doriani
Member
- Nov 24, 2019
- 42
- 38
Ukitaka kuuwa taifa na utaifa, wanyime watu uhuru wa kuhoji na kutowa mawazo yao. Ukitaka kuuwa Demokrasia, wanunue wabunge na wawakilishi wa watu waungane na watawala, wape marupurupu mazuri kutokana na kodi za watawaliwa, wapige msasa wageuke kuwa tabaka maalumu lisiloweza kuhojiwa au kukosolewa, wafanye kuwa waione kazi ya ubunge na Uwakilishi kuwa kazi ya kudumu kwa udi na uvumba, wape nyenzo za kulinda nafasi zao. Mshahara na posho nono, pencheni na kifuta jasho mwishoni mwa kipindi chao, katikati ya umaskini uliokithiri.
Tangaza demokrasia na utawala bora kwa jina tu kuvutia misada kutoka nje na wawekezaji. Wagawe wabunge na Wawakilishi kwa misingi ya hoja za Chama Tawala na hoja za wapinzani katika misingi kama hoja hizo ni za manufaa kwa taifa. Endesha serikali kwa usiri mkubwa ili watu wasijuwe yanayotendeka,wasitukizie kwa kila jambo.
Sahau kabisa lugha ya mtu mdogo na maskini, kwani hana cha kukupa wala kuchagua katika taifa, hapo utakuwa umepanuwa ufa kati ya walionacho na wasio kuwa nacho.
Zikemee Mahkama na Bunge kwa maamuzi usio ya penda wewe. Wakemee waandishi kwa kuandika mambo yanayowaamsha jamii. Jifanye kuwa taifa ndio wewe na wewe ndio taifa. Hapo utakuwa umefanikiwa kujiundia bomu la kukulupukia wewe mwenyewe.
Wazee wanatwambia madaraka yote Hulevya, lakini madaraka makubwa Hulevya zaidi, mtu mpe madaraka atayatumia vibaya, lakini mpe madaraka makubwa zaidi atayatumia vibaya zaidi.
Katika kipindi hiki cha utanda wazi, haitupasi kuzichukulia kelele za watu wadogo kama kelele za watu wasio na maana la kutwambia. Hatupaswi kutangaza demokrasia na utawala bora juu ya mapaa ya nyumba kwa sababu tu ya kuvutia misada.
Hali hiyo imepelekea raia kuwaigopa watawala na watawala wanawaogopa raia. Watawala wanaogopa kuulizwa, na raia wanaogopa kuuliza.