Ukitaka upate tiba bora basi jifunze pitia hapa itakusaidia

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
24,559
47,002
Habari za muda marafiki,kuna haja ni share hii elimu ni nzuri na itakusaidia kwa kiasi fulani jinsi kama mgonjwa unapaswa kujua namna ya kujielezea kwa daktari ili upate tiba bora kwa mtoa huduma.

Ni muhimu tukafahamu kuwa, maelezo yako kwa daktari yanachangia mpaka asilimia 75 ya daktari kuweza kugundua tatizo linalokukabili! (asilimia 25 iliyobaki ni ya daktari kukufanyia uchunguzi wa mwili kwa mikono yake, na vipimo vya maabara).

Hii ina maana ya kwamba, historia anayoipata daktari kutoka kwako, ina mchango mkubwa sana katika kumuelekeza daktari kwenye tatizo sahihi linalokusumbua; ama kumpelekea daktari kukosea kabisa aina ya tatizo ulilonalo, ama hata kushindwa kabisa kufahamu ugonjwa unaokusumbua hasa ni nini. Mambo yafuatayo yatakusaidia kuweza kujieleza vizuri kwa daktari

Usimwambie daktari ugonjwa wako (diagnosis), bali mueleze daktari dalili ulizonazo

Hapa ninawazungumzia wale ambao wanaingia chumba cha daktari na kuanza kujieleza "daktari nina malaria" au "nina typhoid". Hii sio njia sahihi kabisa ya kuanza kujieleza kwa daktari!

Kufahamu aina ya ugonjwa unaoumwa (diagnosis) ni kazi ya daktari, unachotakiwa kufanya ni kuelezea dalili zako, kwa mfano "kichwa kinaniuma na ninaharisha tangu juzi".Hii ndiyo namna bora kabisa ya kuanza kujieleza mbele ya daktari!

Hakuna kitu ambacho kinamfanya daktari aghafilike kama mgonjwa kuanza kusema diagnosis yake badala ya kuelezea dalili zake.

Epuka kutumia maneno ambayo yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja kwa watu tofauti

"Daktari nina homa tangu juzi" siku zote mgonjwa akianza kujieleza kwa kauli hii kwangu, swali linalofuata ambalo huwa nauliza ni "unamaanisha nini unaposema homa"?

Na huwa napata maana tofauti kwa watu tofauti. Wengine husema wanamaanisha mafua na kukohoa, wengine wanamaanisha kuwa joto la mwili liko juu, wengine husema wanamaanisha kuwa wanaharisha, na kadhalika.

Hivyo basi, badala ya kuanza kujieleza kuwa una "homa" (ambayo kiukweli,kwa daktari asiekuwa makini, na akachukulia homa kwa maana ya kidaktari, anaweza kukupa ugonjwa ambao wala hauna kabisa), ni vyema ukajieleza kwa kutumia maneno ya moja kwa moja na kwa kutaja dalili zote ulizonazo, moja baada ya nyingine.

Usiseme uongo wala kuficha kitu chochote kwa daktari kuhusu afya yako:

Hakuna kosa kubwa (mimi huita suicidal mistake) kwa mgonjwa kufanya, kama kumdanganya kwa makusudi daktari, au kuficha kitu fulani kuhusu afya yake au kuhusu ugonjwa wake. Huna sababu yoyote ya kumdanganya daktari au kumficha kitu daktari kwa sababu zifuatazo

Kwanza, kumdanganya daktari kutapelekea daktari kushindwa kubaini tatizo lako, au hata kumpelekea kukosea ugonjwa unaokusumbua; kwa sababu kama tulivyoona awali, daktari anatagemea maelezo yako kwa asilimia 75 kugundua tatizo lako

Pili, hicho unachoogopa kumwambia, kuna uwezekano mkubwa kabisa ya kuwa ameshawahi kukisikia/kukiona na haitakuwa mara ya kwanza yeye kusikia/kuona hicho kitu, hivyo huna sababu ya kuogopa

Tatu, nakuhakikishia kuwa kuna uwezekano mkubwa sana (asilimia 99.9) kuwa, daktari atasahau hata sura yako mara baada tu ya wewe kutoka nje ya chumba chake, achilia mbali tatizo lako ulilomwambia!! Kwa mfano, kwa wastani siku ambayo naona wagonjwa naweza kuona wagonjwa zaidi ya 50; na nara zote mwisho wa siku huwa sikumbuki sura za wagonjwa niliowaona, achilia mbali matatizo yao

Unapoenda hospitali, nenda na dawa zako zote unazotumia au uliwahi kutumia kwa tatizo ulilo nalo

"Nilikuwa natumia vidonge fulani hivi vyeupe vikubwa vya duara" usitegemee kabisa daktari aweze kugundua kuwa ni aina gani ya dawa uliyokuwa unatumia kwa maelezo ya aina hii!

Maana, rangi ya dawa haina umuhimu wowote katika kile ambacho kipo ndani ya dawa. Na kimsingi, kuna dawa ambazo zinapatikana katika rangi tofauti kutegemea na kiwanda zilipotengenezwa, lakini zina kitu kile kile ndani yake!!

Hivyo basi, kama tatizo ulilo nalo ni la muda mrefu, na uliwahi kwenda hospitali na ukapewa dawa ni vyema ukaenda na dawa hizo pale unapokwenda tena hospitali kwa tatizo hilo; au angalau ukabeba kikopo ambacho kilikuwa na dawa hizo.

Kwa watoto, aende mtu ambae anakaa na mtoto na/au anafahamu vizuri historia ya ugonjwa wa mtoto

Huwa napata tabu sana pale ninapomuona mtoto anaesumbuliwa na dalili fulani, halafu namuuliza aliemleta, "amekuwa na dalili hizo kwa muda gani" halafu jibu ninalopata linakuwa "sijui".

Jibu la aina hii linakuwa halina msaada wowote ule kwa daktari, bali huleta usumbufu usio wa lazima kwa daktari; Hivyo basi ni muhimu aende mtu ambae anafahamu vizuri historia ya tatizo la mtoto.

Uliza maswali kuhusu ugonjwa wako, vipimo na matibabu

Mara nyingi madaktari huwa tunajisahau kuwaelezea wateja wetu kwamba ni nini anaumwa, na ni vipimo gani anatakiwa kufanya (na majibu ya vipimo hivyo), na matibabu ni yapi.

Hivyo basi, daktari akimaliza kukuhudumia na kukwambia "nenda maabara" kwa mfano, unatakiwa umuulize kwa utaratibu, kuwa je, daktari anadhani una ugonjwa upi? na amekuandikia vipimo gani?

Na pia, hata ukirudi kwa daktari na majibu ya vipimo vyako, ni vyema ukamuuliza majibu yanasemaje, na yanamaanisha nini; Vile vile kwa dawa atakazokuandikia.

Daktari ambae anajua anachokifanya hatapata shida kabisa kukuelezea yote hayo (labda kama umeuliza kwa ukali au kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu)
 
Mimi u t i inanisumbua bado,nimemeza karibu zote,nimechoma sindano lakini imerudi tena.nisaidie nifanyaje kaka
 
Male miaka 28 mkuu
Mara ya mwisho ulitumia dozi gani na je ulimaliza dozi na masharti uliyopewa na daktari?pia ukiwa unaitibu nenda na mwenza/mpenzi wako health center mtibiwe pamoja na amini tatizo litaisha
 
Nilimaliza.mara ya mwisho nilichoma sindano pamoja na dawa Aina ya metro
Mara ya mwisho hiyo wakati daktari anakupa matibabu ulienda na mwenza wako?unaweza ukawa unajitibu ila ukasahau chanzo,maana. Kwa wa wanaume huwa inatokea mara chache kuwa na UTI SUGU kutokana na maumbile
 
Mara ya mwisho hiyo wakati daktari nakupa matibabu ulienda na mwenza wako?unaweza ukawa unajitibu ila ukasahau chanzo,maana. Kwa wa wanaume huwa inatokea mara chache kuwa na UTI SUGU kutokana na maumbile
Sikua na demu special,ila tangia huu mwaka uanze sijaenda peku.hili ni tatizo la mwaka jana.nisaidie nitumie njia gani zaidi maana naona dawa zinadunda.nimejaribu pia na baking soda,lakina wapi!
 
Sikua na demu special,ila tangia huu mwaka uanze sijaenda peku.hili ni tatizo la mwaka jana.nisaidie nitumie njia gani zaidi maana naona dawa zinadunda.nimejaribu pia na baking soda,lakina wapi!
Jaribu hii dosi Cephalexin kwa siku 7
 
Back
Top Bottom