Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,987
- 144,319
Uamuzi wa wamerekani kutunyima misaada japo utatuathiri zaidi sisi wananchi wa kawaida,bado nauunga mkono kwani utasaidia kuwa-shape watawala wetu.
Pia tutambue ili kuitoa CCCM madarakani, ni lazima tuwe tayari kulipa gharama ya mabadiliko maana hawa jamaa si rahisi kuachia madaraka kirahisirahisi tu bila mashinikizo kama haya ya MCC na mengineyo.
Hata hivyo, siamini kama nchii haiwezi kujitegemea bila msaada wa mataifa ya nje bali tatizo kubwa ni uzembe na kutowajibika ipasavyo katika kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato.
Kwa mfano,nchi hii biashara ya nyumba za kupangisha ni biashara kubwa sana na inayolipa kweli kweli kwa wanaomiliki majumba na nyumba za kupangisha ila tu tumeshindwa kuwa na sera na sheria ya kusimamia ukusanyaji wa kodi katika eneo hili.
Kinachotakiwa ni serikali kuandaa sera na pia kutunga sheria kali itakayomlazimisha mtu yoyote mwenye kufanya biashara hii atoe taarifa TRA na katika serikali ya mtaa na kuwe na adhabu kali kwa atakaebainika kufanya biashara hii kwa siri na pasipo kufuata sheria.
Serikali inaweza pia kuwatumia wenyeviti wa vijiji,watendaji wa mitaa na madiwani katika kuwatambua wale wote wanaofanya hii biashara na serikali inaweza kutoa motisha kwa diwani,mwenyekiti au mtendaji ataekaefanya kazi hii vizuri kama vile kuwalipa kwa kamisheni kutokana na makusanyo yatakayopatikana.
Njia mojawapo ni serikali kuandaa fomu maalumu na kuzisambaza kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa ambao nao watapaswa kuzisambaza kwa wamiliki wa nyumba au majengo katika vijiji au mitaa yao huku wakiwa na nguvu za kisheria kufanya hivyo na zitakazowalinda dhidi ya mtu yeyote yule atakaejaribu kuwakwamisha kwa namna yoyote ile katika jukumu lao hilo.
Pia kuwe na nafasi ya wamiliki kufika TRA au serikali ya kijiji/mtaa na kutoa update za kimaandishi kama ameuza nyumba au jengo lake,kama ameongeza vyumba,kama ameacha kupangisha,n.k na iwe ni kosa kisheria kutotoa taarifa hizi pale mmiliki anapofanya mabadikiko yoyote yale katika biashara yake hii.
Fomu hizi ziwe maalumu kwa watu kujaza taarifa zao kama kama vile ana ya vyumba au nyumba wanazopangisha,ukubwa wake,bei anazotoza,eneo nyumba au vyumba husika vilipo, n.k.
Mbali na fomu hizo kubeba taarifa muhimu zitakazosaidi ukusanyaji wa kodi,fomu hizi ziambatane na tamko la kisheria kuwa ni kosa kisheria kutoa taarifa za uongo na zitaje adhabu inayoweza kumpata mtu atakaetoa taarifa ya uongo katika kujaza form hizo.
Pia,serikali iongeze nguvu katika ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali za mitaa na kuweka bayana kuwa kila mwenyekiti wa mtaa au diwani wa eneo husika atalipwa mshahara kutokana na makusanyo ya kodi hizi ikiwemo na kodi itakayotokana na nyumba za kupangisha ila viongozi hawa wataongezewa jukumu la kusimamia ukusanyaji wa mapata haya katika maeneo yao ya kazi na iwe ni moja ya majukumu yao ya kila siku.
Eneo mojawapo ambalo serikali inaweza kukusanya mapato makubwa ni katika maeneo ambako kuna vyuo.Wanafunzi wengi wanapanga mitaani jirani na vyuo wanavyosoma na siku hizi watu wanajenga mahostel maalumu kwa ajili ya kupangisha wanafunzi na wanaingiza fedha nyingi tu pasipo kulipa kodi.
Ukiacha maeneo vilivyoko vyuo mbalimbali,kuna hili swala la mtu mmoja kumiliki fremu kibao za biashara(maduka n.k) katika jengo lake huku fremu zote au baadhi ya frame hizo akizipangisha na anakusanya kodi pasipo yeye kulipa kodi serikalini zaidi tu ya yeye kulipa property tax ya jengo lake.Bei za fremu hizi kila mtu anazijua na unatakiwa ulipe ama kwa miezi 6 au mwaka.Ni hela ngapi hawa watu wanaingiza pasipo kulipa kodi serikalini?
Nchi hii ina majumba na majengo mengi sana yaliyotapakaa nchi nzima mijini na vijijini yanayotumika katika biashara hii ya kupangisha, na nyumba/majengo haya huishia tu kulipiwa property tax wakati yanaingiza fedha nyingi pasipo kulipiwa kodi!
Hivi kweli inaingia akilini mtu mwenye fremu kibao za biashara katika jengo lake anakupangishia fremu unamlipa kodi yake kwa miezi 6 au mwaka mzima na wanakuja TRA nao unawalipa alafu tajiri huyu yeye anaishia kulipa kodi moja tu ya property tax (kodi ya jengo) wakati anazalisha mamilioni bila kuyalipia kodi?Hii haikubaliki hata kidogo.
Hata hivyo,nashauri nyumba za udongo za kupangisha huko vijjini zisihusishwe katika mpango huo kwani wengi wenye hizi nyumba wanatafuta pesa za kujikimu tu kimaisha huko wanakoishi.
Yako na maeneo mengine mengi tu kinachotakiwa ni watu wa TRA kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuingia mitaani na kufanya utafiti na sio kukaa maofisini tu.