'Ukiuza bidhaa Tsh 100,000, unakatwa kodi 18,000. Je, faida ni Tsh ngapi?'

Basi kuna tatizo mahali....kwenye risiti...mbona inakuwa kama VAT ya BEI ya bizaa + BEI ya bizaa (faida+mtaji)= na ela niliyotoa?
Lete sample ya risit yenye VAT Calculated nikuonyeshe
Bidhaa ziwe zinahusiana na mfano nilioutoa hapo juu
 
Kama hoja yako ni ya kweli nadhani kutakuwa na tatizo kubwa la utekelezaji wa hiyo kodi kwa wafanyabiashara wadogo,wasiokuwa maajenti wa Mali kutoka viwanda vikubwa.

Katika mfumo wa biashara kwa wenye maduka ya nusu jumla ambao mfuko wa ngano anapata faida ya Tsh 1000 unamwambia aweke 18%ataweza kuuza kweli hiyo Mali?
Au unamlazimisha afunge Duka lake na kutafuta kazi nyingine?maana kwa vyovyote serikali itamfilisi.
Usichokielewa hapo ni kwamba huyo muuzaji alipoinunua kiwandani tayari alilipia na VAT ndy maana akalipia 1180 (kwa mfano) kwa kiroba..sasa kosa linakuja ni kuongeza hiyo faida ya 100 kwenye 1180 ambapo akija akidaiwa kodi itamla mpaka mtaji...na hii inatokana na watu wengi kufanya biashara kimazoea kuliko kitaalam..maana hata kupanga bei ya bidhaa ni utaalam..

Wafanyabiashara wengi hawajui thamani halisi ya bidhaa yake anayoiuza. Wengi wanachojua ni ile bei waliolipia kununulia bidhaa tu, Mambo ya usafiri,uhifadhi,mishahara na posho,pango na kodi ndogondogo za jiji hawajui ni kiasi gani zinaathiri gharama katika kila bidhaa husika iliyomo dukani mwake....hapo ndiyo wanafeli
 
Mkuu hapo kwenye VAT Calculation zake haziko hivyo! Kuna fomula yake japo imenitoka kidogo ila sio kuwa 18%ya 12000 ni 2160!!wataalam watakuja.
Mkuu hebu angalia calculation za VAT hapo chini zilivyofanyika, nadhani nipo sahihi
Screenshot_2017-02-27-23-57-05.png
 
Kwaiyo 18000 itakuw refunded kwa mfanyabiashara bdae?
Mkuu itakuaje refunded na VAT hawatozi hivyo, VAT inatozwa katika cost ya bidhaa na sio katika selling price ya bidhaa, maana ukiweka selling price ya bidhaa tayar VAT imo!!
 
Kama hoja yako ni ya kweli nadhani kutakuwa na tatizo kubwa la utekelezaji wa hiyo kodi kwa wafanyabiashara wadogo,wasiokuwa maajenti wa Mali kutoka viwanda vikubwa.

Katika mfumo wa biashara kwa wenye maduka ya nusu jumla ambao mfuko wa ngano anapata faida ya Tsh 1000 unamwambia aweke 18%ataweza kuuza kweli hiyo Mali?
Au unamlazimisha afunge Duka lake na kutafuta kazi nyingine?maana kwa vyovyote serikali itamfilisi.
Jomba VAT haitozwi kwenye faida.
Ngoja nkuelekeze kwa huo mfano wako.
Kwa mfano huyo mfanyabiashara anauza bidhaa zake kwa jumla na faida ikawa hiyo1000/=, kwa kila mfuko, yeye hapo hakatwi VAT bali atatozwa INCOME TAX kama sio kampuni nimtu binafsi lakini kama ni kampuni watatozwa CORPORATE TAX(Naruhusu kurekebishwa kama ntakosea) na yenyewe ni 30%ya faida (naweza kukosolewa pia)
Lakini kwa makampuni yanayonunua na kuuza kuna mambo ya input tax na output tax huko ndio kutafutana mambo ya vat returns
 
Mkuu itakuaje refunded na VAT hawatozi hivyo, VAT inatozwa katika cost ya bidhaa na sio katika selling price ya bidhaa, maana ukiweka selling price ya bidhaa tayar VAT imo!!
Dah!! Kama ivyo kodi kubwa sana mkuu
 
