Ukitaka kujua kuwa chadema wako nyuma ya vurugu za mtwara soma tanzania daima la leo

Katika hali isiyo ya kawaida kabisa, leo gazeti la TANZANIA DAIMA limekuwa lipole sna kwenye ukurasa wake wa mbele huku likiandika JK atoa onyo kali. Upole huu wa gazeti la CHADEMA ni dhahiri kuwa wanajua walichokifanya n sasa wanasikiliizia moto unavyowaka.

CHADEMA sijui kama wanafurahia kusikia watu wamekufa, nyumba zimechomwa na hasara nyingi kutokana na vurugu hizo.



rafiki, unajua kufikiri kweli? sometimes i doubt about your intelligency
 
Analysis zingine ni balaa, jamaa alieleta huu uzi ni sawa na kiongozi anaekwenda sehemu akitegemea atapata upinzani wa nguvu kwa kila hoja anayotoa (assuming kuna mgogoro anaenda kutatua) alafu anakuta kila mtu aliepo kwenye mkutano anamsikiliza vizuri na kutoa hoja kwa kawaida na upole, AKITOKA HAPO ANAANZA KUUMIA NAFSI TENA YA KWANINI HAJAPINGWA
 
taswira ya cdm na vurugu za mtwara haitokani na cdm kuwaambia wananchi washike marungu,bali inatokana na sera yake ya kusimamia haki na ukweli,na hasa kutetea wanyonge,ccm wao hata wawapo bungeni hutetea chama na kuilinda serikali,hata kama wananchi wataathirika wao poa tu,ukiwa ccm na ukawa mkweli na mkosoaji,basi wewe utaitwa mtu hatari,kwasasa wananchi wenyewe na c kwa kuambiwa na m2 wanaelewa sana mambo,mf.bomu la kanisani arusha walishaanza kusema kunasiasa,kama cdm inasababisha vurugu kwa maneno yao je ni kwanini ccm haiwezi kutumia hayohayo maneno kuwafanya wananchi wake waone wanaishi maisha bora?WATU WA MTWARA HAWAJAONGELEWA KWA LUGHA YAO,LUGHA YAO NI JUU YA UMASIKINI WAO WA MDAMREFU BILA HATUA,PAMOJA NA HAYO,MSIIVURUGE NCHI,HAWA MUWANYIME KURA 2015 KWA KISHINDO.SIKU ZOTE WAMEKUA WAKITUMIA UNYONGE NA KUKOSA ELIMU(WALIOWANYIMA)WATU WENGI WA MTWARA KUJIGAMBA WANATOA KURA ZA DEZO BILA KUHOJI.
 
Katika hali isiyo ya kawaida kabisa, leo gazeti la TANZANIA DAIMA limekuwa lipole sna kwenye ukurasa wake wa mbele huku likiandika JK atoa onyo kali. Upole huu wa gazeti la CHADEMA ni dhahiri kuwa wanajua walichokifanya n sasa wanasikiliizia moto unavyowaka.

CHADEMA sijui kama wanafurahia kusikia watu wamekufa, nyumba zimechomwa na hasara nyingi kutokana na vurugu hizo.

hivi wewe si nape au riz? Maana Hawa wa wawili tanzania ambao akili zao ni sawa na za marehemu enzi za zinjatropus.subirini 2015
 
Watanzania wenzangu,wito wangu ni kwamba vurugu za mtwara zisipuuzwe, upelelezi yakinifu ufanyike na wote waliohusika katika vurugu wafikishwe mahakamani, sipendelei sana kuhusisha vyama au dini fulani katika mambo haya kwasababu hayo huongeza chuki ambayo siyo utamaduni wa watanzania kuchukiana, na zaidi ya hapo hatujengi bali tunabomoa zaidi, ukisema chama fulani kimehusika maana yake kuwe na ushahidi wakutosha kuhusisha chama, ukisema dini fulani imehusika uwe na ushahidi juu ya dai hilo hali kadhalika mtu kwa jina lake.

Mtu akienda kushiriki vurugu kwa maana ya kuhamasisha au kwa kwenda yeye mwenyewe atapaswa kushitakiwa kama yeye na siyo chama au dini anayotumikia, But: endapo ikithibitika kuwa mtu huyo ametenda hayo kwa maelekezo ya chama chake ( kuwe na ushahidi wa aidha kikao halali cha chama kilichoadhimia hayo) au dini yake then hapo chama au dini itapaswa kushitakiwa.

Ushauri wangu watanzania ni kwamba tusikimbilie kuamndika vitu ambavyo mwisho wake havina dira kwa nchi yetu, Polisi ipo ni kazi yao kufuatilia na kubaini uhalifu katika nchi yetu.

Natoa pole sana kwa waathirika wa tukio baya hili na kwakweli huu siyo utamaduni wa Kitanzania tumuombe Mungu sana atuepushe na Machafuko.
 
Back
Top Bottom