Ukiwa mchungaji kanisani Nigeria, utajiri nje nje

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Uchunguzi uliofanywa nchini Nigeria umebaini kuwa wachunga kondoo wa Bwana nchini humo mbali ya kuhubiri neno la bwana wanatengeneza pesa ya maana kiasi cha kwamba baadhi yao
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Muandishi wa Nigeria wa jarida la Marekani la masuala ya uchumi, Forbes, wahubiri wa neno la bwana nchini Nigeria wanatengeneza pesa sana kutokana na uchungaji kiasi cha kufanananishwa na matajiri wa biashara ya mafuta.

Mfonobong Nsehe akitoa ripori ya uchunguzi wake alisema kuwa wachungaji wa Nigeria wanaishi maisha ya kifahari na wana miradi mikubwa ya kibiashara.

"Kuhubiri ni biashara inayolipa sana, sawa sawa na biashara ya mafuta", alisema Nsehe.

Utajiri wa wachungaji watano maarufu nchini Nigeria unakadiriwa kufikia dola milioni 200, alisema Nsehe.

Makanisa mengi yameibuka nchini Nigeria na waumini wamekuwa wakiongezeka.

Nsehe alisema kuwa mchungaji tajiri kuliko wote ni Mchungaji David Oyedepo wa kanisa la Living Faith World Outreach Ministry, ambaye utajiri wake ni dola milioni 150.

Mchungaji Oyedepo ndiye anayeshika nafasi ya pili akimiliki ndege nne, kampuni ya uchapishaji, chuo kikuu na shule moja na majumba ya kifahari jijini London na Marekani.

Mchungaji Chris Oyakhilome wa kanisa la Loveworld Ministries ana utajiri unaokadiriwa kuwa kati ya dola milioni 30 na 50. Mchugaji Oyakhilome anamiliki kampuni ya magazeti na majarida, stesheni ya televisheni, hoteli na kampuni ya majumba.

"Wachungaji hawa wanaishi maisha ya kifahari utawaona kwenye ndege zao binafsi na magari ya kifahari", alisema Nsehe.

Wachungaji wengine walioingia kwenye listi ya utajiri ni mchungaji Temitope Joshua Matthew mwenye utajiri kati ya dola milioni 10 na 15, Mchungaji Matthew Ashimolowo dola milioni 6-10, na mchungaji Chris Okotie mwenye utajiri kati ya dola milioni 3-10.

Nsehe aliongeza kuwa wawakilishi wa wachungaji wote isipokuwa mchungaji Ashimolowo, wamethibitisha taarifa ya umiliki wa mali za wachungaji hao.

wanamiliki ndege, hoteli na biashara kubwa.
 
Zama za ubepari.....hata dini ni BIASHARA.....
KUNA KIPINDI ILIWAHI KURIPOTIWA TOKA ,MBEYA KUA KUNA BAADH YA WACHUNGAJI WANALAZIMIKA KUTUMIA HIRIZ ILI KUITA WAUMINI!!!!!!!
SO DINI INALIPA
 
Zama za ubepari.....hata dini ni BIASHARA.....
KUNA KIPINDI ILIWAHI KURIPOTIWA TOKA ,MBEYA KUA KUNA BAADH YA WACHUNGAJI WANALAZIMIKA KUTUMIA HIRIZ ILI KUITA WAUMINI!!!!!!!
SO DINI INALIPA
a
acheni kuwafuata fuata watumishi,nadhani huduma yao inafaida kwa wengi duniani sasa huyu jamaa anataka watumishi wawe maskini? heri maskini wa roho maana ufalme wa mungu ni wao, imeandikwa watumishi wa bwana watkula madhabahuni
msitizame walipo tazamani pia walipoanzia.
 
Kama Wachungaji kazi yao ni kuhubiri neno la Mungu aliye hai. Mungu wanaye mhubiri hao wachungaji ni Tajiri. Mungu huyo huyo ndie aliye wapa hao wachungaji kazi, sasa unategemea wafanyakazi wa Mungu ambaye ni tajiri na kaumba dhahabu na almasi wawe MASKINI? Sasa huo utakuwa mfano gani kwa waumini? Please JF let us be real na tutumie akili yetu kamili na sio kufuata mkumbo.

Kama Yesu Kristo tu katika huduma yake ya miaka mitatu alikuwa na accountant, what does it tell you? Was Jesus Poor? Huyo Judas accountant/mweka hazina alikuwa anaweka nini kama si FEDHA?

People read the Bible in its own context na acheni ushabiki msio uweza au juwa.

MaxShimba, A friend of God and A Bondservant of Jesus Christ
 
Back
Top Bottom