Ivi mtu utasemaje VAT analipa mteja wakati hadi sasa nalazimishwa niandike risiti ya soda take away ya tsh 1000.sasa hapo mteja analipaje VAT wakati mimi ninanunua 800 nauza 1000 na nitoe risiti ya VAT. na ukumbuke kila nikikata risiti deni laongezeka kule tra mweisho wa mwaka nadaiwa kodi sijawai ona
 
Mkuu hujui biashara utakuwa!
Kodi zipo za aina tofauti kulingana na zinavyotozwa, mfano kuna VAT, PAYE, INCOME TAX, CORPORATE TAX nk.
VAT inatozwa katika bidhaa zinazouzwa na kununua ila. VAT ipo katika aina ya "indirect tax" tax kwa maana ya kuwa mlipa kodi yeye haoni kama amelipa kodi mfano nikinunua soda katika take away yako kwa Tsh 1000/= ni mimi ndie ntaelipa kodi ya Tsh 144/=kwa soda nilipokuwa. Swali! TRA hawapo kwenye take away yako watajuaje kama nimelipa kodi kwa kunywa soda kwako, ndipo hapo naposisitizwa kuchukua risit ili wewe mwenye take away upeleke 144/=yangu ya kodi TRA. Kama sikuchukua risiti maana yake hakuna uthibitisho kuwa nimelipa kodi hivyo kodi utalamba wewe wa take away.
PAYE hii ni aina ya kodi ambayo ni "direct" na anaetozwa kodi anaona jinsi gani kalipa kodi na kiasi gani mfano kodi wanayotozwa wafanyakazi walioajiriwa kila wapatapo mishahara mwisho wa mwezi.
INCOME TAX hii ndio utatakiwa kutozwa wewe mwenye take away, kwa mfano wa soda ulinunua kwa Tsh 800/=,VAT Tsh 144/=" ukauza kwa Tshs1000/=. Utanipelekea Tsh 144 /=yangu kama VAT TRA. Utabakiwa na pesa ya mauzo ya soda Tshs856/= ikihali wewe ulinunua kwa Tsh, 800/= hivyo umetengeneza faida ya Tshs 56/= ambapo kwako ni Income NA TRA watakupigia hesabu zao za kodi kwa hiyo faida yako ya Tshs, 56/=
 
Hili ndo swali nililokutana nalo mara tu baada ya kushuka kutoka kwenye mwendokasi "mminyano". Nilishangaa kuona Kariakoo ipo kama jumapili wakati leo ni siku ya kazi. ...' we hebu fikiria mtu akitoka magomeni mpaka
Kariakoo nauli sh 650, akitoka 650.

Wakati ule unaweza ukamwomba konda usafiri kwa mia tatu tu kuanzia magomeni mpaka Kariakoo, watu lazima wapungue'....alisema jamaa mmoja aliyekuwa anakunywa kahawa. Jamaa mwingine akadakia,.... '' sijawahi kuona kariakoo fremu zipo wazi zinakosa wafanya biashara wa kupanga!!!...hii haijawahi kutokea'' ...

nilipomdadisi sababu, aliendelea....' Wewe hebu fikiria, mfanyabiashara akiuza bidhaa kwa 100,000 TRA wanachukua 18,000 sasa jiulize, mfanyabiashara alinunua ile bidhaa kwa sh ngapi, na anapata faida sh ngapi baada ya kutoa kodi na gharama mbalimbali ikiwepo 18,000 ya TRA....?'.

Nilibaki macho kodo...., Kiukweli serikali iangalie hizi kero na nauli za mwendokasi, na pia iangalie namna ya kuhuisha au kupromote biashara kwa mzunguko kama wa miaka ya nyuma ili kodi ya kutosha ikusanywe...
Ukiuza recharge voucher za simu za 100000 faida yake ni 5000,sasa ukikatwa 18000 hapo lazima uimbe mabata madogo dogoo
 
Ivi mtu utasemaje VAT analipa mteja wakati hadi sasa nalazimishwa niandike risiti ya soda take away ya tsh 1000.sasa hapo mteja analipaje VAT wakati mimi ninanunua 800 nauza 1000 na nitoe risiti ya VAT. na ukumbuke kila nikikata risiti deni laongezeka kule tra mweisho wa mwaka nadaiwa kodi sijawai ona
Wewe niwakala tu wakukusanja kodi mzigo wa kodi utamlalia mtumiaji wa mwsho,
Sema kodi inapunguza faida yako, ndo maana watu wengne wanakwepa kodi!
Nadhani hapo chini itakusaidia kupata namna VAT inavyotozwa
View attachment 475239
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom