Ukitaka kujua namna Tanzania itakavyokuwa chini ya Upinzani, angalia namna CHADEMA kinavyoongozwa

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,668
40,917
Ukitaka kupata picha hata bila ya kukipigia kura chama cha upinzani namna watakavyotawala nchi angalia namna vyama vinavyoongozwa.

Ingawa wapo watakaosema kuwa kuna tofauti kati ya nchi na chama, ila chama ndio kipimo pekee kwa vyama vya upinzani kwa mtu anayetaka kufanya maamuzi, kwani watu huunda taasisi na taasisi ndio watu, na watu hao hao ndio huunda Taifa, hivyo namna unavyowaongoza watu katika taasisi ndivyo utakavyowaongoza katika Taifa.

Chadema ina uoza ufuatao;

1. Utawala wa kimabavu.

Hakuna mwenye haki wala ubavu wa kupingana na maanuzi ya mwenyekiti, maamuzi ya mwenyekiti ndiyo ya mwisho. Mifano ya walijaribu kupingana na mwenyekiti wakakutana na nguvu zake, ipo mingi. mifano ya maamuzi yaliyofanyika bila kupingwa ipo mingi, hakuna haja ya kufanya marudio.

2. Utawala usiokuwa na kikomo;

Chadema hakina kipengele cha ukomo wa uongozi wa mwenyekiti, hiyo inatuambia kuwa endapo Chadema watachukua nchi, kama walivyobadili katiba ya Chama, na kwa ubabe wa mwenyekiti, hakuna atayeweza kumzuia kubadili katiba ya Nchi ili atawale milele.

3. Uwazi wa mapoto na matumizi.

Kuna matumizi ya Zaidi ya Bilioni 7 yasiyokuwa na maelezo,

Chini ya Chadema tegemea upotevu mkubwa wa fedha za kodi za wananchi kwa kashfa za kila namna.

4. Uongozi usiojali jinsia.

Chadema hawaamini katika usawa wa kijinsia, hilo lipo wazi. Hakujawahi tokea kiongozi mkuu wa chama cha chadema wa jinsia ya kike. wote ni wanaume.

Chini ya Chadema tegemea nchi kuongozwa kwa mfumo dume.

Hayo ni baadhi ya mambo machache sana ambayo utakumbana nayo chini ya utawala wa Chama cha Upinzani kama chadema.

Orodha ya vyama ni nyingi, mfano CUF mbayo migogoro haiishi. Hakuna maelewano, hivyo tegemea kuwa na serikali ambayo kila mtu ana maamuzi yake kulingana na kikundi chake.

NCCR ambayo kiongozi mkuu wa chama ni tegemezi kwa vyama vingine, kiongozi kama huyu hawezi kuweka dira ya Taifa na kuisimamia.

Kwa uchache tu upinzani wetu ndivyo ulivyo na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sasa ndivyo watakavyoendesha serikali, usitegemee watabadilika watakaposhika madaraka.
 
Magonjwa ya akili na upungufu wa madaktari bingwa wa magonjwa hayo:,...........
 
Ingenoga usingetia maelezo ya namna wapinzani wanavojiendesha, ukaacha tu watu wajifikirishe wenyewe.
 
Hoja yako ingekua na maana kama kutakua na uchaguzi ill watu wasije chagua cdm, lakini kwa hali ilivyo tukiangalia chaguzi ndogo na kubwa zilizopita hakuna uchaguzi wowote mpaka labda 2030 wakati mtukukufu atakapo kuwa Mugabe fulani hivi nakushauri hifadhi hizo busara zako mpaka wakati huo!
 
Hoja yako ingekua na maana kama kutakua na uchaguzi ill watu wasije chagua cdm, lakini kwa hali ilivyo tukiangalia chaguzi ndogo na kubwa zilizopita hakuna uchaguzi wowote mpaka labda 2030 wakati mtukukufu atakapo kuwa Mugabe fulani hivi nakushauri hifadhi hizo busara zako mpaka wakati huo!
Mkuu kutakuwa na nini hiyo 2030?
 
Mkuu kutakuwa na nini hiyo 2030?
Hivi unavyo fikiri TZ kuna uchaguzi? Angalau wa wabunge kidogo, lakini wa ofisi kuu huwa hamna hata Nape anajua ss mtukufu akiwapo ndio hata wa ubunge hautakuwapo labda 2030 wakati mtukufu atakapokua Mugabe flani hivi lakini kwa sasa ni mwendo kagamemseveniEthiopiaNamibiankuruzinza mpaka Mobutu wa Seseseko Ngudubengu wa Zambanga
 
Back
Top Bottom