Ukiwa kiongozi unaweza kuwa na nguvu na madaraka ya kunyamazisha watu, unapoona idadi ya wa kunyazishwa inazidi jiulize ni kwanini?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,268
Uongozi uko katika ngazi nyingi. Wengine walibahatika kuwa viranja shuleni, kapteni wa timu ya chandimu, kiongozi wa msafara, kiongozi wa jumuia ya kanisa nk.

Katika nguvu na mamlaka ya kiongozi ni kuwaambia watu wanyamaze kelele zikisidi. Hii ni moja ya sifa ya kiongozi kuweza kulidhibiti kundi la anaowaongoza.

Kiongozi akikosoa uwezo wa kudhibiti anaowaongoza basi hakuna haja ya kuwa na kiongozi.

Wakati huo huo kiongozi anahitaji hekima ya kujua chanzo cha kelele za kudhibiti. Kiongozi ukiona watu wa kuwanyamzaisha wanakuwa wengi au kelele za kudhibiti zinazidi.

Jiangalie wewe kama kiongozi, ulikosea wapi?
 
Kiongozi anaejaribu kuwanyamazisha wananchi wake au kuziba masikio asiwasikilize huyo ni mtu hatari sana kwa sababu
1.Anawazarau wananchi wake
2.Anawaonea anaowangoza
3.Ni mwizi
 
Mafisadi Mlizoea kuishi bila kulipa kodi, lazima mbweke

Ila Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
 
Mafisadi Mlizoea kuishi bila kulipa kodi, lazima mbweke

Ila Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
Yule mropokaji na msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Huna lolote wewe, unachokifuata tunakijua. Huo ubwabwa sii ungeenda kwa Rungwe tuu?
IMG_20201011_074035.jpg
 
Back
Top Bottom