Ukitaka kujuwa kuwa kiswahili hakijitoshelezi sikiliza 'Clouds FM'

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,674
1,685
Sidhani kama ukienda Uingereza utakuta radio zao zina majina ya Kiswahili lakini sisi kwa kuanzia hawa Clouds FM, Capital FM, Radio Free Africa, Voice of Tabora na kadhalika, sasa ukitaka kudhihirisha kuwa kiswahili kina mapungufu mengi wewe sikiliza hiyo 'Clouds FM' vipindi vyao vya 'Sports' mtangazaji wao Jeffrea.
Huyu kwa ukweli anaudhi udhi udhi mno.
 
Neno tosheleza katika uwanja wa lugha si zuri katika kuielezea kwa sababu sidhani kama kuna lugha inayojitosheleza hapa duniani na ndiyo maana mara kwa mara misamiati mipya huibuka.

Ila lugha hukua na kupanuka endapo tu wazungumzaji wake wataamua kuikuza na kuipanua.

Kwa sasa Kiswahili hakinipi matumaini ya kukua na kupanuka.
 
kukwepeka inawezekana tena vizuri sana, cha msingi ni serikali yetu kuwa komavu hasa katika kipengele cha kutoa maamuzi, najua inashindikana kwa sababu jamii yetu bado changa, tunaishi kwa misaada mingi toka nje hivyo tu kama television na remoti.
 
mawazo mgando hasa yani ukichomekea maneno ya kiingereza unaonekana msomi inakeraaaaa mno
 
Sidhani kama ukienda Uingereza utakuta radio zao zina majina ya Kiswahili lakini sisi kwa kuanzia hawa Clouds FM, Capital FM, Radio Free Africa, Voice of Tabora na kadhalika, sasa ukitaka kudhihirisha kuwa kiswahili kina mapungufu mengi wewe sikiliza hiyo 'Clouds FM' vipindi vyao vya 'Sports' mtangazaji wao Jeffrea.
Huyu kwa ukweli anaudhi udhi udhi mno.

Sasa ingaliitwa MAWIMBI RUDIA MAWINGU huoni kama watu wangechoka kuitamka, au hata kuiogopa !!
 
kiswahili ni lugha adhimu yenye misamiati ya kutosha ndio maana hata umoja wa mataifa na vyombo mbalimbali vya kimataifa vikiwemo bbc na deuch welle radio na vyuo vya kiswahili mfano beijing china na marekani na uingereza vinakitumia sana, tatizo liko hapa nyumbani kuanzia viongozi wetu wanahabari wetu mpaka watu w kawaida kabisa kuchanganya Kiswahili na kiingereza ili tu waonekane wa kisasa na wasomi
mwishowe wanajikuta hawawezi kuongea kiswahili fasaha wala kiingereza fasaha!
hebu jaribu kusoma magazeti ya udaku na hizi redio za udaku utatamani kutapika jinsi wanavyochanganya kiingereza na kiswahili
tatizo linaanzia bakita wapowapo tu, wakifuatiwa na walimu na wakufunzi kwenye shule na vyuo vya uandishi ni uvundo mtupu mwisho ni wamiliki wa vyombo vya habari
 
msiletege masuala ya hii redio kwenye jukwaa hili la great thinkers au wewe ni kibon..e?
 
Lukindo, nilitaka kusisitiza jinsi matumizi YASIYO SAHIHI ya kiswahili yanavotumika na watangazaji na si kuilenga Clouds FM ambayo haina tatizo lolote, tena wanajitahidi mno kutuhabarisha mambo muhimu yanayotuhusu. Tatizo ni huyu mtangazaji wao Jeff anavokera kwa kuchanganya KISWAHILI na Kiingereza licha ya kuwapelekea ujumbe wa kumuomba ajirekebisha.
Tafakari.
 
Sidhani kama ukienda Uingereza utakuta radio zao zina majina ya Kiswahili lakini sisi kwa kuanzia hawa Clouds FM, Capital FM, Radio Free Africa, Voice of Tabora na kadhalika, sasa ukitaka kudhihirisha kuwa kiswahili kina mapungufu mengi wewe sikiliza hiyo 'Clouds FM' vipindi vyao vya 'Sports' mtangazaji wao Jeffrea.
Huyu kwa ukweli anaudhi udhi udhi mno.

Sasa kwa wewe na huyo Jeffrea kutokujua (kujua mind you, not kujuwa) Kiswahili ndio kuna maanisha Kiswahili hakijajitosheleza?
 
Nakushukuru mno kwa kunielewa.
kiswahili ni lugha adhimu yenye misamiati ya kutosha ndio maana hata umoja wa mataifa na vyombo mbalimbali vya kimataifa vikiwemo bbc na deuch welle radio na vyuo vya kiswahili mfano beijing china na marekani na uingereza vinakitumia sana, tatizo liko hapa nyumbani kuanzia viongozi wetu wanahabari wetu mpaka watu w kawaida kabisa kuchanganya Kiswahili na kiingereza ili tu waonekane wa kisasa na wasomi
mwishowe wanajikuta hawawezi kuongea kiswahili fasaha wala kiingereza fasaha!
hebu jaribu kusoma magazeti ya udaku na hizi redio za udaku utatamani kutapika jinsi wanavyochanganya kiingereza na kiswahili
tatizo linaanzia bakita wapowapo tu, wakifuatiwa na walimu na wakufunzi kwenye shule na vyuo vya uandishi ni uvundo mtupu mwisho ni wamiliki wa vyombo vya habari
Sasa tufanye nini na wizara ya utamaduni/baraza la kiswahili tunavo vinaponda pesa yetu?
 
Sasa kwa wewe na huyo Jeffrea kutokujua (kujua mind you, not kujuwa) Kiswahili ndio kuna maanisha Kiswahili hakijajitosheleza?
Huyu ni mtangazaji wa radio anapaswa kufahamu kuwa jinsi ya kupasha habari kuna athari gani kwa msikilizaji!
Tafadhari msikilize japo siku moja tu.
 
Hoja yako ilitakiwa ijikite kuwa waandishi wa habari hawatumii Kiswahili fasaha na sio kwenye Kiswahili kutojitosheleza.

Kwa sababu kama Kiswahili hakijitoshelezi kama ulivyodai kwenye kichwa cha habari hapa, basi huyo Jeff na mwandishi mwengine yoyote hana kosa kwa kuchanganya na Kiingereza
 
Sasa ingaliitwa MAWIMBI RUDIA MAWINGU huoni kama watu wangechoka kuitamka, au hata kuiogopa !!

Kwani hawawezi kuita redio yao REDIO MAWINGU? Mbona Radio Tumaini na Radio Maria wameweza? Au kwa sababu hizi mbili si redio za kibiashara? Kwa nini tusiachane na upuuzi wa kuita vituo vyetu majina ya ajabu ajabu? Mara utasikia:-
  • Choice FM
  • Passion FM
  • Times FM
  • Clouds FM
  • Radio One
  • Radio Free Africa
  • East Africa Radio
  • Kiss FM
  • TBC FM (kutoka Radio Tanzania Dar Es Salaam) etc etc.
Upuuzi mtupu!
 
Kwa upande mmoja nakubaliana nawe, lakini sio Jeff pekee anayefanya hivo ukiachilia mbali WAHESHIMIWA wabunge hivi karibuni nae rais wetu nilimsikia akichanganya lugha katika ufunguzi wa barabara.
Hoja yako ilitakiwa ijikite kuwa waandishi wa habari hawatumii Kiswahili fasaha na sio kwenye Kiswahili kutojitosheleza.

Kwa sababu kama Kiswahili hakijitoshelezi kama ulivyodai kwenye kichwa cha habari hapa, basi huyo Jeff na mwandishi mwengine yoyote hana kosa kwa kuchanganya na Kiingereza
Nimemtumia huyu mtangazaji kwani amekuwa hajirekebishi licha ya ujumbe aliokwisha tumiwa na wasikilizaji wake, ndo maana nikadhani labda KISWAHILI ni tatizo kujieleza!
 
Kwa upande mmoja nakubaliana nawe, lakini sio Jeff pekee anayefanya hivo ukiachilia mbali WAHESHIMIWA wabunge hivi karibuni nae rais wetu nilimsikia akichanganya lugha katika ufunguzi wa barabara.Nimemtumia huyu mtangazaji kwani amekuwa hajirekebishi licha ya ujumbe aliokwisha tumiwa na wasikilizaji wake, ndo maana nikadhani labda KISWAHILI ni tatizo kujieleza!

Hoja ninayoizungumzia hapa ni kuwa iwapo unatueleza kuwa Kiswahili hakijitoshelezi (kama ulivyofanya kwenye kichwa cha habari hii), basi huwezi kumlaumu mtumiaji Kiswahili kuchanganya Kiswahili na lugha nyengine

Iwapo unasema Kiswahili kinaweza kujitosheleza (walau kwa kiwango kikubwa zaidi ya inavyoonekana sasa), basi kichwa chako cha habari kimetupoteza.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom