Ukitaka mtoto wako awe na akili nyingi fanya hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukitaka mtoto wako awe na akili nyingi fanya hivi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mopaozi, Mar 8, 2012.

 1. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160


  Kila kunapokucha tunashuhudia mpasuko mkubwa wa maadili kwa watoto na vijana wetu, pamoja na baadhi ya watoto kuwa na akili za kuzaliwa, watoto wengi wameharibikiwa na akili. Wengi ukiwaona wana uwezo mzuri, ila akili zao zimeharibiwa na malezi. Kumbuka Mungu anasema "Kumcha Bwana ni chanzo cha Maarifa…" Mithali 1:7. Wazazi wengi tunawalaumu watoto kwa kutokuwa waadilifu, ni jambo la kawaida kusikia "Heri nisingezaa kuliko kuwa na watoto kama hawa". Mambo yafuatayo yanachangia kuharibu akili ya watoto:


  1. Wazazi hawana Muda wa kuwafundisha watoto neno la Mungu ambalo ndilo chanzo cha Maarifa yote ya uadilifu na kuwa na Hekima katika jamii, kuna wasomi wengi lakini sio wa kutegemewa katika jamii "They are hopeless". Wazazi wengi wanakazania elimu ya kawaida, hiyo ni sawa, lakini elimu bila Mungu ni hatari, na ndicho tunachokiona siku hizi.

  2. Ugonvi wa Wazazi na Maisha yasiyo na Amani na Upendo kati ya wazazi – Watoto wanaathirika kisaikolojia wanapoona Baba na Mama wanagombana, hasa wanapoona mmoja anaonewa, na mwingine kuonekana katili. Watoto wako "very sensitive" na jambo hilo, na wakati wote wanakuwa ni "Upset Minded", hali hii inaathiri uwezo wao wa akili. Wazazi acheni magonvi mbele ya watoto ni hatari.

  3. Malezi ya Mtoto yanaanzia Tumboni, hakikisheni mama akiwa mja mzito, ale vyakula vyenye virutubisho kwa ajili ya kujenga Afya na Akili ya Mtoto. Hasira na Moyo wa huzuni kila mara huathiri mtoto tumboni. Vileo havitakiwi kabisa, vina athari kubwa kwa mtoto.

  4. Kumbuka chochote unachonena na kutenda mbele ya mtoto ndiyo elimu unayomfundisha. Kuna watu midomo haina Breki, wanaporomosha matusi hadi ya nguoni, ni wakali, na kila saa midomo iko juu, na tabia ya kuwadanganya watoto kuwa huyu ni Uncle, na usiku anahamia chumba cha baba na Mama, huo ni Uasherati na uzinifu, watoto lazima wataiga tabia hizo, na wakiwa vija wakubwa unaanza kuwalaumu.

  5. Chumba cha kulala kiwe na faragha, wazazi wengi wanalala na watoto, na vitoto vya siku hizi vinakomaa kabla ya wakati, utafikiri kamelala kumbe kanajisikilizia, huku kamefumba macho kabla hakajaiba kuchungulia. Hivi unafikiri michezo ya watoto ya Baba na mama unafikiri wanaitoa wapi? wanaigiza hata mama anavyolia, kilio cha furaha. Kwa ujumla hayo ndiyo yanajaza akili zao hadi wanaenda kuchora kwenye karatasi za mitihani.


  Wazazi wasilale na watoto chumba kimoja, pia chumba kiwe na milango inayofaa na dari lisiwe wazi, liwe na "sealing board". Siku hizi nyumba za kupanga zimekuwa changamoto kubwa kuharibu tabia za watoto na vijana. Vyumba havina siri, Vijana na watoto hawapati usingizi usiku kwa sababu ya starehe kutoka vyumba visivyo na faragha. Wazazi watawajibika kwa kuharibu akili za Vijana na watoto wasipozingatia ushauri huu.

   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  umenena na ubarikiwe sana
   
 3. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Ushauri mzuri, lakini nahisi ni mgumu kidogo utekelezaji. Kwanza dini hazina mvuto siku hizi baada ya kufanywa biashara zaidi. Wazazi hatuendi na watoto wanaiga, ngoja tujikongoje katika hili. Pili mtoto ni mmoja miaka 2 - 4, alale chumbani peke yake, ngumu kidogo. katika umri huo wengi wanakojoa kitandani kwa hiyo anahitaji kuamshwa mara kwa mara ili tabia isiendelee. kuhusu Matusi na maneno yasiyofaa labda tuhame uswahilini maana tayari mamboyalishaharibika huko!

  Umesahau swala la nidhamu ya mavazi naongezea. Baba unaevaa kata K, mikufu mikubwa, heleni, unasuka nywele, unapaka wanja, unatinda nyusi -UJUE UNAMUANDAA MTOTO WAKO KUWA SHOGA. Kwa upande wa mama sisemi leo ni siku yenu duniani, ila mnajua sana tu!
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Mleta mada umenena lakini hembu angalia na sisi tuaoishi kwenye nyumba za TEMBE je tutawezaje kuwatenga watoto wetu saa ya malazi usiku?
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kitu kingine kinachochangia upungufu wa akili kwa watoto wetu ni lishe bora tunawapa sembe badala ya dona,ngano iliyokobolewa n.k wataalamu wanasema nafaka isiyokobolewa ni inasaiDia sana katika makuzi ya akili ya mtoto saga mahindi yasiyokobolewa changanya na mtama na uwele kwa afya bora ya akili za watt wetu
   
 6. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  kote umechangia bora lkn hapo neno la Mungu hivi hawa ambao hawaabudu mbona wanamaarifa na uelewa mpana. mimi naona ungewa utawafundishe maadili mema na sisi wazazi tuwa mfano haya neno la Mungu naweza kusema ni sumu kwenye fikra zetu kila mtu anawajibika kwa imani yake. tuwafundishe watoto wetu uzalendo
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nahisi Mwanaasha alikosa mambo flani!
   
 8. M

  Makupa JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu mbona umesahau Tv nazo ni sumu kali mno kwa watoto, nilishangazwa kuona watoto wa miaka miwili wanapigana busu la ndimi
   
 9. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mi nakubaliana na namba tatu tu! Haya mengine si kweli. Wazazi wangu mimi ndo niliwashawishi kwenda kanisani na nimesoma na watoto wa wachungaji walikuwa wanafeli sana tu,wazazi walikuwa in a polygamist ndoa so mnajua nini kinatokea kuhusu ugomvi, sikumbuki niliacha kulala na wazazi lini lakini nakumbuka baba na mama nilicheza nikiwa na miaka mitatu(kuna dada nilimkojoleaga machoni baada ya kunisura,sijui yuko wapi yule dada), sikutukanwa matusi lakini nilikuwa nakaripiwa sana. Nimekuwa na akili kama kawaida tofauti na hawa watoto wa siku hizi. Tusitafute majibu mepesi kwa maswali magumu. Mifumo yetu ya elimu imeharibu kizazi hiki! Mtu anaanza la kwanza mpaka la saba na mitaala imebadilishwa mara saba. Shuleni watoto wanafundishwa kukariri maswali na majibu na sio kuelewa, ukichezesha lugha kidogo tu lazima waandike verse.
   
 10. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu,mi kuna Mwanafunzi ana mimba yangu yupo home. Ngoja nianze kumrisha msosi wa maana
   
 11. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  wakifika umriwa miaka 15 wafungulie account
  waonyeshe kadi zao za bank akuna mtoto anaetaka kurithi shida sikuhizi hili nalolitasaidia kusoma kwa bidii
   
 12. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unaonaje ukijisalimisha POLISI kwanza kwa kumharibia maisha yake huyo mwanafunzi!! Yaani hujafikilia kuwa alipaswa kusoma kwanza halafu hiyo mimba ije kwa wakati wake?
  Huna huruma kwa watoto wa wenzako?
   
 13. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Watoto wetu wapunguze kuangalia tv na wawe wanasoma kupata knowledge kuliko kufaulu mitihani
   
Loading...