Ukitazama picha ya kisiasa, Elimu imekuwa si mkombozi tena kwa Mtanzania

Ubuntuwize

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
312
91
Kwa mujibu wa takwimu za sasa ni kwamba, elimu inapanda mara dufu kutoka mwaka 2015 mpaka hivi sasa 2020.

Kwa mtazamo huo ningetarajia kabisa watu wawe na uwezo angarau wa kuona mapungufu makubwa yaliotokea katika utawala wa miaka 5 ya bwana JPM. Tofauti na hilo wengi mamegeuka kuwa washabiki na kuweka pembeni kabisa elimu zao. Hivi sasa wengi wamegeukia ushabiki na mkumbo wakijiangalia wao binafsi na sio maslahi ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Utaona kundi kubwa la wasomi ndio wanaoongoza kwa kufuata mkumbo na kutochukua walau muda kidogo kufanya tathimini au uchambuzi wa tulikotoka na tunakoelekea.

Kufanya hivi ni kuisaliti elimu yao kwani ni ukweli usio pingika kuwa wamejifunza mengi huko ma shuleni na vyuoni, wamejifunza juu ya ujasiri wa baadhi ya viongozi walio watangulia hasa wale walio pigania uhuru wa nchi mbali mbali na kufanya mapinduzi ya kweli.

Nilitarajia wasomi wawe chachu ya ku "Spark brain" za Watanzania ili wasiendelee kuburuzwa na kutoa changamoto kwa viongozi watakao chaguliwa kujua kwamba hii nchi sio mali yao binafsi. Kuleta ustawi wa taifa sio ombi kwa kiongozi bali ni wajibu wake kwa taifa kwani linakua lime mchagua kama muwakirishi tuu wa kuongoza harakati za maendeleo.

Mwisho natoa wito kwa wasomi wote (Walienda shule yeyote) kutumia taaluma zao kuibua mijadara itakayo saidia kuchochea upatikanaji wa viongozi bora na sio wasindikizaji tu.

Wasalaam

MONANJA
 
Mi nimekuelewa kabisa ila fanya marekebisho kidogo.

Angarau = Angalau.

Mijadara = Mijadala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom