Ukitaka usiugue kila wakati, tumia njia hii

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Fanya hivi kila siku

1. Unapoamka Asubuhi kula Tunda la Tufaha (Apple) Hutoweza kuonana Daktari siku nzima.
An apple a day keeps the doctor away

Apple.jpg


2. Kula Punje 2 za Kitunguu Saumu hutapata ugonjwa wa kansa (Saratani).

Kitunguu Saumu kinga ya kudumu.jpg


3. Kunywa juisi ya lemon kila Siku asubuhi hutapatwa na unene.

juisi  ya limau.jpg


4. Kunywa glasi 1 ya maziwa ya ng'ombe ya asili sio Maziwa yanayo uzwa Madukani hutopatwa na maradhi ya mifupa kuuma mwilini.
maziwa.jpg



5. Kunywa Maji ya Uvuguvugu lita 3 kwa siku hutopatwa na maradhi yoyote yale.


Maji ya uvuguvugu.jpg


chanzo:MziziMkavu
 
Kifo hakizuiliki wakati uko njiani kwenda kununua ndimu unaweza ukagongwa na gari
 
Kwa maisha yetu wengi yalivyo magumu huu ni mtihani vitu vyote hivyo utaanzaje kuhangaika navyo wakati saa 11 alfajil unatakiwa uwe road kwenda kwa mdosi... Anyway mwnye uwezo wa kufanya hivi na afanye. Ahsante sana mzizi.
 
Tatizo kitunguu swaum kinaacha kinywa na harufu Kali sana mkuu
Hakuna namna ya kuzuia harufu
Kula Kitunguu Saumu pamoja na Maziwa na pia ukimaliza kula kitunguu saumu kula punje 4 za hiliki au punje 4 za Karafuu au kula tango moja linakata harufu ya kitunguu saumu Au kunywa maji ya Uvugvugu glasi 3 asubuhi inakataka harufu ya Kitunguu saumu.
 
Hata mimi hio harufu yake ilinishinda...halafu unakuwa hauko comfortable na wenzako ofisini...mara bigG haitoki mdomoni ilimradi karaha tu..nikaacha. kama ndugu mzizimkavu akipita hapa atupe msaada jinsi ya kutoa hio harufu ya kitunguu saumu

Kula ndizi au apple

Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango
Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.
 
Back
Top Bottom