Ukitaka kujua viongozi wa kisiasa wamefanya elimu yako kuwa ya kichina jibu swali hil

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
409
Points
0

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
409 0
Wanabodi heshima kwenu,
Wanasiasa wa tanzania wameingilia kazi ya watalamu hasa elimu yetu.
Shule zimeanzishwa bila kukidhi vigezo vya kuitwa shule.
Sio hilo tu wameshindwa kutambua kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ngazi zote kwani watalamu wa china hawajui kiswahili wanafanyaje kazi tanzania?
Wameamua kukumbatia lugha ya wakoloni na mfumo wa kikoloni na lugha ya kiingereza bado watanzania wasomi wameshindwa kuimudu yamkini nawe ni mmojawapo.
Kama unabisha elimu yako si ya kichina kwa maana chini ya kiwango kutokana na siasa kutokuwa safi
Jipime kwa kujibu hili swali:
Badili sentensi hii kuwa ya kiingereza au iandike kwa lugha ya kiingereza.

"Baba hivi, Mimi ni mtoto wa ngapi katika uzao wako?
ahsanteni kwa majibu
Nitoe wito kukipigania kiswahili kwenye katiba mpya kiwe lugha rasmi ya kufundishia ngazi zote

mods naomba muiache jukwaa hili la siasa tupime nilichojadili
 

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
392
Points
225

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2012
392 225
HEY DADY,I'M A CHILD OF HOW MANY OF UR DESCENDANTS au unaweza ukasema HEY DADY.I'M CHILD OF WHICH NUMBER OF UR DESCENDANTS, HEY DADY,OF WHICH NO# DO I BELONG TO UR CHILDREN. Unaweza ukanisahihisha unajua kutafsiri sentensi moja kwenda lugha nyingine ni vigumu sana sio kiswa-english tu bali hata english-kiswahili na lugha yeyote ile hata awe mtaalam vipi haya mambo yanakushinda samtime mfano neno moja la kiingereza linaweza kupata tafsiri sahihi ya sentensi 2 za kiswahili na vice-versa.
 

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Messages
2,768
Points
2,000

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2012
2,768 2,000
Good, vizuri sana kwa mada hii.anacho jaribu kutuonesha mtoa maada ni kwamba sentesi hizo za kiingereza zitakuwa nyingi sana na tofauti sana.tofauti hizo zinasababishwa na na uelewa mdogo wa lugha yenyewe. sasa, kama lugha yenyewe ni shida, je tunaweza kuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kwa kujifunza kwa kutumia lugha tusiyo imudu? na ndio maana tupo hapa leo. wanasiasa hawajui kiingereza lakini wanaking'ang'ani kiingereza. watu hufikiri vizuri wanapo waza kwa LUGHA YAO.
 

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Messages
10,216
Points
1,250

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2009
10,216 1,250
tusikimbilie kingereza wakati hata kiswahili hatujui vizuri. Mtu anasema;
1. Kitu ambacho nilichofikiria...
2. Hii nyimbo ni nzuri...
3. Hilo la kwanza, lakini la pili...
4. Kwa niaba yangu...
5. Mimi kama mimi...
6. Leo ni tarehe moja, mbili (ni mosi, pili)...
7. Chini ya 'mvungu'...
8. Selasini, semanini, n.k......
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
10,995
Points
2,000

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
10,995 2,000
Wanabodi heshima kwenu,
Wanasiasa wa tanzania wameingilia kazi ya watalamu hasa elimu yetu.
Shule zimeanzishwa bila kukidhi vigezo vya kuitwa shule.
Sio hilo tu wameshindwa kutambua kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ngazi zote kwani watalamu wa china hawajui kiswahili wanafanyaje kazi tanzania?
Wameamua kukumbatia lugha ya wakoloni na mfumo wa kikoloni na lugha ya kiingereza bado watanzania wasomi wameshindwa kuimudu yamkini nawe ni mmojawapo.
Kama unabisha elimu yako si ya kichina kwa maana chini ya kiwango kutokana na siasa kutokuwa safi
Jipime kwa kujibu hili swali:
Badili sentensi hii kuwa ya kiingereza au iandike kwa lugha ya kiingereza.

"Baba hivi, Mimi ni mtoto wa ngapi katika uzao wako?
ahsanteni kwa majibu
Nitoe wito kukipigania kiswahili kwenye katiba mpya kiwe lugha rasmi ya kufundishia ngazi zote

mods naomba muiache jukwaa hili la siasa tupime nilichojadili
Hoja yako ingepata nguvu zaidi kama ungetoa mfano wa maneno ya kiswahili yanakosewa hapa JF kila siku tena na wahitimu wa chuo kikuu. Mtu anamaliza chuo hajui kuandika, kujieleza au kusoma kiswahili achilia mbali kiingereza. Ni wengi sana sana sana.
 

KIGENE

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
1,191
Points
1,500

KIGENE

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2011
1,191 1,500
Swala la kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia limeshajadiliwa kwa kina, swali linakuja je kiswahili chenyewe tunakijua na ni kswahili pekee hatukijui au na masomo mengine.
Vilevile tunapashwa kujiuliza inakuwaje ni sisi tu Tanzania tunashindwa kuimudu lugha ya watawala wetu wa zamani, wakati majirani zetu wanazimudu lugha za wakoloni wao.
Pamoja na kukikuza na kukienzi kiswahili bado wa Tanzania tunapashwa kujua lugha za mataifa mengine kwa vile hata mataifa yaliyoendelea bado yanajifunza lugha nyingine zinazotumika kimataifa.
Inaonekana kuna udhaifu katika ufundishaji wa kiingereza kwa sababu haiwezekani mtu afundishwe lugha hiyo hiyo kwa muda wa miaka isiyopungua ishirini na mwisho wa siku ashindwe kuimudu,wakati huohuo Mtanzania anaenda Urusi anasoma Kirusi miaka miwili harafu anamudu kusoma shahada yake vizuri.
 

MpangoA

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Messages
362
Points
0

MpangoA

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2012
362 0
Tanzania tunaweza kitu kimoja tu...Siasa za maji taka! Si lugha, si mpira, si uongozi, si utawala, si ukulima, si biashara, si utalii, si urembo, si kutetea mipaka yetu.

Acheni watanzania wajikomboe kwa kujua kiingereza nafasi zetu zinamalizwa na wageni. Mwajiri gani wa kiswahili atakupa kazi bwana? Kiswahili tunakijua kimeshindwa kutufikisha kwenye neema, wakubwa na wanaharakati kama mtoa mada wanatudanganya watoto wao wanapeleka English Medium au nje ya nchi. UNAFIKI!
 

richone

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
146
Points
195

richone

Senior Member
Joined Apr 3, 2012
146 195
dad! many many is born and me in oder number.
kingereza is very cantankerous
elimu yangu ni BA linguistics ya chuo kikuu cha UDSM, masters UDOM na sasa natauta PHD UDSM
 

Forum statistics

Threads 1,392,742
Members 528,684
Posts 34,116,790
Top