singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Baada ya suala la rushwa hasa kwa watumishi wa Serikali kuendelea kuwa kubwa, Mkuu wa Mkoaa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda ametangaza ofa kwa wakazi wa jiji hilo muda na wakati wowote kujitokeza katika ofisi yake kuchukua kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia endapo Mwananchi ameombwa rushwa na watumishi hao wa Serikali.
RC Makonda amebainisha kuwa kutokana na suala la watumishi hasa wa kada ya Afya kuwadai wananchi rushwa pamoja na maafisa wengine katika jiji la Dar es Salaam, amekuja na Mkakati huo wa kutoa fedha kwa kiasi chochote kile ambacho Mwananchi atakiitaji endapo ataombwa rushwa na mtumishi wa Serikali ndani ya Mkoa wake.
Aidha, Makondna pia amewataaka wananchi kuzingatia sheria na kanuni mbalimbali zilizowekwa bila kuvunja sheria na kubainisha kuwa, yeye na timu yake wataendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi popote pale walipo ndani ya Jiji.
Kwa upande wa watu wanaofanya shughuli za kuombaomba barabarani, RC Makonda amewataka wananchi kusitisha hatua ya kuwapatia pesa watu hao pamoja na watoto wao kwani wengi wao wamegeza suala hilo kama mtaji na kwa sasa wanandaa utaratibu maalum wa kuweza kuwaondoa kwenye maeneo yote ya Jiji.