Ukitaka kujuwa kuwa kiswahili hakijitoshelezi sikiliza 'Clouds FM'

Kwa hili la kukibananga kiswahili kwa kweli waandishi wa habari hasa wa redio na magazeti wanaongoza, yaani siku hizi imekuwa jambo la kawaida kabisa kusikia mwandishi wa habari akisema " nitacheza nyimbo ya msanii fulani ( anataja jina), huku akiwa amekusudia kucheza wimbo mmoja tu na wala sio nyimbo za msanii huyo!
 
Kiingereza ni lugha ya kimataifa huwezi kwepa ndugu
Zipo nyingi tu lugha za kimataifa ikiwa na Kireno, Kijerumani, Kihispania, Kifaransa, Kihausa, Kiswahili, Kitaliano na kadhalika. Tatizo sisi tumekiheshimu Kiingereza kama ni muarobaini, hivi BARAZA LA KISWAHILI lingeamua kikikuza Kiswahili kwa kuchukuwa MANENO toka katika LUGHA ZETU ZA ASILI kingekuwa na radha nzuri mno.
 
Kwa hili la kukibananga kiswahili kwa kweli waandishi wa habari hasa wa redio na magazeti wanaongoza, yaani siku hizi imekuwa jambo la kawaida kabisa kusikia mwandishi wa habari akisema " nitacheza nyimbo ya msanii fulani ( anataja jina), huku akiwa amekusudia kucheza wimbo mmoja tu na wala sio nyimbo za msanii huyo!
Hapa umenikumbusha mtangazaji anatuambia 'na sasa habari za michezo za kimataifa, ligi kuu ya England imeendelea tena leo kwa....., Arsene Wenger kamshutumu mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano ......... mwisho wa habari za kimataifa'. Jamani, mie huudhika na kufikiri tatizo ni ELIMU ya shule au ni UKASUKU tuuuuu.
 
Hoja ninayoizungumzia hapa ni kuwa iwapo unatueleza kuwa Kiswahili hakijitoshelezi (kama ulivyofanya kwenye kichwa cha habari hii), basi huwezi kumlaumu mtumiaji Kiswahili kuchanganya Kiswahili na lugha nyengine

Iwapo unasema Kiswahili kinaweza kujitosheleza (walau kwa kiwango kikubwa zaidi ya inavyoonekana sasa), basi kichwa chako cha habari kimetupoteza.
Hakijitoshelezi, ndio maana wengine wanapitiliza.
 
Tatizo limeanzia na mji wa MZIZIMA kubitizwa Dar Es Salaam.
Kwani hawawezi kuita redio yao REDIO MAWINGU? Mbona Radio Tumaini na Radio Maria wameweza? Au kwa sababu hizi mbili si redio za kibiashara? Kwa nini tusiachane na upuuzi wa kuita vituo vyetu majina ya ajabu ajabu? Mara utasikia:-
  • Choice FM
  • Passion FM
  • Times FM
  • Clouds FM
  • Radio One
  • Radio Free Africa
  • East Africa Radio
  • Kiss FM
  • TBC FM (kutoka Radio Tanzania Dar Es Salaam) etc etc.
Upuuzi mtupu!
Tufanyeji maana wenzetu waliamua kuheshimu lugha zao za ASILI kwa mfano Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Malawi na kadhalika.
 
Hapa umenikumbusha mtangazaji anatuambia 'na sasa habari za michezo za kimataifa, ligi kuu ya England imeendelea tena leo kwa....., Arsene Wenger kamshutumu mwamuzi kwa kumpa kadi ya njano ......... mwisho wa habari za kimataifa'. Jamani, mie huudhika na kufikiri tatizo ni ELIMU ya shule au ni UKASUKU tuuuuu.

Tatizo la waandishi wetu ni ulimbukeni wa kutojua umuhimu wa tasnia yao ya habari katika jamii na athari ya upotoshaji wao kwa jamii, na hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na uvivu wao wa kutopenda kujifunza!
 
kukwepeka inawezekana tena vizuri sana, cha msingi ni serikali yetu kuwa komavu hasa katika kipengele cha kutoa maamuzi, najua inashindikana kwa sababu jamii yetu bado changa, tunaishi kwa misaada mingi toka nje hivyo tu kama television na remoti.
Mhn natilia shaka UCHANGA hapa, tuna wizara ya UTAMADUNI na kuongezwa BARAZA la KISWAHILI tokea UHURU, hawa jamaa kama wangeamua KUKIKUZA Kiswahili kwa kuchukua maneno toka LUGHA zetu za ASILI hivi sasa Kiswahili kisingechanganywa na Kiingereza. Neno "NG'ATUKA" limeingizwa na BABA WA TAIFA toka lugha yake ya ASILI ati kwa nini mengine yasiingizwe na kukifanya Kiswahili kiwe na asili ya KIAFRIKA badala ya Uarabu na Uingereza?
 
Hata Kingereza hakijitoshelezi, kama unabisha niwekee sentensi hii kwa Kingereza, ''Baba mimi ni mtoto wako wa ngapi?''
 
Tatizo la waandishi wetu ni ulimbukeni wa kutojua umuhimu wa tasnia yao ya habari katika jamii na athari ya upotoshaji wao kwa jamii, na hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na uvivu wao wa kutopenda kujifunza!
Hapo upo SAHIHI kabisa, utakuta huyo mtangazaji anayeng'ang'ania habari za huko England hata MAJINA ya vilabu kutamka sawia HAWEZI.
 
Hata Kingereza hakijitoshelezi, kama unabisha niwekee sentensi hii kwa Kingereza, ''Baba mimi ni mtoto wako wa ngapi?''

Tena Kiingereza ndiyo kimeazima maneno hadi kutoka kwenye Kiswahili. Kutoka kwenye Kilatini na Kifaransa ndiyo usiseme. Huko kimeazima balaa.

Ndiyo maana nikasema neno 'tosheleza' si zuri katika kuielezea lugha.
 
Niwekee basi hii sentesi kwa Kingereza, ''Baba mimi ni mtoto wako wa ngapi?'' Mie shule yangu ya kata kaka, naomba kusaidiwa
 
Tena Kiingereza ndiyo kimeazima maneno hadi kutoka kwenye Kiswahili. Kutoka kwenye Kilatini na Kifaransa ndiyo usiseme. Huko kimeazima balaa.

Ndiyo maana nikasema neno 'tosheleza' si zuri katika kuielezea lugha.
Ndio maana nina USHAWISHI wa kukiendeleza Kiswahili kwa kutumia maneno toka kwenye LUGHA ZETU ZA ASILI.
 
Neno tosheleza katika uwanja wa lugha si zuri katika kuielezea kwa sababu sidhani kama kuna lugha inayojitosheleza hapa duniani na ndiyo maana mara kwa mara misamiati mipya huibuka.

Ila lugha hukua na kupanuka endapo tu wazungumzaji wake wataamua kuikuza na kuipanua.

Kwa sasa Kiswahili hakinipi matumaini ya kukua na kupanuka.

kwann unasema hivyo? je unafikiri BAKITA bado hawajatimiza malengo yao?
 
kwann unasema hivyo? je unafikiri BAKITA bado hawajatimiza malengo yao?

Umeshawahi kutembelea tovuti ya BAKITA?

Je, BAKITA wameshawahi hata kutengeneza kamusi ya Kiswahili sanifu?

Je, kila mwaka kuna maneno gani mapya ambayo huingizwa kwenye kamusi yoyote ile ya Kiswahili sanifu?
 
kiswahili ni lugha adhimu yenye misamiati ya kutosha ndio maana hata umoja wa mataifa na vyombo mbalimbali vya kimataifa vikiwemo bbc na deuch welle radio na vyuo vya kiswahili mfano beijing china na marekani na uingereza vinakitumia sana, tatizo liko hapa nyumbani kuanzia viongozi wetu wanahabari wetu mpaka watu w kawaida kabisa kuchanganya Kiswahili na kiingereza ili tu waonekane wa kisasa na wasomi
mwishowe wanajikuta hawawezi kuongea kiswahili fasaha wala kiingereza fasaha!
hebu jaribu kusoma magazeti ya udaku na hizi redio za udaku utatamani kutapika jinsi wanavyochanganya kiingereza na kiswahili
tatizo linaanzia bakita wapowapo tu, wakifuatiwa na walimu na wakufunzi kwenye shule na vyuo vya uandishi ni uvundo mtupu mwisho ni wamiliki wa vyombo vya habari
Napenda sana Kiswahili...sana tu.
 
Umeshawahi kutembelea tovuti ya BAKITA?

Je, BAKITA wameshawahi hata kutengeneza kamusi ya Kiswahili sanifu?

Je, kila mwaka kuna maneno gani mapya ambayo huingizwa kwenye kamusi yoyote ile ya Kiswahili sanifu?
TOVUTI sijawah kutembelea na sijui kama ipo.
kamusi ya kiswahili sanifu naijua ile iliyotengenezwa na TUKI
Kuhusu misamiati mipya sijui vzr ila nisikilizapo lugha yetu ama lulu za kiswahili naona kama kuna maneno mapya ingawa sijui lini yaliingizwa.
swali kwako--- kinachokuza lugha ni maneno mapya ama wigo wa uongeaji(matumizi ya ) lugha husika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom