Ukiwa in teen ages tukio gani mzazi alikufanyia ukaona umeonewa na ukamchukia?

Duuh pole mkuu sasa ndoto yako inaishi au ilikufa kabisa.
Haikuwa ndoto yangu.. Ila nadhani ilikuwa ni peer pressure tu kwa wakati ule!! Maana ilikuwa kama huwezi kuzichapa na mtu inakuwa ngumu kupewa ushirikiano na wadau kitaani

Wengi waliojifunza Boxing waliishia kuwa wakabaji tu na waraibu wa madawa ya kulevya.
Mzee wangu nadhani aliona mbali ndo maana hakutaka kabisa nijihusishe na hayo mambo.

Kikubwa alichofanya aliniwekea ratiba ngumu sana kuanzia asubuhi nikienda shule kisha nikitoka shule naenda katika masomo ya ziada (tuition) mpaka jioni saa 12.. Weekend ilikuwa naenda kwa Babu yangu huko nje ya mji kidogo.
 
Kunipiga saaanaaa kila nikiongozana na wanafunzi wenzangu wa kiume, na kila mwanafunzi wa kiume atayejaribu kuongozana nami ikitokea ameonwa na mzazi wangu au kaka yangu nae anapigwa.

Kupigwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa, ilifika sehemu nikawa wakiongea nawasikiliza wanipige wamalize.

Ila walinisababishia niingie kwenye mahusiano mapema as niwe na sehemu ya kujifariji.
Means haikukusaidia hiyo adhabu au unajionaje kwa sasa.
 
Haikuwa ndoto yangu.. Ila nadhani ilikuwa ni peer pressure tu kwa wakati ule!! Maana ilikuwa kama huwezi kuzichapa na mtu inakuwa ngumu kupewa ushirikiano na wadau kitaani

Wengi waliojifunza Boxing waliishia kuwa wakabaji tu na waraibu wa madawa ya kulevya.
Mzee wangu nadhani aliona mbali ndo maana hakutaka kabisa nijihusishe na hayo mambo.

Kikubwa alichofanya aliniwekea ratiba ngumu sana kuanzia asubuhi nikienda shule kisha nikitoka shule naenda katika masomo ya ziada (tuition) mpaka jioni saa 12.. Weekend ilikuwa naenda kwa Babu yangu huko nje ya mji kidogo.
Ashukuriwe mzee.
 
Means haikukusaidia hiyo adhabu au unajionaje kwa sasa.
Adhabu bila kosa? Nadhani walidhani ndio njia ya kunilinda ila haikuwa sahihi as mimi nilikuwa najilinda na nilikuwa naogopa mno kuwa na tabia mbaya yeyote.

KWA sasa niko poa ila nimejifunza mtoto wa kike ili umlinde awe rafiki na uongee nae KWA uwazi otherwise unamuharibu
 
Vizuri sana.
 
Habari wana MMU.

Bila shaka sitakuwa nje ya content ya jukwaa nikisema mahusiano yangu na baba mzazi wangu wakati niko teen's ages yalinifanya niishi kwa wasiwasi sana nikijuwa nanyimwa haki na sipendwi na mzazi wangu hasa wa kiume.

Nakumbuka nilikuwa nishamaliza darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 15 siku moja nikaenda disco vumbi, kama kawaida kule kijijini kabla ya siku ya harusi huwa kuna siku kadhaa za burudani, hivo nikaamua kwa mara ya kwanza kushiriki na mimi hili kwanja nililokuwa nasimuliwa tu na wenzangu maana mimi mzee alikuwa hataki kabisa niende pamoja na matukio alioona yeye kama.mzazi sio size yangu.

Nikaondoka usiku huo bhana, ile narudi mida ya saa 6 usiku nanyata ile bila kishindo, nikashika kitochi (kurunzi) changu namlika hadi kitandani naona hakuna godoro.....duuuh.

Akili ikaruka,,,nikawaza nimeibiwa au !!! Kwa kuwa nilikuwa na wadogo zangu rooms nyingine nikawaamsha kuuliza nao wakashangaa!!

Kama ndani ya dakika 3 hivi mzee akaingia ndani,,,mbona nasikia kelele? Hamjalala tu? Mara akatupa jicho chumbani kwangu na akauliza godoro liko wapi......April26 kidogo mkojo upite maana mzee alikuwa mkoloni mweuzi kwa kichapo. Nikajuwa hapa lazima nilambe dadekii.

Nikajifanya namdanganya, baba nimetoka nje kujisaidia narudi nakuta godoro hamna, akauliza ,,,umetumia masaa mangapi kujisaidia,,,?? Mimi kimya.... Kumbe bhana keshaandaa na fimbo mbili kali hatari palepale nikaanza kukichezea kichapo!!

Kula stick kula fimbo kula ukuni hadi nikawa hoi.....aiseee.....mzee akasema ole wako siku nyingine urudie uone.

Kumbe bhana alikuja ndani hajanikuta akaamua kubeba na kupeleka ndani kwake na akawapiga bit madogo nikiuliza wajifanye hawajui....!!! Alisoma chezo tangu naondoka aliniona akanipotezea tu.

Baadae akanambia nenda fata godoro pale ,,,pumbavu wewe na iwe mwisho

Wakuu nilikaa kwa muda kama miezi 3 nikiwa kama mgonjwa wa akili,,,si unajuwa age hizo ndo za ku-question sheria,,,, why nipigwe mbona baba wa fulani hawapigi wanae na wengine nawazidi umri lakini wanaenda disco???

Basi bhana sikuwa na jinsi ikabidi nifate sheria. Nashukuru malezi yake yamenisaidia sana hadi sasa najibunia. Mzee wangu baba April26 nakutakia kila la kheri mzee wangu, msalimie na mama yangu. Amina.

EBU SEMA NA WEWE JAMBO GANI UNAAMINI KWA SASA HAPO ZAMANI ULIKUWA WRONG LAKINI ULIVOADHIBIWA ULIMIND SANA MZAZI WAKO.

Fafanua uliposema umechezea ukuni wajuba tunataka kuelewa vizuri
 
Adhabu bila kosa? Nadhani walidhani ndio njia ya kunilinda ila haikuwa sahihi as mimi nilikuwa najilinda na nilikuwa naogopa mno kuwa na tabia mbaya yeyote.

KWA sasa niko poa ila nimejifunza mtoto wa kike ili umlinde awe rafiki na uongee nae KWA uwazi otherwise unamuharibu
Nakumbuka kuna binti alipata mimba jirani yangu kisha akaenda kuitoa clinic za kitaa na kuishia kuharibiwa,kuugua muda mrefu mpaka kufa. Wakati anaumwa alinifungukia siku nimeenda kwao kumpa hi,,baba mkali,mama mkali vipigo kote mpaka aliogopa kusema home kwa ana mimba. Kama hata mmoja wa wale wazazi angekuwa rafiki lazima yule dada angekuwa hai mpaka leo. Wazazi tujitahidi kuwa close na wanetu ili wakipata matatizo tuwe kimbilio lao la kwanza .
 
Kpnd Niko Fom 3...mzee wangu wa kufkia alkua Anaokota mifuko ya viroba ,alaf anaileta na kuituma home...Badae anamwambia bi mkubwa kua mimi ni mlevi...
Duuh hii sasa kiboko !! Huyo angeweza hata kukuuwa sema alikosa mazingira tu.
 
Nakumbuka kuna binti alipata mimba jirani yangu kisha akaenda kuitoa clinic za kitaa na kuishia kuharibiwa,kuugua muda mrefu mpaka kufa. Wakati anaumwa alinifungukia siku nimeenda kwao kumpa hi,,baba mkali,mama mkali vipigo kote mpaka aliogopa kusema home kwa ana mimba. Kama hata mmoja wa wale wazazi angekuwa rafiki lazima yule dada angekuwa hai mpaka leo. Wazazi tujitahidi kuwa close na wanetu ili wakipata matatizo tuwe kimbilio lao la kwanza .
Mungu amrehemu huko aliko. Amina.

Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom