Ukiwa mnyonge Tanzania...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nani atakusemea?
Nani atakutetea?
Nani atakulilia?
Nani atakhsimamia?
Nani atakuulizia?

Utanyang'anywa ardhi yako!
Utahamishwa kwa nguvu toka ardhi ya wazazi wako!
Kiwanja chako kitauzwa kwa mwingine

Utabaki unahangaika kufuatilia ofisi hadi ofisi
Nani atakutetea unapopigwa virungu?
Wanapokuja na kukuambia 'ondoka' nani utamuuliza nani 'kwa nini?'

Na wakikutoa uhai wako kwa nguvu nani atasimama na kudai haki yako?
 
Katiba inazungumzia suala la EQUALITY i.e Haki ya Usawa; Je Haki ya Usawa maana yake ni Right of EQUALITY or Right to EQUALITY? Kipi ni muhimu zaidi, hasa katika kunyanyua wanyonge?
 
I prefer a wholesome and complete equality, hasa mbele ya sheria.
 
Mkuu umesahau kuwa kuna chama cha wakulima na wafanyakazi!!

Tumaini la wanyonge.
 
Unanifanya nimkumbuke Mwangosi,maskini kishasahaulika.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hii katiba si ipo siku zote????
Imemsaidiaje mnyonge??????

Katiba inazungumzia suala la EQUALITY i.e Haki ya Usawa; Je Haki ya Usawa maana yake ni Right of EQUALITY or Right to EQUALITY? Kipi ni muhimu zaidi, hasa katika kunyanyua wanyonge?
 
Katiba inazungumzia suala la EQUALITY i.e Haki ya Usawa; Je Haki ya Usawa maana yake ni Right of EQUALITY or Right to EQUALITY? Kipi ni muhimu zaidi, hasa katika kunyanyua wanyonge?

Mchambuzi katika kunyanyua wanyonge 'Right to EQUALITY' ndio mpango mzima (IMO)... But then again ukilifikiria sana hivi ikiwa yoyote kati ya hizo likisimamiwa vema si lolote laweza faulu?
 
Mbaya zaidi ni kuwa wengi wa wanyonge hao hao wanapo ushinda huo 'unyonge' na kuwa na uwezo wa kuweza pata haki yao; wanasahau walikotoka na walokuwa wanyonge wenzao.

da AshaDii, usisahau kwamba wengi wa watu wanaojitokeza kusema ni watetezi wa wanyonge huwa na maneno matamu yenye kutia matumaini ilihali nafsini mwao wanajijua kwamba ni wafariji wataabishaji.

natamani kama tungeweza kuujua moyo wa mtu, kiukweli wengine kabla ya kusimama mbele yetu kuongea tungekuwa tumekwisha waambie wasiongee.

lakini pia tunasahu kwamba, unyonge tunaukubali sisi wenyewe, kwa kupenda kutumika kwa aujaira usokuwa na tija. angalia wanafunzi wetu wa vyuo wanamaliza lkn hawajui ajira wapate wapi wala mazingira ya kujiajiri hayapo. angalia viwanda vyetu havimtegemei kijana wa tz ya leo na wala usomi wa kijana huyu hauna manufaa kwa kijana huyu. inasikitisha sana kijana anakuwa mtumwa ilihali alitegemewa awe msaidizi wawazazi wake waliao aduni kwa umaskini na kutokusoma.

vijana ambao hawajasoma hawa ndio kabisa wanatia huruma na wachache wanaojua biashara wanawatumia hawa kupata hela na kuwaacha kwenye umaskini uliokithiri. na hakuna anayeweza kukemea haya......... too sad
 
Last edited by a moderator:

or else wanawanyonga wanyonge wenzao kwa bidii, kama vile wanacompensate pumzi waliyoinyimwa kitambo. Mnyonge akitoka anawajua wanyonge wenzie kuliko yoyote, anajua pa kuminya!
 
Mchambuzi katika kunyanyua wanyonge 'Right to EQUALITY' ndio mpango mzima (IMO)... But then again ukilifikiria sana hivi ikiwa yoyote kati ya hizo likisimamiwa vema si lolote laweza faulu?
Mchambuzi na AshaDii mnaongelea right to equability ama right for.....kwa watu gani?? je utaliongelea hilo kwa watu wenye uchu wa utajiri?? je utalisemea hilo kwa watu ambao wanapenda kuwa juu zaid waitwe mabwana na wengine wakiwa watumwa kwake?? tusijidanganye ukombozi wa mnyonge haupo kwenye usawa bali upo kwenye utash wake.
 
Last edited by a moderator:
...Na hapa tunapotoa mawazo yetu, kuna viongozi hapa wameshafanya utafiti wa sehemu ya kuuza, na sasa wamekaa mezani na 'wawekezaji', wanapatania ardhi. Aidha washapanga kutumia jeshi la polisi kwatishia kuwaua wahusika. Ooh mnyonge!!
 
Nani atakusemea?
Nani atakutetea?
Nani atakulilia?
Nani atakhsimamia?
Nani atakuulizia?

Utanyang'anywa ardhi yako!
Utahamishwa kwa nguvu toka ardhi ya wazazi wako!
Kiwanja chako kitauzwa kwa mwingine

Utabaki unahangaika kufuatilia ofisi hadi ofisi
Nani atakutetea unapopigwa virungu?
Wanapokuja na kukuambia 'ondoka' nani utamuuliza nani 'kwa nini?'

Na wakikutoa uhai wako kwa nguvu nani atasimama na kudai haki yako?

Hii habari naifananisha na habari za Jehanam (kwa wale wa imani). Once ukiingia humo ni kilio na kusaga meno - hakuna cha Bw. Yesu wala Mtume wakati huo. Kile kipindi cha neema na toba kinakuwa kimepita; ni kilio na kusaga meno for ever and ever. Lucifa na wafuasi wake wakimtenda kila aliyeko humo jinsi wapendavyo bila utetezi au msaada wowote. Habari Njema na Maandiko Matakatifu yakiwa yamekwisha kupita.

Naiona nchi yetu ikiwa na uelekeo huo, mwenye nguvu ndiye atakayekuwa (na wamekwisha kuwa) na haki. Mnyonge hatakuwa na mtetezi wakitutenda wapendavyo wao.
 
usalama wetu tukivamiwa na majambazi na vibaka nani atatulinda na kututetea? Polisi? hapana.... BIG NO... they are killing us.
 
Mbaya zaidi ni kuwa wengi wa wanyonge hao hao wanapo ushinda huo 'unyonge' na kuwa na uwezo wa kuweza pata haki yao; wanasahau walikotoka na walokuwa wanyonge wenzao.

CASE STUDY: Le Mutuz
 
da AshaDii, usisahau kwamba wengi wa watu wanaojitokeza kusema ni watetezi wa wanyonge huwa na maneno matamu yenye kutia matumaini ilihali nafsini mwao wanajijua kwamba ni wafariji wataabishaji.

natamani kama tungeweza kuujua moyo wa mtu, kiukweli wengine kabla ya kusimama mbele yetu kuongea tungekuwa tumekwisha waambie wasiongee.

lakini pia tunasahu kwamba, unyonge tunaukubali sisi wenyewe, kwa kupenda kutumika kwa aujaira usokuwa na tija. angalia wanafunzi wetu wa vyuo wanamaliza lkn hawajui ajira wapate wapi wala mazingira ya kujiajiri hayapo. angalia viwanda vyetu havimtegemei kijana wa tz ya leo na wala usomi wa kijana huyu hauna manufaa kwa kijana huyu. inasikitisha sana kijana anakuwa mtumwa ilihali alitegemewa awe msaidizi wawazazi wake waliao aduni kwa umaskini na kutokusoma.

vijana ambao hawajasoma hawa ndio kabisa wanatia huruma na wachache wanaojua biashara wanawatumia hawa kupata hela na kuwaacha kwenye umaskini uliokithiri. na hakuna anayeweza kukemea haya......... too sad

Gfsonwin… Hapa tulipofika haitakiwi ujenge trust ya asilimia 100 kabisa kwa viongozi. Ndio maana kwangu mimi viongozi woote ambao wanawakilisha wanawakilisha/wanania ya kuwakilisha wananchi huwa naona wote wapo sawa kasoro huwa mmoja aweza kuwa in power na mwingine not in power… Ama tofauti nyingine yaweza kuwa mmoja kapata bahati ya kuwakilisha na tushaona uchemfu wake na mwingine anakuwa hajapata bado bahati ya kuwakilisha hivo bado anakuwa hajaonesha uwezo ama uchemfu wake. Katika viongozi kuna tu ile yupi ni mlaji lakini walau anajali pia maslah ya wananchi?

Wasomi unaweza watazama vyoyote vile mtu aamuavyo. Ila kumbuka kuwa the so called wasomi mara nyingi ndio wameonesha na kudhihirisha kuwa ni adui kubwa wa ‘Mnyonge'. Kumbuka kuwa Kiongozi wa leo ni msomi wa jana na juzi, msomi wa leo ndio kiongozi wa kesho na keshokutwa… But still HAKUNA hope kuwa kuna uwezekano wa a better Tanzania ya Wanyonge.
 
Mchambuzi na AshaDii mnaongelea right to equability ama right for.....kwa watu gani?? je utaliongelea hilo kwa watu wenye uchu wa utajiri?? je utalisemea hilo kwa watu ambao wanapenda kuwa juu zaid waitwe mabwana na wengine wakiwa watumwa kwake?? tusijidanganye ukombozi wa mnyonge haupo kwenye usawa bali upo kwenye utash wake.

So far mimi naona kuwa moja ni bora ya nyingine... Ila whatever the case, yoyote ambayo ingekuwa hapo ingepewa kipaumbele kungekuwa na unafuu kwa wanyonge. Sijaelewa kuwa Mchaumbuzi analiangalia kivipi... Nasubiri atae ufafanuzi kama hatojali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom