linalofanyika Libya linaonesha kuwa tahadhari kwa watanzania, ili wasiendelee na moto wa mabadiliko kisa eti vyama vyenye nguvu kama CHADEMA, CUF au NCCR vyaweza kuwa kama waasi wa Libya.

Hii ni propaganda mpya inayobuniwa huku wabunifu wakilia kuwa na wao hawafurahii kuuwawa Gaddafi eti siyo utamaduni! Ilihali aliuwawa kwa misimamo yake ya KULINDA WIZI WA RASLIMALI ZA WATU WAKE KWENDA MAGHARIBI, NA NDIYO MISINGI ALIYOWAJENGEA WATU WAKE.

Na ukiangalia chama kama CHADEMA pia kinahubiri kulinda na kutumia raslimali za nchi kwa manufaa ya watanzania na ndiyo maana CDM wamekuwa wakiomboleza kila mara waTZ wanapoumizwa na serikali kwa maslahi ya wazungu mfano NYAMONGO, BUZWAGI, GEITA, TULAWAKA.

CDM inawezaje tena kufananishwa na waasi walioingia kwa maslahi ya NATO.

WAnaJF naomba mchango wenu kwenye hili.
 
Hiyo ndiyo haswaa SIASA mkuu!
Ishu si tukio la kuuawa Gaddafi, maana kitendo hiki kimetokeaa kama hatua ya mwisho kabisa ya regime yake, na haikupangwa kitokee!
Hivyo kusimamia kifo hicho kama mfano wa ubaya wa upinzani si sahihi!
Ishu ya Libya inatakiwa kuangaliwa kwa mapana na marefu yake, na kama inakubalika mtu akae madarakani kwa miaka 42, hata kama anagawa Megawati za bure kwa kila raia!
 
Wewe husomi hata vyombo vya habari, kuwa mdadisi bwana. Gadaffi kilichomuua ni muda mwingi wa kukaa madarakani. Ndiyo maana watanzania wanajiuliza hiyo ni sababu tosha ya kutoa uhai wa mtu?

Aidha matumizi ya majeshi ya magharibi ni sahihi?. Na hapo ndiyo suala la CDMA kufananishwa na waasi linaingilia kati kwa sababu waasi walianza kama wao , kwa nini tena jeshi la NATO?

Kumbe hata Maandamano ya kubeza kila linalofanywa na Serikali nchini mwetu yanaweza kuanzishwa na wazawa kumbe kuna wageni wako nyumba. Naunga mkono hoja. Tujihadhari siyo sisi tu tusio na itikadi yoyote bali hata wale watakao sukumwa kufanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya wachache
 
Hiyo ndiyo haswaa SIASA mkuu!
Ishu si tukio la kuuawa Gaddafi, maana kitendo hiki kimetokeaa kama hatua ya mwisho kabisa ya regime yake, na haikupangwa kitokee!
Hivyo kusimamia kifo hicho kama mfano wa ubaya wa upinzani si sahihi!
Ishu ya Libya inatakiwa kuangaliwa kwa mapana na marefu yake, na kama inakubalika mtu akae madarakani kwa miaka 42, hata kama anagawa Megawati za bure kwa kila raia!
Kwa hiyo suluhisho ni kumuua? kama ulimsikiliza msemaji wa NTC kule Libya alisema anachojua ni kwamba Gadaffi alikamatwa akiwa hai ila kifo kimetokeaje hawajui na kwamba watafanya uchunguzi. Nadhani wamegundua kuwa wazungu wamewaingiza choo cha kike , hawakutarajia kuwa Gadaffi angeuawa. Kuna haja ya kujifunza kitu hapa , Tunapokubali kurubuniwa na hawa jamaa kufanya vurugu zisizo za msingi katika nchi zetu tutambue kuwa siku zote malengo yetu na yao si sawa. Na kwa nini hoja kwao siku zote inakuwa raslimali za taifa? Wanajua wazi wazi kuwa watakuwa na uwanja mpana wa kuzitawala. Mbona Somalia hawakwenda?
 
Viongozi wetu wa kiafrika ndio wao wanatengeneza mazingira yakuwapa nafasi nchi za magharibi kuwanyonga kutokana matendo mabaya wanayotendea wanainchi mfano mtu anakaa madarakani miaka 42 utadhani nchi yake milele.
 
Siasa za Tanzania ni ngumu kwa sababu wananchi wengi hawana upeo mkubwa hivyo hulaghaiwa kiurahisi.
kuifananisha ishu ya Libya na Chadema ni ujinga uliopitiliza.
 
Kwa hiyo suluhisho ni kumuua? kama ulimsikiliza msemaji wa NTC kule Libya alisema anachojua ni kwamba Gadaffi alikamatwa akiwa hai ila kifo kimetokeaje hawajui na kwamba watafanya uchunguzi. Nadhani wamegundua kuwa wazungu wamewaingiza choo cha kike , hawakutarajia kuwa Gadaffi angeuawa. Kuna haja ya kujifunza kitu hapa , Tunapokubali kurubuniwa na hawa jamaa kufanya vurugu zisizo za msingi katika nchi zetu tutambue kuwa siku zote malengo yetu na yao si sawa. Na kwa nini hoja kwao siku zote inakuwa raslimali za taifa? Wanajua wazi wazi kuwa watakuwa na uwanja mpana wa kuzitawala. Mbona Somalia hawakwenda?

Pole kama kweli unafikiri viongozi wa waasi wamechukizwa na jinsi Gaddafffi alivyouawa. Hizo ni politics tu katika kutimiza malengo yao huku wakicheza na akili za wenye kumeza mambo bila kutafakari. Ukitumwa kumleta hasa muuaji wa Gadaffi utamkamata nani: mzungu? Viongozi wa NTN, au aliyemalizia kumpiga risasi? Tafakari!
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..
 
Kaka nini maana ya mroho wa madaraka .Huyu mroho wa madaraka yukoje labda tuanzie hapa naomba mnisaidie kuelewa neno hili kwa kweli ili niingie kwenye mjadala .
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..

nakushauri kapimwe akili haraka
 
Kuwa mpinzani siyo kupinga kila serikali iliyoko madarakani.Kufanya hivyo ni uzuzu.Sio kila chama cha upinzani pia kinakuwa kwenye harakati kwa maslahi ya wananchi wake na Africa kwa Ujumla.

Kwa mfano mimi nimekuwa nikipenda harakati za MMD wakati Levy Mwanawasa Anagombea nimekuwa nikivutwa sana na sera zake na hata alipokuwa madarakani ingawa mara nyingi nimekuwa sipendi status quo nilijikuta bado nikitamani ashinde awamu ya pili ya Urais Zambia.Hata hivyo katika uchaguzi uliofuata baada ya Mwanawasa kufariki nimekuwa nikivutiwa sana na sera za michael Sata against sera na mfumo wa kusimamaia raslimali za wazambia uliosimamiwa na Rupiaha Banda wa chama kile kile cha MMD.Sasa kwenye siasa ni suala la kuangalia Angle zote za ideas

Ndiyo maana kuna watu kwenye mitandao wamefikia hataua ya kuchukulia mambo vibaya na au hata watu kuchukulia tofauti unaposema kitu kinzani na jinsi walivyotegemea iwe.Ukiwa mwanasiasa au chama cha siasa chenye kutoa mawazo huru bila unafiki utapata shida kweli kweli,na inapaswa kuwa hivyo.

Kwa mfano pamoja na kwamba napenda Demokrasia(ingawa Demokrasia hii ya Magharibi inahitaji mjadala) lakini mimi binafsi nawaona NTC kama vibaraka na fedheha ya Afrika.Gaddafi atabakia kuwa shujaa wangu.

Zimbabwe chama cha Upinzani cha MDC nakiona fedheha nyingine ya Afrika.comrade Mugabe anabakia kuwa shujaa wangu.Huko Uganda mimi naendelea kumuona Museveni kama kiongozi Muhimu na mwanamapinduzi aliyefanikiwa kwa kiwango kikubwa inagawa si kwa asilimia zinazotakiwa kwa wanamapinduzi wa kweli kwa ajili ya uganda na kwa Africa.Hata hivyo Museveni ametia aibu kuruhusu operation ya Kumtafuta kony kuwa assisted na America,hiyo ni Embarassment.Si kila serikali ilyoko madarakani ni mbaya,haramu na si kila chama cha upinzani ni haramu au halali katika muktadha wa mapinduzi au maslahi kwa wananchi.tunahitaji mijadala mikali zaidi ya hii.........na hasa dhana ya democracy katika western Model kuwa imposed Africa!
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..

Ndugu,

Unapolinganisha waasi wa Libya na Chadema unatukana.......!
 
Hiyo ndiyo haswaa SIASA mkuu!
Ishu si tukio la kuuawa Gaddafi, maana kitendo hiki kimetokeaa kama hatua ya mwisho kabisa ya regime yake, na haikupangwa kitokee!
Hivyo kusimamia kifo hicho kama mfano wa ubaya wa upinzani si sahihi!
Ishu ya Libya inatakiwa kuangaliwa kwa mapana na marefu yake, na kama inakubalika mtu akae madarakani kwa miaka 42, hata kama anagawa Megawati za bure kwa kila raia!
mkuu mimi nitofautiane na wewe kidogo,
Ni bora ya udictator wa Gaddafi mara 100 kuliko demokrasia ya ccm.
Kama udikteta utatupatia maji bure, elimu bure, afya bure, miundombinu bora, umeme bure na kwa upande mwengine demokrasia ikakuchaji kwa bei ya ajabu hivyo nilivyovilist utachagua kipi? funguka macho mkuu.
Niambie kipindi cha nyerere kulikuwa na demokrasia gani na misifa yote mnayompa? Tv yenye imeanzishwa kipindi cha mwinyi. Tanganyika nzima ni nyerere (&co) tu ndo alikuwa na tv pale ikulu. Hakuna vyombo huria va habari na mengine mengi. Haya mambo yaangalie kwa mapana yake.
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..

