Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kilimasera, Jan 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wanaume wote raia wa kigeni watakaotaka kuwaoa wanawake wa nchini Tajikistan watalazimika kuzifungua waleti zao na kuwanunulia nyumba wake zao kabla ya ndoa kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo leo.
  Kuanzia leo mwanaume yeyote ambaye si raia wa Tajikistan ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Urusi, atalazimika kumnunulia nyumba mwanamke anayetaka kumuoa kama sharti kubwa la kwanza kabla ya harusi.

  Hiyo ni kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa leo na bunge la nchi hiyo ambapo sharti kubwa lingine lililopitishwa ni kwamba mwanaume atalazimika kukaa mwaka mmoja nchini humo kabla ya kupewa kibali cha kuruhusiwa kuoa.

  Watunga sheria wa Tajikistan wamesema kuwa sheria hiyo mpya itasaidia kuwalinda wanawake wanaotelekezwa na waume zao raia wa kigeni.

  "Baada ya ndoa kuvunjika, majukumu ya kuwalea watoto huangukia kwa mama na serikali", alisema mwakilishi wa rais bungeni, Dzhumakhon Davlatov.

  Davlatov aliongeza kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza idadi ya wanaume watakaowatekeleza wake na watoto wao.

  Wanaume wengi toka Afghanistan na Iran, ndio wanaoongoza kwa kuoa wanawake wa Tajikistan ingawa katika miezi ya karibuni kumekuwa na ongezeko la wanaume wengi toka nchi za barani ulaya, Marekani na Japan wanaooa wanawake wa Tajikistan.

  Tajikistan ni nchi maskini iliyokuwa miongoni mwa nchi zilizounda Umoja wa Sovieti na uchumi wake umetetereka tangu mwaka 1990 kutokana na matatizo ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
   
 2. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sheria hii ilitakiwa kuwepo hapa kwetu Tanzania,na ingesaidia sana wale wadada walioachiwa vichotara vya kitaliano kuanzia Isaka,Kagongwa,Kahama,Masumbwe, Ushirombo na kuendelea mpaka Ngara.
   
 3. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  hii ya ukwel yan kwa lugha nyngne marufuku mgen kama mackin kuoa yan dah safi
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  kwa bonngo vin'gast wote watataka kuolewa na foreigners tu hata kama vibabubabu
   
 5. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh hii kali.

  Wachina nasikia huko singida na tabora amefanya mambo. Serikali ichangamkie dili ili watoto wapate matunzo.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii imetulia!
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hata hapa tz hii sheria ipo ila kwa kificho. Dada zetu wajanja wanaitumia sana!
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wanaangalia mawe kama huna mawe unakosa mke!
   
 9. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,107
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  hii ingekuwaa bongo ingekuwaa poaa sanaa,tushaa chokaa kulea ma uncle ma point 5 banaaa
   
Loading...