Ukitaka kuwa "mwanasiasa" jitahidi sana usiwe mtu wa aibu wala hasira

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,476
2,000
Kinachoendelea sasa hivi katika nyanja ya siasa hapa Tanzania kinasadifu kitu kilichowahi kusemwa na mtangazaji/mzungumzaji mmoja wa kituo cha clouds fm

Mtafakari Mwambe anaita vyombo vya habari, anatangaza kwamba kwa kutumia haki yake akiwa na akili timamu anajiondoa chadema na kujivua nafasi zote alizokuwa nazo ikiwemo ubunge. Polepole anampokea.

Halafu ghafla anaitwa arudi bungeni, anaitika anaenda bila aibu!

Mtafakari Lijialikali, anatumia muda wa kutoa mchango wake kwenye bajeti, anashutumu chama chake, analia, anaomba kazi ccm tena anamuomba Spika!

Watafakari wabunge wa chadema, wanalilia lockdown, wananyimwa. Wanalilia basi wapimwe wananyimwa. Wanaamua kujitenga, halafu wanarudi kuchanganyikana na ambao hawajapimwa wala kujitenga.

Watafakari wabunge viti maalum, wamepigana, wameonwa, wameteuliwa, kabla ya bunge kuisha wanajiondoa chamani wanahamia chama kingine kwa kutangaza hadharani mbele ya watoto wao, wajukuu, waume/wapenzi kwamba kwa miaka yote mitano walikuwa wana "enjoy" manyanyaso ya kingono

Kama si ku enjoy, kwanini uvumilie unyanyasaji wa kingono kwa miaka mitano?

Mwisho kabisa mtafakari, Spika Ndugai na matendo yake tangu mwaka huu uanze dhidi ya upinzani.

Baada ya kutafakari yote hayo na mengine mengi ambayo unayafahamu fikiria pia kwamba wakati wanafanya hayo wengine wana watoto, wajukuu, mke/mume na wanayaona yanayofanywa na Baba/Mama, Babu/Bibi, nk

Kama ni mtu wa aibu aibu na hasira hasira na kutafakati tafakari sana kila kabla ya kutenda jambo, siasa za bongo zinakushinda asubuhi mapema
 

Kalesya

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
655
1,000
Welevu wamekaa kimya, ndo sababu mbumbumbu wametamalaki kwenye siasa za Tz.
Mbumbumbu anapoongoza hujaa hofu na wasiwasi na kuropoka kwasababu anajua welevu hawapo pamoja nae.
 

Pelle mza

JF-Expert Member
May 15, 2008
2,919
2,000
......fikiria pia kwamba wakati wanafanya hayo wengine wana watoto, wajukuu, mke/mume na wanayaona yanayofanywa na Baba/Mama, Babu/Bibi, nk..
Noma, Amewa-R.Kelly wamama wa viti maalumu mpaka wametoka nduki mmoja mmoja!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom