Ukiukwaji haki za raia vituo vya polisi umekithiri

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,550
29,626
Pamoja na ulinzi wa haki za raia kuainishwa kwenye Katiba yetu lakini jeshi la polisi wamekubuhu kusigina katiba kwa kutenda mambo ya hovyo dhidi ya watuhumiwa

1. Mawasiliano

Wananchi wengi wanaokamatwa wanazuiwa kuwasiliana na ndugu zao wawapo kituoni na hili husababisha usumbufu mkubwa kwa watuhumiwa na jamaa zao

2. Hukumu kabla ya mashtaka

Watuhumiwa wengi wa kesi ndogo ndogo kama vile wizi wa kuku, baiskeli na aina hiyo wanapigwa kikatili ili wakiri makosa yao kwenye karatasi za maelezo hivyo wengi hupelekea kupata ulemavu au kupoteza maisha

3. Mahabusu kukaa muda mrefu bila kupelekwa mahakamani

Vituoni kuna tabia ya kuzuia dhamana za baadhi ya watuhumiwa ambao wanadhaminika hadi watoe rushwa na kuna mtindo watuhumiwa wanarundikwa hata zaidi ya mwezi wakiwa vituoni huku wakikosa haki ya kujibu mashtaka au kufutiwa mashtaka yao.

4. Rushwa

Mshtaki na mshtakiwa mara nyingi huombwa rushwa ili kuweka mazingira mazuri ya mwenendo wa kesi pale kituo cha polisi.

6. Kubambikia kesi

Kwa mfano. Mtuhumiwa wa uzururaji kama anatulizwa kituoni zaidi ya wiki mbili kisha anatafutiwa robbery case ili akamuliwe fedha au apotee kabisa...

Kuna vijana wengi wanakamatwa kwa petty cases lakini wakifikishwa vituoni wanapewa "vichwa" yaani kubambikiwa kesi.

Nimeeleza kwa uchache baadhi ya kero lakini naamini wengi humu mnazo kero nyingi dhidi ya jeshi la polisi.

Jeshi letu linapaswa kujikita kwenye jukumu lake la kikatiba la ulinzi wa raia na mali zao.... ushirikiano na mahusiano mazuri baina ya polisi na raia hupelekea kupingua ama kuisha kabisa kwa uhalifu nchini.

IGP boresha jeshi lako liwe lenye tija

Uzi tayari
 
Halafu wakuu wa vituo hawatimizi wajibu wao wa kuwatembelea mahabusu kujua makosa waliyoshikiliwa nayo.

Unakuta mtu anatoa fedha polisi ili mtoto wa jirani yake atiwe adabu kwa kuwekwa mahabusu...

Kuna mengi yanaogofya vituoni hapo
Kijitonyama - Mabatini



IGP Sirro tupia jicho lako hapo. Kuna kila aina ya uchafu.
 
Back
Top Bottom