Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Nani atakusemea?
Nani atakutetea?
Nani atakulilia?
Nani atakhsimamia?
Nani atakuulizia?
Utanyang'anywa ardhi yako!
Utahamishwa kwa nguvu toka ardhi ya wazazi wako!
Kiwanja chako kitauzwa kwa mwingine
Utabaki unahangaika kufuatilia ofisi hadi ofisi
Nani atakutetea unapopigwa virungu?
Wanapokuja na kukuambia 'ondoka' nani utamuuliza nani 'kwa nini?'
Na wakikutoa uhai wako kwa nguvu nani atasimama na kudai haki yako?