Myopic thinking, Je Gaddafi aliyeitawala Libya kwa miaka 43 na kuifanya Libya "shamba" lake,
na badaye kumtaayarisha mwanaye Seif Islam kurithi madaraka ya nchi, yeye siyo mroho wa
madaraka (BTW kinyume cha mroho ni nini?)

Je CCM inayochakachua matokeo ya general election in order to cling on power, kama huo
sio uroho wa madaraka ni nini?

Peleka huko CCM indoctrine za mwaka 47. Gaddafi alikuwa na choice hata kama amefanya mazuri kiasi
gani kama watu anao waongoza wamemkataa basi alikuwa na hiari ya kuondoka, likewise CCM, hata
kama imefanya mazuri (kama yapo) Kama watanzania tumewachoka na hatuwataki they have to listen na
kufungusha virago, that is what we call democracy dude!
 
nakushauri kapimwe akili haraka

umeniwahi mkuu, nilitaka kumshauri INAUMA aende hospitali kupima akili au Tumpeleke MILEMBE DODOMA.
cdm wangekuwa na uroho wa madaraka 2010 wangeingia barabarani baada ya kuchakachuliwa na magamba. Pili NTC wameshirikiana na nchi za magharibi kumuuwa general GADAFFI wakati CDM inashirikiana na wananchi kuwaondoa mafisadi. Mpaka hapo hujaona tofauti yao?
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..

Angalau nimekufahamu undani wako. Sishangai kwa kuwa upo kwenye pay list ya CCM. Unazi ni kupigania usichokiamini, bali unachofaidika nacho. Wewe ni mnazi. Hebu tuangalie nani ni mroho wa madaraka kati ya CCM na CHADEMA.

1. Wakati wa uchaguzi mkuu JK alitoa ahadi kama rais, zinazokadiliwa kufikia shilingi trilioni 90 (kinyume cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 aliyoisaini kwa mbwembwe ikulu). Dr. Slaa aliahidi elimu bure (Mwl. Nyerere alifanikiwa), Kupunguza kodi kwenye vifaa vya ujenzi (Kwa kubadilishana na kodi kwenye madini), kati ya hawa watu wawili ni nani alikuwa na uchu wa madaraka?

2. Mpaka leo CCM haijasema ilitumia kiasi gani cha pesa za kampeni zake hizo na jinsi walivyozipata (kinyume na sheria ya uchaguzi), CDM wameishatoa. Chama gani hapa kina uchu wa madaraka?

3. Tume ya uchaguzi ilituhumiwa kutumiwa na JK kupindisha matokeo (Tume haikupinga wala usalama wa taifa), kiasi kwamba toka uchaguzi kupita na tume kumtangaza JK mshindi, tume hiyo haijui alishinda kwa kura ngapi (rejea matokeo ya moshi vijijini, Geita, Musoma vijijini na kwingine ambako tume ilijikanyaga kwa kutoa matokeo mara mbili). Nani mwenye uchu wa madaraka?

4. Uchaguzi wa Igunga, CCM ilitumia Sh. bilioni tatu kupata jimbo moja tu na mbunge mmoja (Haijakanusha). Pia ilituma mawaziri wake kutoa ahadi za kiserikali (sheria wametunga na kupitisha wenyewe), Refer Ahadi za waziri wa ujenzi kujenga madaraja n.k.

Walirusha risasi za moto, walitishia watu kwa bunduki (Rage), walitumia vikosi vya kijasusi waziwazi (Green Guards), walijeruhi, wameuwa, wamenunua shahada za watanzania masikini ili tu wawanyime fursa ya kupiga kura, wametumia Polisi kupindisha sheria (kununua shahada ati si kosa la jinai), wamegawa mahidi, sukari, nguo, pesa mchana kweupe (TAKUKURU walizima simu zao, Polisi waliwabambikiza kesa za unyang'anyi raia wema walioripoti uhalifu huo), nani hapo mwenye uchu wa madaraka.

4. Raia huru wameuawa Mbarali, Tarime, Nyamongo, Juzi juzi tu Geita woote hao wameuawa na CDM? Arusha ni CDM waliokuwa na Bunduki? Hivi ninyi mmekuwa wanyama kiasi cha kusahau hata ahadi za chama chenu "Ati binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni Moja"
 
Mwalimu Nyerere aliuchukia sana ubepari akasema "UBEPARI NI UNYAMA". Pia wale wanao ukumbatia ubepari ni wanyama kama ubebari wenyewe, kwa kauli thabiti kabisa "UCCM NI UNYAMA"
 
Kumbukeni kuwa NTC walitangaza zawadi nono kwa atakaetoa taarifa za kukamatwa gadafi akiwa hai au mfu.pili huwezi kutenganisha waasi wa libya na chadema...wote hawa ni waroho wa madaraka ambao wako tayari kuua ili waingie madarakani..

Umeshaanza kuweweseka tena!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom