Salaam wana JF.
Kabla ya yote ningependa kuweka wazi kuwa mimi si mwanasheria bali ni "sayansi ya mambo ya uhai" (life sciences) kwahiyo sitaweza kunukuu vifungu vya sheria/katiba wala sherehe zake. Kwa maana hiyo basi, niko tayari kurekebishwa na pia natanguliza kuomba msamaha pale nitakapokosea.
Msingi wa mada yangu ni kauli za Rais Magufuli kwa CAG mpya katika hafla ya kumwapisha; alimuonya kuwa asidhani kuwa cheo hicho ni muhimili mungine wa dola kama ilivyo Rais, Spika au Jaji Mkuu. Bali alisisitiza kuwa CAG ni mdhibiti na mkaguzi tu wa matumizi ya fedha za serikali na mwenye serikali (anayetoa hizo fedha) yupo.
Kwa kauli hizi mbili tunapata picha kwamba CAG hasifanye makosa kwa kufanya ukaguzi bila maelekezo kutoka kwa "mwenye fedha zake" na kutuhumu au kuilamu serikali kuhusika na mapungufu yoyote atakayoyabaini katika ukaguzi wake. CAG akifanya hivyo itakuwa ni sawa na kujiona kuwa yeye ni muhimili wenye mamlaka ya kuituhumu mihimili mingine bali anachotakiwa ni kufanya ukaguzi wake kwa mujibu na maelekezo ya Rais au Spika na sio vinginevyo. Na CAG akikiuka maelekezo anaweza kung'olewa hata kabla ya kumaliza "fixed term of five year" kwa mujibu wa sheria.
Kwa mtazamo mungine Rais anamaanisha kuwa CAG hana kinga, mamlaka wala uhuru wa kutekeleza majukumu yake atakavyo labda kwavile mwenye hizo fedha sio yeye CAG bali ni Serikali na kwahiyo serikali tu ndo inaweza kuamua kufanyike ukaguzi au la.
Kwa maoni yangu, mtazamo huu wa Rais juu ya mamlaka, kinga na uhuru wa CAG hata kama vimeandikwa kwenye sheria si lolote si chochote mbele yake. Lakini anaposisitiza kwamba CAG si muhimili maana yake hatambui mamlaka, kinga wala uhuru alivyotunukiwa CAG kwa mujibu wa sheria. Kiufupi Rais anavunja sheria na katiba bali anajiona yeye yuko juu ya hivyo na huku ndo ile kujimwambafai aliosema JK.
Ingawa sijawahi kumsikia CAG Uttoh wala Assad akijinasibisha kuwa wao ni muhimili mungine, dhana hii ya CAG/NAOT kuwa muhimili nimeisikia mara nyingi ikiongelewa katika serikali za awamu zilizopita. Awamu hizo ndizo zilizoilea dhana hii. Lakini yatupasa tujiulize kwanini serikali za awamu zilizotangulia zilikuza dhana kwamba CAG/NAOT ni sawa na muhimili wa serikali? Kadhalika yatupasa tuelewe kwanini serikali ya awamu hii haitaki kusikia dhana hii?
Jibu ni moja tu; Serikali za awamu zilizopita zilikuwa zinaendasha nchi kwa kufuata utawala wa sheria. Marais waliopita walitambua mamlaka, kinga na uhuru wa CAG katika kutekeleza majukumu yake. Ukweli ni kwamba katika kumtukuza CAG kuna mantiki kubwa ndani yake ambayo Rais Magufulj haitambui aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Ingawa ni kweli kwamba Rais ndiye anayeteua CAG na kwamba anaweza kufanya uteuzi huo kwa muda wa kufumba na kumbua jicho (hakuna masharti magumu), bado kutengua uteuzi wake ni "shughuli pevu" kwa mtu anayeheshimu sheria na katiba ya nchi. Kutengua uteuzi wa CAG sio sawa kutengua Waziri, RC au Mkurugenzi wa taasis ya Serikali.
Mathalani, sheria inapoweka sharti kwa Rais kupata mwafaka/ridhaa ya Jumuia ya Madola kufanya uchunguzi (investigation) ndipo atengue aliyemteua maana yake CAG sio cheo chepesi kama Magufuli anavyochukulia. Lakini hii ndo mantiki au msingi wa kuheshimika kwa CAG hadi akaonekana kuwa ni muhimili mungine. Ni dikteta tu ndo asiyeweza kutambua na kuzuia Dhana ya CAG/NAOT kuwa ni Muhimili.
Asanteni.