Ukitaka watanzania wasahau ndoa..wanakanisa tukapime dna za watoto wetu

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Kama kuna dhambi ambayo naiheshimu ni kutunza mtooto wa watu
dhambi hii imeiuma sana hasa kwa watanzania wengi na kinachonifurahisha
nje kupima dna ni cha kawaida lakini watanzania wakifikira kupimana dna wanawaza ndoa zao

wanaajiuliza je ikitokea sio mtoto wangu nitawaeleza nini ndugu zangu...

Je ndoa yangu ndio itaishia mwisho????

Je baada ya hapo mama atakubali kumpeleka mtoto sehemu ya kutunzia watoto wasiokuwa nawazazi

ni maswali mengi wanajiuliza lakini imefikas sasa wakati muafaka watanzania tuamke tuanze kupima watoto wetu......wengi wanakimbilia kupima ukimwi ni nzuri ukweli unabaki ugonjwa mkubwa uliofichwa ndani ni kutunza mtoto wa mtu



mh rais mtaafu alisema ugonjwa huuu yaani ....umefichwa mahali pabaya sana sana na ndio maana tunaisha lakini mkuu ukweli unabaki ako kagonjwa cha kuchapiwa na kuzalishiwa mwisho kutunza watoto si wako kimeshamiri na kinatapakaa kama kaugonjwa cha ukoma

maombi yangu kwa mungu usisubiri mwanao afanane ati na marehemu babayako ama bibi yako kapime dna uishi kwa amani
 
Kuishi kwa matumaini ndiyo mpango mzima Best! Sasa watu wana miaka 20 kwenye ndoa wakapimane DNA si kuuana kwa presha?
 
^^
Ukimchunguza sana mke,,hutaishi nae.
Kuanzia mapishi hadi watoto.
Kulea watoto wasio wako bila wewe kujua sio dhambi ni sadaka ya ukunjufu wa moyo
^^
 
umevurugwa nini?????Eboo! tupime watoto ili iweje sasa???????
tuwatupe?
tuwapeleke orphanage centres? tuwapeleke kwa baba zao ambao nao pia wana wake zao ambao hawakawaambia kuwa wana watoto wengine?
tuvunje ndoa zetu??
tuuane kwa kuumizwa na usaliti??
mbona wanawake wanawapokea waliozaliwa nje bila kuwapima?
WEWE NANI KAKUZUIA KUPIMA WAKO?
Sababu zako ni zipi haswa za msingi maana wewe pia sio kichaa hebu tupe zako kwanza.
 
umevurugwa nini?????eboo! Tupime watoto ili iweje sasa???????
Tuwatupe?
Tuwapeleke orphanage centres? Tuwapeleke kwa baba zao ambao nao pia wana wake zao ambao hawakawaambia kuwa wana watoto wengine?
Tuvunje ndoa zetu??
Tuuane kwa kuumizwa na usaliti??
Mbona wanawake wanawapokea waliozaliwa nje bila kuwapima?
Wewe nani kakuzuia kupima wako?
Sababu zako ni zipi haswa za msingi maana wewe pia sio kichaa hebu tupe zako kwanza.

hahahaaaa namsubiri client kwanza
 
Kabla zoezi la kupima DNA za watoto wetu wenye Bastola wote wanyang'anywe vinginevyo tutashinwa hata kuzika misiba itakuwa mingi mno,Mbona mababu zetu walimegeana na ikabaki siri ? kwanini tusikubaliane na methali zao kuwa KITANDA HAKIZAI HARAMU
 
Siwezi kuwashauri watu wafanye hii DNA testing hasa kwasababu ya uzoefu wa hulka ya Mwafrica!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom