Ukitaka kuoa au kuolewa hakikisha unamshirikisha baba au mama yako

Kama wamekufa wote, inakuaje??

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hiyo ni case ambayo haiwezi kutokea muolewaji na muowaji wote hawana wazazi hata mmoja.. Kumbuka Furaha ya Ndoa yenu ni Pamoja na Wazazi wenu kuona wajukuu na furaha ya wajukuu ni pamoja na kuwashirikisha
 
sijaelewa, niwashirikishe nataka kuolewa au niwashirikishe wanichagulie mume sababu tu waowalichaguliwa?? halaf futa kauli kuwa hakuna case ya wanaooana wote kukosa wazazi ipo sana,

ndoa ni maamuzi binafsi wewe unayeolewa au kuoa ukishakubali hilo limetosha wao watakushaur tu namna ya kuishi kwenye ndoa yako.
 
Hiyo ni case ambayo haiwezi kutokea muolewaji na muowaji wote hawana wazazi hata mmoja.. Kumbuka Furaha ya Ndoa yenu ni Pamoja na Wazazi wenu kuona wajukuu na furaha ya wajukuu ni pamoja na kuwashirikisha
Duuh aisee nmeshangaa ati ni case ambayo haiwez kutokea we unaish dunia gani ndgu yangu ulicho nacho ww sio wote wanavyo uwe unawaza nje ya box pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada mnamshambulia bure tu kufikiri,wazazi ndoo baraka za mtoto duniani.Hata Mungu alietuumba kasema labda kama hatuamini kuwepo kwa muumba.

Unapowashirikisha pale ambapo unaona umempata mwanaume au mwanamke nao wao wakatoa ushauri na kukupa baraka ,mambo mengi utaepukana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni case ambayo haiwezi kutokea muolewaji na muowaji wote hawana wazazi hata mmoja.. Kumbuka Furaha ya Ndoa yenu ni Pamoja na Wazazi wenu kuona wajukuu na furaha ya wajukuu ni pamoja na kuwashirikisha
natumai umeteleza tu!
 
Ushauri,

Ukitaka kuoa au kuolewa kamwe usimdharau mama au Baba yako. Hata Babu yako amedumu na bibi yako kwa kuwa alichaguliwa Mke au Mume na Wazazi wake..

Ni Ushauri tu.
Watakuambia hilo ni jambo binafsi.
Naongezea:
1.chagua mtu wa Imani yako ( ambaye beliefs zenu ,ziwe za kikabila na kidini zinaendana)
2.Pata vetting ya wazee ( hawa wameona mengi na usipuuze ushauri wao)
 
sijaelewa, niwashirikishe nataka kuolewa au...

ndoa ni maamuzi binafsi wewe unayeolewa au kuoa ukishakubali hilo limetosha wao watakushaur tu namna ya kuishi kwenye ndoa yako.

Hakuna asiyejua matokeo ya hizi ndoa zetu, ambao tunajifanya tunajuana wenyewe na tunapendana sana.... hivyo tumechaguana tuoane.

Hivyo basi, siku nawe ukiwa mzazi halafu uone wanao wanajiolea tu.... ndo utaelewa unachosema leo.
 
Mleta mada mnamshambulia bure tu kufikiri,wazazi ndoo baraka za mtoto duniani.Hata Mungu alietuumba kasema labda kama hatuamini kuwepo kwa muumba.

Unapowashirikisha pale ambapo unaona umempata mwanaume au mwanamke nao wao wakatoa ushauri na kukupa baraka ,mambo mengi utaepukana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaelewa ila kwa kuwa baadhi yao wameshajisseendoff utetezi wao ni huo unaouana ila madhara ni Makubwa sana kujiamulia wa kuoa bila kushirikisha Wazazi au Walezi hata kama unawazidi kipato au Elimu au Cheo au wewe ndiyo wanayekutegemea. Kumbuka Mabega hayawezi kuzidi Kichwa. Wewe Mtoto utabaki kuwa bega tu kwa Wazazi wako na huwezi kuwaidi chcohote.

Ndiyo Maana ukiona ndoa nyingi zinavyoharibika wa Kumkimbilia haraka haraka ni Mzazi wako ...
 
Hakuna asiyejua matokeo ya hizi ndoa zetu, ambao tunajifanya tunajuana wenyewe na tunapendana sana.... hivyo tumechaguana tuoane.

Hivyo basi, siku nawe ukiwa mzazi halafu uone wanao wanajiolea tu.... ndo utaelewa unachosema leo.
Upo Sahihi kabisa Mkuu.. Kumbuka na sisi ni wazazi wa watoto wetu kama leo tukiwadharau wazazi wetu kuwashirikisha jambo zito kama hilo halafu unakuja kuwashirikisha kwenye Michango ni utovu wa Nidhamu kabisa na kumbuka Ndoa unakaribisha ukoo tofauti kwenye koo yako sasa ikimshirkisha mzazi kuna jicho la tatu litaoa yale ambayo wewe kwa mihemuko huwezi kuyaona.
 
Ushauri,

Ukitaka kuoa au kuolewa kamwe usimdharau mama au Baba yako. Hata Babu yako amedumu na bibi yako kwa kuwa alichaguliwa Mke au Mume na Wazazi wake..

Ni Ushauri tu.
Kuna mama mmoja nilimuomba anisaidie kutafuta mke
Akaniambia siku hizi watu huwa hawachaguliwi mtu wa kumuoa au wa kuolewa nae
 
Hiyo ni case ambayo haiwezi kutokea muolewaji na muowaji wote hawana wazazi hata mmoja.. Kumbuka Furaha ya Ndoa yenu ni Pamoja na Wazazi wenu kuona wajukuu na furaha ya wajukuu ni pamoja na kuwashirikisha
Unaongea kitu cha kufikirika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom