Ukitoa maoni wanayoyakubali, una akili, ni kichwa, n.k. Ukitoa yasiyowapendeza ni mjinga, ni zwazwa....

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,223
113,545
Hivyo ndivyo vipimo vya makamanda! Hususan makamanda waliomo humu JF!

Hawa watu siku hizi wamekuwa ni vituko kabisa.

Wengine wameshakariri kiasi wakiona umeandika kitu hata hawajisumbui kusoma na kuelewa [narudia tena, kusoma na kuelewa] ulichokiandika.

Wao wanaenda moja kwa moja kutapika kile walichokikariri na kugongeana Likes tu.

Utawaona wanakuambia ‘we jamaa zamani nilikuwa nakuona una akili lakini tokea ununuliwe na Lumumba umekuwa jinga kabisa’.

Wengine watasema ‘zamani nilikuwa nakuona una busara, una mapointi makali, nilikuwa nakuona ni kichwa kumbe nilikosea’.

Hayo utaambiwa pindi utapokuwa umeandika jambo au mambo wasiyokubaliana nayo.

Ukiandika yanayowafurahisha utamwagiwa sifa kem kem. ‘Huyo ndo Nyani ninayemjua [sijui hata umenijulia wapi]’, ‘ Nyani back to his senses’ na Nyani this, Nyani that!

Hivi kwani mtu hawezi kuwa na akili hata anapotofautiana nanyi nyie makamanda?

Kwenu wenye akili ni wale wanaofikiri, kuwaza, na kuongea kama nyie tu?

Sijawahi kuona watu walio parochial na closed-minded kama hawa makamanda!

Wakati mwingine huwa nadhani labda vitu haviko sawa vichwani mwao.
 
UKiwa kwenye ulaji lolote unaweza kusema, ukiweza kuingia rohoni mwa Nape kipindi hiki nadhani ungepata fundisho zuri sana. Hata Leprofeseri Kitila kwa sasa si unamuona? Haya mambo hayahitaji elimu ya juu kuyajua hata kule kijijini watu ambao hawajaenda shule kabisa wanajua mtu akiwa kwenye ulaji huwa hana shida ya kufikiria wenzie akishatolewa hapo ndio akili humkaa sawa. Kwa kuwa ni mnufaika na mfumo huwezi kuona tatizo ngoje mfumo ukutema utajua na kulewa tu. Mwenye busara nyakati hizi anatakiwa kutumia akili sana wakati wa kuandika humu.
 
Tatizo UVCCM hua hamkubali kushindwa mnapinga mpaka kitu chenye logical evidence
"delusion of grandeaur"

sasa sijajua na wewe Kama umeanza kupata "delusion of persecution"
 
hawa makamanda ni madikteta wa mawazo, wao ndio wapo sahihi kila siku kama malaika, chama na viongozi wao huwa hawakosei. Mtu yeyote ambae si kamanda hana akili nzuri, ili uwe na akili timamau ujiunge na makamanda, wasomi makamanda, great thinker makamanda kwa hiyo yote mazuri duniania ni ya makamanda tu, wanywa viroba makamanda, matusi ndio sera ya makamnda, kutokuwa na heshima kwa watu wazima ni makamanda, kugeuza nyeusi kuwa nyeup ni makamanda tu, na huo ndio ukamanda
 
Right on the money!
 
Back
Top Bottom