Ukiukwaji Katiba, Tanzania tunafeli Wapi?

Nchi si shamba la mtu. Nchi huendeshwa kwa kufuata katiba.

Inatia moyo majahili kama kina Alpha Conde wanapotiwa adabu kwa kukiuka katiba:

"Rais Alpha Conde alitaka kuvunja Katiba ya Nchi ili imruhusu kugombea kwa muhula 3 na bunge kumuongezea mshahara."

Sote hatupendi katiba ya nchi kuchezewa. Sote tungependa tabia hizi zikome. Lakini nani wa kumfunga paka kengele?

Wapo wanaomsubiri kwa dhati fulani achukue hatua, lakini si wao. Wana mawazo wakiyaita bora kabisa ambayo wangetaka fulani huyo ayachukue na hata hatua zipi afuate, lakini si wao.

Hao hao ni mafundi wa kuona makosa, kusema na kukosoa wakionyesha wapi fulani huyo anakwenda kombo. Wana ujasiri wa kubeza na hata kutukana wakiona fulani huyo anachelewa mno au hafanyi sawa sawa kulingana na matarajio yao.

Lolote baya likimkuta fulani huyo, hao hao hutokea na kumtupia lawama, kejeli na hata matusi kwa wasichoacha kukiona kuwa ni ujinga wake tu.

Hao hao kunako mafanikio huwa wako mstari wa mbele kwa ajili ya matunda yaliyo bora zaidi kuliko hata fulani yule aliyejitoa muhanga.

Hili ni rundo la "opportunists" wasio wa kuendekeza. Wanataka matokeo tu lakini si washiriki. Hawa wananunulika. Wako kimaslahi zaidi. Hawa ni mzigo na kimsingi hawafai.

Mjini wanajulikana kama wapenzi watazamaji.

Ni heri kuwekeza zaidi kwa wanachama ambao hata wanaojulikana kwa majina kama ni wetu, kuliko kwenye blanketi lenye kila Tom na Jerry ndani yake.

Hata kwa idadi ya wanachama wa Sipunda peke yake walio tayari kuyajaza magereza, mbona katiba ingeheshimiwa?

Mikutano ya vyama vya siasa na makongamano ni kwa mujibu katiba. Si kwa hisani ya mtu yeyote, chama au serikali.

Uvunjifu wa katiba haukubaliki.
taifa la mbumbumbu.
 
ugonjwa tunaujua dawa inafahamika tatzo tunaogopa kuchoma sindano

Hapo kwenye "tunaogopa" silabi "tu-" bila kuwa muwazi inakuwa na ukakasi wa kutosha.

Labda ingekuwa hivi mkuu:

"ugonjwa tunaujua dawa inafahamika tatzo baadhi tunaogopa kuchoma sindano"

Bila neno "baadhi" pale, wengine unatokosea sana mkuu.
 
taifa la mbumbumbu.

Hapana. Ni muhimu kutambua kama ilivyokuwa kwa Alpha Conde serikali yake ilikuwa imejipanga na kada hizi:

"Machinga, wapiga debe, boda boda, vibaka vibaka, sungu sungu na wa namna hiyo "at the expense of the rest.""

Kumbuka kada hizo ndiyo ambazo ni rahisi ku kuingia mtaani bila kujali hali.

Sisi tuna group kubwa la opportunists, labda kama ulivyo wewe ambao wangependa mno kuwaona wengine mbele, lakini si wao.

Ni muda sasa wa kuwataka opportunists kama hao kuufyata bila kujali nafasi zao kwenye vyama.

Pasipo na kujitoa kikamilifu haipo katiba mpya.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hapo kwenye "tunaogopa" silabi "tu-" bila kuwa muwazi inakuwa na ukakasi wa kutosha.

Labda ingekuwa hivi mkuu:

"ugonjwa tunaujua dawa inafahamika tatzo baadhi tunaogopa kuchoma sindano"

Bila neno "baadhi" pale, wengine unatokosea sana
umeeleweka sana
 
Back
Top Bottom