Ukitaka kujua tabia ya rais wetu angalia tabia za wateule wake kama maDED, maRAS, maRC, maDC.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Kuna msemo mashuhuri unasema "Ukitaka kujua tabia ya mtu wachunguze rafiki zake".

Hawa ni baadhi tu ya wateule wanaoaminiwa na mkulu....

1. Madelu ...kashifa ya majina.
2. January... kuiba mtihani Galanos.
3. Makonda... kashifa ya majina na kupiga wazee.
4. Gambo.....akiwa DC alipelekwa mahakamani ...degree za ch..p..
5. Muhongo...kashifa ya Escrow na kurudia shule.
6. ..... to be continued......

Kwa sisi ambao tulikuwa hutuijui tabia ya rais Magufuli mbali ya kuambiwa tumeanza kuijua kupitia kwa wateule wake.

Rais hawezi kukwepa matendo na matukio yanayofanywa na wateule wake ya kwamba hayamuhusu, kwa vile vituko vingi vinafanyika bila kuvikemea na wakati mwingine tumesikia akipongeza.

Kuna watu wengine wamefikia hatua ya kudhani huwa wanatumwa kufanya hayo wanayoyafanya na mteule wao.

DED anapompigisha deki mwalimu mbele ya mwanafunzi bila kukemea tabia hiyo, basi tunaweza kudhani bila shaka hata kama angekuwa yeye angefanya hivyo.

Siku RC wa Arusha mh. Gambo alivyotaka kukwamisha uzinduzi wa mradi wa Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto tunaweza kudhani hata angekuwa yeye angefanya hivyo.

Vitendo vya polisi kuvamia na kuvuruga vikao na mikutano ya vyama vingine bila ya yeye kuona tatizo ni kuonyesha dhahiri anabariki.

Mifano iko mingi, hata kitendo cha kutokuchukua hatua juu ya Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha na mbunge waliotuhumiwa kumteka mwalimu Batuli.

Kwa vile rais hufumbia macho vituko kama hivyo nilivyovitaja, na wakati mwingine kusikika akiwapongeza wahusika, ina maana tabia walizonazo hao anaowapongeza zina-reflect yeye alivyo.

Bound to be corrected.
 
Quinine uko sahihi hawa jamaa ni watu wa visasi na sijui kama Tz ya viwanda itawezekana kwa visasi hivi ??!!
 
Kama ni kweli Gambo alipigiwa simu na JPM na kumwambia yupo pamoja nae baada ya kuvuruga hafla ya Uzinduzi wa ujenzi wa hospital ya wakina mama na watoto.

Basi kutakuwa na shida kubwa sana kwenye nafasi ya juu kabisa ya utawala wa Nchi hii.

Na kawaida ya watu type ya Gambo huwa hawaaribu mara moja. Atakuja kuharibu siku nyingine ndipo mamlaka ya uteuzi wake itakapoona ilivyo achwa utupu.
 
Kama ni kweli Gambo alipigiwa simu na JPM na kumwambia yupo pamoja nae baada ya kuvuruga hafla ya Uzinduzi wa ujenzi wa hospital ya wakina mama na watoto... Basi kutakuwa na shida kubwa sana kwenye nafasi ya juu kabisa ya utawala wa Nchi hii.
Na kawaida ya watu type ya Gambo huwa hawaaribu mara moja.. Atakuja kuharibu siku nyingine ndipo mamlaka ya uteuzi wake itakapoona ilivyo achwa utupu.
Gambo mwenyewe alisema tena mbele ya kamera kuwa rais kampongeza,

sijui zilikuwa pongezi za kukwamisha maendeleo au kitu gani.
 
7m ni nyingi,acha niishie hapa............
images-396.jpeg
 
Kama ni kweli Gambo alipigiwa simu na JPM na kumwambia yupo pamoja nae baada ya kuvuruga hafla ya Uzinduzi wa ujenzi wa hospital ya wakina mama na watoto... Basi kutakuwa na shida kubwa sana kwenye nafasi ya juu kabisa ya utawala wa Nchi hii.
Na kawaida ya watu type ya Gambo huwa hawaaribu mara moja.. Atakuja kuharibu siku nyingine ndipo mamlaka ya uteuzi wake itakapoona ilivyo achwa utupu.
ndipo atakapo pandishwa cheo
 
Nchi ya kusadikika nchi ya viwanda nchi ya matajiri kuishi kama mashetani...daaah....kuna wakati sitaki kusikia mambo ya Taifa la maajabu ya dunia hata kidogo kwani viongozi wayafanyayo awamu hii ni vituko visivyo na kifani.
 
jpm anahitaji sana maombi maana hata yeye aelewi tunaenda wapi,kila siku matamko,matendo yake ni tofauti na maneno mikopo hakuna,dawa hakuna mahakama ya mafisadi hakuna jaani shida tupu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom