#COVID19 Ukiugua ugonjwa ambao hauna tiba na ukapona, je inahitaji kupatiwa chanjo?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,884
Tumeona kati ya watu 200 million walioambukizwa na kuugua ugonjwa wa COVID-19, ni watu milioni 4 tu wamekufa. Ina maana zaidi ya million 190 wamepona bila kuwa na na specific treatment ya ugonjwa wa UVIKO-19. Ni kwamba miili ya wagonjwa hawa iliweza kujitengenezea specific antibodies against COVID-19.

Swali langu ni je? Watu wa aina hiyo kuna ulazima wa kudungwa sindano ya chanjo ya COVID-19?
 
Umuhimu upo mkuu maana virus ina uwezo wakujibadlisha hivyo ndio maana hichi kirus kina wimbi tofauti kama hili tulilonalo sasa wanaita delta kuna aina ingine inaitwa lambda imeanzia california, kwa uelewa wangu ni kwamba ni vizuri kuwa na kinga ili kusaidia mwili uweze kupammbana na mabadiliko ya wimbi moja hadi jingine.
 
Tumeona kati ya watu 200 million waliyoambukizwa na kuugua ugonjwa wa covid 19 ,ni watu milioni 4 tu wamekufa. Ina maana zaidi ya million 190 wamepona bila kuwa na na specific treatment ya ugonjwa wa uviko 19 ni kwamba miili ya wagonjwa hawa yaliweza kujitengenezea specific antibodies against covid 19 swali langu ni je? Watu wa aina hiyo kuna ulazima wa kudungwa sindano ya chanjo ya covid 19?
Hapana mkuu chanjo haitajiki tena hapo bali ni damu ya bwana Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu na yako na vizazi vijavyo.
 
Hapana mkuu chanjo haitajiki tena hapo bali ni damu ya bwana Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu na yako na vizazi vijavyo.
Hapana mkuu chanjo haitajiki tena hapo bali ni damu ya bwana Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu na yako na vizazi vijavyo.
Duuuh.nimeuliza kisayansi wewe unanijibu kiroho? Mimi nataka sayansi kwanza
 
Umuhimu upo mkuu maana virus ina uwezo wakujibadlisha hivyo ndio maana hichi kirus kina wimbi tofauti kama hili tulilonalo sasa wanaita delta kuna aina ingine inaitwa lambda imeanzia california ,kwa uelewa wangu ni kwamba ni vizuri kuwa na kinga ili kusaidia mwili uweze kupammbana na mabadiliko ya wimbi moja hadi jingine
Je Kirusi kikijibadilisha nini kinaongezeka na kwanini?
 
Tumeona kati ya watu 200 million waliyoambukizwa na kuugua ugonjwa wa covid 19, ni watu milioni 4 tu wamekufa.Ina maana zaidi ya million 190 wamepona bila kuwa na na specific treatment ya ugonjwa wa uviko 19. Ni kwamba miili ya wagonjwa hawa yaliweza kujitengenezea specific antibodies against covid 19.

swali langu ni je? Watu wa aina hiyo kuna ulazima wa kudungwa sindano ya chanjo ya covid 19?
Kuugua covid mara ya kwanza na kupona haikufanyi usiugue tena. Hakuna mtu anapenda kuugua. Kwa hiyo kuchoma sindano ya kinga ni kwa ajili ya kujizuia ukiambukizwa tena,usigue kama ulivyougua mwanzo.

Kuugua covid kumegawanyika,nafikiri ni kufuatana na damu au na uimara wa kinga zako mwilini. Mfano mimi nimeugua kama mara mbili hii ndude na kupona,lakini nilikuwa naendelea tu na shughuri zangu kama kawaida,lakini kuna wengine mpaka wanalazwa na wengine wanalala tu majumbani wanashindwa kuendelea na shughuri zao za kila siku sababu ya hayo maradhi.

Mfano mwingine watoto,huwa wakiambukizwa wanaendelea tu shughuri zao. Na wanawake ni kama haiwasumbui sana kuliko wanaume. Na vifo ni vingi vya wanaume kuliko wanawake. Wanaume wanakufa wengi na huu ugonjwa kuliko wanawake.

Na kuugua kwa mara ya kwanza covid na kupona hakukufanyi usiugue tena na tena. Kila utakapoambukizwa utaugua tena na kuna uwezekano ukaugua zaidi ya pale mwanzo ama wengine wanapoteza maisha,atakapougua mara nyingine,japo mara ya kwanza alipona.

Kwahiyo sasa ili kuepuka hayo ndio umuhimu wa chanjo. Japo mimi sitachanjwa.

Kuna mzee wangu,msomi wa zamani,alikuwa na uhitaji sana wa kuchanjwa,na mimi nilipenda achanjwe ksbb ya utu uzima. Nikamuelekeza namna ya kujaza form mtandaoni. Alivyoingia tu hapo,akasoma sehemu iliyoandikwa “nchi haitahusika kwa madhara yoyote utakayoyapata”. Hapo moyo wake ukanywea,akaamua kuahirisha kwanza
 
Najibu kulingana na elimu yangu ya udaktari wa wanyama maana mie sio daktari wa binadamu hivo naomba nisiulizwe maswali yoyote yanayohusu swala zima la corona.

Mwilini mfumo wa kupambana na vimelea umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni defence line ya kwanza na defence line ya pili, vimelea vinapofanikiwa kupita ngome ya kwanza ambayo immune cells ambayo ndio first line ya defence ya mwili, hao vimelea (pathogens) wanataenda kukutana na second line of defence ambayo inaundwa na B-cells na T-cells

Hawa B-cells wao wanadeal na kuzalisha askari kinga wa kupambana na infection ambazo zinaweza kuwa za bacteria au virus au wengine, ambapo waga wanaenda kuundwa specific kulingana na aina ya ugonjwa (antibodies)

Na huyu T-cells amegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Helper T-cells na Killer T-cells, ambapo huyu Helper T-cells yeye anaenda kusaidiana na B-cells kwenye zoezi zima la kutengeneza Antibodies lakini huyu Killer T-cells yeye anaenda kuuwa zile Cells za mwili ambazo zinakuwa zimeathiliwa na ugonjwa husika

sasa baada ya kuugua na kupona ndipo hizi cells kwa pamoja yani B-cells na T-cells zinaunda Memory ya pathogens ambao walishambulia mwili wakati uliopita ili kama wakija kwa mara ya pili basi wasiwe na kazi ya kurudia process bali ni kuzalisha moja kwa moja Antibodies

Lakini tunajua kuwa virus wana sifa ya kubadirika badirika nawewe wakati unaugua na mwili unaunda Antibodies waliunda dhidi ya strain fulani na sio zote, kwahiyo kama utakuja kuwa infected na corona tena kwa mara ya pili ambao watakuwa sawa sawa na wale wa awali maana yake mwili wako utakuwa na Natural vaccine ambayo iliundwa wakati umeugua kwa mara ya kwanza

Lakini kama ikitokea umeugua corona lakini ikawa imekuja na strain au aina tofauti ya virus safari hii mwili wako hautakuwa na Natural vaccine ambayo itapambana na hao virus kwa 100% na hapo ndipo linakuja swala la kutakiwa kupewa tena chanjo ya corona maana hujui exactly watakuja wajuba wa cuba au Alshabab. Nadhani kwa huu uelewa wangu mdogo angalau nimejaribu kujibu mkuu

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
 
Mh ,hata siyo uelewa mdogo.ni mkubwa sana.nilitaka pia kujua madhara ambayo MTU anaweza akapata kama atachanjwa wakati bado ana natural specific immunity gained during the infection.

Lakini pia kama chanjo zitakuwa zinauzwa,ni dhahiri kwamba low income countries hatutaweza kumudu gharama kwa sababu kwa nature ya kirusi kujibadirisha MTU anaitaji aina zaidi ya mbili ya chanjo.
Hapa lazima tuwapigia magoti matajiri.kumbe herd immunity kwetu ilikuwa bora kwetu masikini kuliko hii massive immunization.
 
Umuhimu upo mkuu maana virus ina uwezo wakujibadlisha hivyo ndio maana hichi kirus kina wimbi tofauti kama hili tulilonalo sasa wanaita delta kuna aina ingine inaitwa lambda imeanzia california, kwa uelewa wangu ni kwamba ni vizuri kuwa na kinga ili kusaidia mwili uweze kupammbana na mabadiliko ya wimbi moja hadi jingine.

Hivi hii vaccine tunayopata ( j&j) na zingine zipo kwa ajili ya kirusi kipi cha corona?
 
Kuna ulazima wa kudungwa chanjo kwa sababu kama uliugua kirusi cha Delta ukapona ikija Lambda inakuondoa.Hii ndiyo sababu ilinilazimu mimi kwenda kuchanja.
 
Hivi hii vaccine tunayopata ( j&j) na zingine zipo kwa ajili ya kirusi kipi cha corona?
Nimeona nakusikia wakisema waliochoma j&j watalazimika kuchoma buster kuongezea j&j nguvu yakukabiliana na wimbi jipya liitwalo lambda ambalo limeanza tena hivi karibuni huko Califonia kwa jj ilikuwa mahususi kwa delta
 
Nimesoma hizi chanjo jinsi zimetengenezwa na naoma SINOVAC wametoa aina ya chanjo ambazo mfumo wake ni kama ule wa chanjo za zilizokuwa zinatengenezwa kwa ajili ya ugonjwa wa ini na homa ya manjano.
Chanjo ni muhimu kwa sababu ya wadudu tofauti tofauti wanaotokea sehemu tofauti tofauti kwa wakati huu. Lakini kwa namna wanavyobadilika kwa kasi napatwa na wasiwasi na umuhimu wake kwa maana sasa amekuja MU variant ambaye chanjo ya sasa inaweza isisaidie.
 
Back
Top Bottom