Ukiwa mdadisi usiangalie taarifa za habari kupitia TV za Tanzania

Polisi

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,082
639
Wakuu leo sikuwa busy sana na hivyo nikaona ni fursa muafaka kukaa na my wife kuangalia taarifa ya habari. Kuna mambo mawili yamenishtua kidogo na nikawa najiuliza lengo hasa la taarifa ya habari ni nini?
Jambo la kwanza ni la mwandishi wa ITV kumuhoji mhe. Prof. Mwandosya juu ya uvumi kuwa amefariki dunia. Aliuliza hivi 'Mhe. Mwandosya kuna uvumi kuwa umefariki dunia, unaweza kuwaambia nini watanzania?' Tatizo langu: Je mwandishi alitaka ku confirm kama mwandosya amefariki kutoka kwa mwandosya mwenyewe?
Nikaendelea kukodolea macho TV. Nikamsikia mhe. Nape na kauli hii: 'Tanzania ina wenyewe, na wenyewe ni CCM'. Nikajiuliza, hivi kweli nape alidhamiria kuongea neno hilo?
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI JAMIIFORUMS
 
ya mwandosya mkuu umeua. Khaaa, hivi kwa nini namimi sikujiuliza hili la mwandosya, maana wakati anamuuliza kwa simu saa 12 jioni nilimsikia live. Aisee uko makini mkuu, mweeee!
 
Hivi ndivyo tasnia ya habari ilivyo hapa Tanzania, ukitaka kupata kichefuchefu mwite mwanahabari mpe habari yako kisha kesho angalia kilichooandikwa.
 
Kama waandishi wa habari ni kioo cha jamiiTZ basi tumekwisha
 
Tatizo mwandishi wa tz akitoka shule na cheti chake anaingia kazini na kuanza kuandika habari bila kupewa mafunzo maalum na wanahabari mashuhuri/wazoefu. Usitarajie kama kuna semina fupi ya kuwafunda wanahabari ili wawe bora, sidhan kama hii kitu kipo(semina).
 
Nimeipenda ID yako ingawa unaongoza kwa kula rushwa
Mkuu, polisi wanaongoza kwa kushawishiwa kupokea hongo. Hakuna polisi mwenye ubavu wa kula rushwa. Rushwa wamekula akina RA, EL, na ....na . nadhani wawajua
 
Ni sawa na unaongea na mtu live kisha unamuuliza' hivi wewe ninayeongea nawe umekufa au mzima?'

Nakwambia jana mimi nilibaki mdomo wazi. Ningekuwa mimi ningemwambia ' ni kweli mtangazaji nimekufa, nione atasemaje'. Te. te
 
Alaf kitu kingine ni kwamba, mwandishi anayemhoji mtu lazima awe na capacity kubwa ya reasoning kichwani mwake, kama mwandishi reasoning yake ni ndogo ndo kama hivyo iliyomtokea Mwandosya!

Ni aibu yaaani!
 
Jambo la kwanza ni la mwandishi wa ITV kumuhoji mhe. Prof. Mwandosya juu ya uvumi kuwa amefariki dunia. Aliuliza hivi 'Mhe. Mwandosya kuna uvumi kuwa umefariki dunia, unaweza kuwaambia nini watanzania?' Tatizo langu: Je mwandishi alitaka ku confirm kama mwandosya amefariki kutoka kwa mwandosya mwenyewe?

waandishi wengi ni failures as waalimu, na waafrika ni wavivu wakutafuta maarifa mengine ili kujiweka fiti kwenye professional
 
Alaf kitu kingine ni kwamba, mwandishi anayemhoji mtu lazima awe na capacity kubwa ya reasoning kichwani mwake, kama mwandishi reasoning yake ni ndogo ndo kama hivyo iliyomtokea Mwandosya!

Ni aibu yaaani!

Kweli kabisa mkuu. ile issue ilikuwa nyeti na ilitakiwa ahojiwe na senior journalist mwenye capacity kubwa ya reasoning. Taarifa kama ile ikiwa mislead inaweza kuleta maumivu makubwa kwa baadhi ya watu mioyoni
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom