Ukiwa mbunge Tanzania hutaweza kuwa rais mzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiwa mbunge Tanzania hutaweza kuwa rais mzuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwananthropolojia, Oct 8, 2012.

 1. mwananthropolojia

  mwananthropolojia JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 954
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Rais mzuri ni yule mwenye maono,dira, mipango na mikakati ya namna ya kuitekeleza mipango yake ambayo yanaendana na dira na maono ya anapotaka tufike, na si hayo tu, rais mzuri pia ni mtekelezaji na msimamiaji wa mipango iliyowekwa bila kuyumbishwa na siasa za upepo ambazo zinaweza kumpotezea dira aliyojiwekea pamoja na wananchi wake kufika.

  Nasema wabunge wetu wa tanzania hawawez kuwa marais wazuri kutokana na kazi wanazofanya kama wabunge hapa Tanzania ,nimekuja kugundua kazi kubwa ya wabunge wetu ni kuwakilisha mawazo ya wananchi ambao wamewatuma ,hawana dira yao wenyewe,kazi yao nyingine ni kupoint kwenye madhaifu tu bila kuwa na nguvu yoyote ya utekelezaji kwani hawana mafungu yao wenyewe ya kutosha kwenye majimbo yao.

  Pesa zinazoenda kwenye halmashauri mara nyingi mbunge anakua hana sauti kuu ya kuzisemea, kuzisimamia na kuzitumia kwa mipango na mikakati aliyokuwa amepanga kuitekeleza kwa ajili ya wananchi wake. Atakutana na madiwani ambao nao watakua wanapigania maslahi ya majimbo walikotokea,

  Wakurugenzi wa mji ambao nao wana mipango yao tofauti ya maendeleo ya mji na vipaumbele tofauti huku naye mkuu wa wilaya akiwa na ajenda zake alizotumwa na rais au binafsi ili aweze kuendelea kubaki katika nafasi aliyopewa na ikiwezekana kupunguza ushawishi wa mbunge.

  Kutokana na hali hiyo nini kinachowatokea wabunge wetu?

  Moja anaishia kubwabwaja sana akiwa bungeni kuhusu matatizo ya jimboni mwake,ataorodhesha msururu wa matatizo huku akijua hilo fungu litakalotoka inabidi ligawanywe tena likifika kwenye halmashauri, kutokana na tofaut ya vipaumbele kati yake na wabunge wenzake ambao kuna uwezekano wakawa wanagawana halmashauri,mkurugenzi wa mji, madiwani na mkuu wa wilaya kwa maana nyingine pesa hazitatoshah, alafu ajenda zake nyingi zisipopitishwa kutokana na udogo wa fungu atasema ni kosa la serikali au halmashauri kwani wananchi wote tumemuona bungeni na kwenye halmashauri alivyovimba hata kufikia hatua ya kupinga bajeti

  Pili anaanza kujenga tabia za mazoea ya kusema uongo mbele za wananchi wake kwa miaka 5 mfululizo ,ni miaka mingi sana ya kuulizwa maswali yaleyale na wananchi wako kiasi ambacho inamjengea usugu kazini na anakua mtaalamu hasa aliyebobea katika fani ya ulaghai na mbaya zaidi kama ana miaka zaidi ya mitano bungeni atakua muumini mzuri wa ulaghai na ghiliba za kisiasa

  Tatu kazi yake kubwa itakuwa kufanya mikakati na kazi za dharura ama matatizo ya dharura ya jimbon mwake na kujijengea tabia na akili za dharura au zimamoto ambazo zitamjengea umaarufu unaoweza kumrudisha tena bungeni kwa awamu nyingine na kusahau kazi ngumu za urais za kila siku za utendaji ambazo kila dakika na masaa ni dharura kwani mipango ni mingi,pesa zipo nyingi za utekelezaji na usimamiaji wa miradi ya maendeleo kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni

  Kwa staili hii ya uongozi wa wabunge wetu na vikwazo wanavyokutana navyo hakika akija kuwa rais maendeleo yataenda taratibu sana,kazi nyingi hazitaenda,usimamiaji utakuwa mdogo ama dhaifu sana,ataelemewa na mzigo wa kazi na kuamua kuteua mawaziri wengi na wasaidiz wengi wa kumsaidia kazi huku akishindwa kuwasimamia

  Kutokana na maisha ya uongo aliyokua akiishi bungeni ya kutoa ahadi nyingi na kushindwa kutekeleza kutokana na ufinyu wa bajet, atarudi tena na uongo uleule wa bajeti ni ndogo,wakati ukweli ni kwamba amevunja rekodi ya ukusanyaji mapato,wafadhili wametoa mafungu ya kutosha ya kuziba mianya yote ya bajeti, lakin bado atashindwa kusimamia utekelezaji wa mipango kutokana na ile PICHA KUBWA ya maendeleo kamili na dira ya anapotaka kwenda ilishampotea kichwani mwake siku nyingi alipokuwa mbunge

  Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini? njia na mbinu za kufikia maono yake ameshasahau ,kwani alishazoea kufanya kidogodogo na nusunusu, amesahau namna gani ya kuiweka mipango na mikakat kwenye utekelezaji kamili. Ndio utashangaa rais msomi lakin anashindwa kuitumia elimu yake katika kutekeleza mipango aliyojiwekea, kwani alishapoteza huo uwezo alipokuwa mbunge hata itafikia hatua ataishia kusema "sielewi kwanini Tanzania ni nchi maskini"

  Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayonifanya niamini ukishakua mbunge urais Tanzania haukufai ni bora tutengeneze nafasi za magavana ambao watakua wana nguvu karibia sawa na rais katika utekelezaji wa mipango na mikakati ya maeneo yao kwani hiyo itamjenga uzoefu wa kuwa na fungu la kutosha kugawa, kutekeleza na kusimamia maendeleo ya maeneo yao,hata akitaka urais tunapata picha halisi ya tunapotaka kwenda kama taifa sio wabunge hawa ambao tayari akili zao zimejiandaa kutudanganya na kufanya kazi nususnusu za maendeleo.

  SIJUI WADAU MNASEMAJE KWENYE HILI SUALA?
   
Loading...