Robinhomtoto
JF-Expert Member
- May 17, 2017
- 238
- 244
Leo nimewasikia viongozi wa Serikali Na CCM mkoa wa Mwanza wakimwaga Sifa kem kem Kwa Mzee Francisco Maige Kanyasu Mchoraji wa Nembo ya Taifa. Mzee amepewa majina makubwa kama vile "Genius" Paroko wa kanisa katoliki ametoa angalizo kuwa tusimshughulikie MTU akiwa mahututi au amekufa Na akasema Marehemu Kanyasu angethaminiwa mchango wake mapema pengine asingeishi maisha aliyokuwa anaishi.