Ukitaka kumtongoza mwanamke tumia sikio la kushoto…………utampata………….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukitaka kumtongoza mwanamke tumia sikio la kushoto…………utampata………….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 30, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wataalamu wamebaini kwamba, sikio la kushoto ndilo likilishwa kauli ya upendo hushika sana kauli hiyo na aliyeambiwa kauli hiyo huwa hawezi kuisahau kirahisi. Uwezekano wa jambo hili siyo suala la kudhani, kwani linaweza kuelezewa kutokana na mfumo wa akili. Kauli hii inaweza kuwashangaza wengi, lakini ndivyo wataalamu wanavyoeleza.

  Kwa nini wanasema hivyo?

  Wanasema hivyo kutokana na ukweli kwamba sikio la upande wa kushoto linathibitiwa na upande wa kulia wa ubongo. Upande huu wa kulia wa ubongo ndiyo ambao unashughulika na hisia za binadamu kama furaha, huzuni na mengine. Kwa kuwa upande wa kulia wa ubongo ndiyo unaodhibiti hisia za binadamu na sikio la kushoto linadhibitiwa na upande huu wa ubongo, kauli zote za kihisia zikipitia kwenye sikio la kushoto zinakuwa na ugumu katika kufutika. Ugumu huu unatokana na ukweli kuwa zimeingilia mahali pake.

  Kwa hiyo kama tunataka kuhakikisha kwamba wapenzi wetu hawasahau kirahisi au maneno tunayowaambia kuhusiana na jinsi tunavyowapenda yanawaingia kwa kina, inabidi tuzungumze nao kwa kupitishia maneno hayo kwenye sikio la kushoto……………
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,680
  Trophy Points: 280
  Gud mrng dingi.. . . .Ngoja nijitahidi kila nikimyatia Smile nimuende upande wa kushoto.Eti anadai ana bikra!Kama ni kweli si nitakua luck guy?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Naomba niweke angalizo: Hapa sizungumzii yale mapenzi ya mwanamke kuvutiwa na mwanaume kutokana na rasilimali anazomiliki...Gari, nyumba, biashara kubwa au ukwasi alio nao mwanaume, kwani hapo mwanaume hahitaji kutumia gia kubwa sana kumpata mwanamke........Mimi nazungumzia mapenzi ya dhati lakini sio ya kuhemkwa. Nazungumzia mapenzi ambayo yanatoka moyoni kabisa.

  Maana najua kuna watu watakuja hapa na kusema shida yote hiyo ya nini wakati siku hizi chapaa inaongea...........!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sio kusudio langu kuwafundisha uasherati...............Kama umempenda Smile peleka posa si ameshasema ni BIKRA...............!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,680
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi,sasa nitaendaje kwao bila kuongea nae?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ngoja nirudie kusoma anatomy na physiology ya ubongo kwanza....Nitarudi baadaye

  Babu DC!!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nikusaidie kukuwekea link au?
   
 8. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mhhhh....Nitarudi baada ya majaribio.
   
 9. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya...
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ngoja nimnong'neze huyu mdada hapa kwamba amependeza kwa kutumia sikio lake la kushoto,, halafu nitrudi na mrejesho
   
 11. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  hii tamu hii. Nishahfadh panapostahli
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afadhali umeweka angalizo mapema
   
 13. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  nifanyeje ili kuhakikisha sikio la kushoto linatumika in the gradual loving processes?
   
 14. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Na ukishampata ukamuacha hiyo kauli iliyohifadiwa vilivyo kwenye ubongo itachukua muda gani kufutika?
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nitashukuru sana!
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
 17. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unavyomwambia nakuacha unatumia sikio la kulia.
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Una akili wewe.....................Nakupa TANO..............!
   
 19. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duuh sasa ndio nimejua kwanini I am not successful in love life, I am somehow kiziwi upande wa kushoto. Sitaki kuamini!
   
 20. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yaani Hiyo Avatar Yako nimeizimiaje,,,, Nimependa Lipstick hiyo ukiangalia Half of your Lips On the left ndo ziko red. Are you trying to tell us something like we should move toward U r left ear??
   
Loading...