Ukitaka kujua kama wewe ni mchawi ama una roho ya kichawi

mathabane

JF-Expert Member
Jan 27, 2013
2,406
1,888
Nimegundua asilimia kubwa ya waafrika kama sio Waswahili ni wachawi kwa asili.

Tatizo kubwa wanalokumbana nalo ni ukosefu wa zana zá kufanyia kazi ili kutimiza adhima yao.

Ukitaka kujua kuwa wewe pia ni mchawi uliekubuhu : Hivi hapa chini ni viashiria :

í. Unapata faraja ukiona mwenzio kupata majanga.

ii. Roho inakuuma ukisikia mafanikio ya mwenzako.

iii. Habari njema kwako ni mtoto wa jirani yako kufukuzwa shule. Habari mbaya ni mtoto kufaulu.

vi. Habari mbaya kwako ni mtoto wa mwenzio kuolewa, faraja yako ni pale ameachika ama hapati mtoto.

v. Habari njema kwako ni mfanyakazi mwenzio/bosi wako kutumbuliwa.

vi. Habari mbaya kwako ni jirani kununua gari, habari njema ni gari lake lipige mzinga.

vii. Habari njema kwako ni MV Nyerere kuzama na kuuwa watu.

Ongezea nawewe zá kwako kujipima.
 
UKITAKA KUWAJUA WACHAWI WA KITANZANIA KWA WEPESI, ANZISHA UZI HUMU JF WA KUSIFIA MAFANIKIO YA MTU KAMA MBWANA SAMATTA, SSB, MENGI ama MO! Nakuambia utawajua!
 
Na mnaompinga MAGUFULI na kazi zake anazotufanyia Ni wachawi vile vile.msiompenda Rais wetu Ni wachawi.ndo tushasema!
 
unadhani wazungu ndio hawana roho ya kwanini, we jidanganye tu!
Unadhani sanchez hataki kuwa kama ronaldo, inamuuma nayeye pia, jealous
 
Kutamani sio vibaya.

Nyie Waswahili unataka akatike mguu ili asikupite. Ama ikiwezekana afe kabisa
 
Nimegundua asilimia kubwa ya waafrika kama sio Waswahili ni wachawi kwa asili.

Tatizo kubwa wanalokumbana nalo ni ukosefu wa zana zá kufanyia kazi ili kutimiza adhima yao.

Ukitaka kujua kuwa wewe pia ni mchawi uliekubuhu : Hivi hapa chini ni viashiria :

í. Unapata faraja ukiona mwenzio kupata majanga.

ii. Roho inakuuma ukisikia mafanikio ya mwenzako.

iii. Habari njema kwako ni mtoto wa jirani yako kufukuzwa shule. Habari mbaya ni mtoto kufaulu.

vi. Habari mbaya kwako ni mtoto wa mwenzio kuolewa, faraja yako ni pale ameachika ama hapati mtoto.

v. Habari njema kwako ni mfanyakazi mwenzio/bosi wako kutumbuliwa.

vi. Habari mbaya kwako ni jirani kununua gari, habari njema ni gari lake lipige mzinga.

vii. Habari njema kwako ni MV Nyerere kuzama na kuuwa watu.

Ongezea nawewe zá kwako kujipima.
Hada wazungu hawataki weusi tufanikiwe, hata wachina hawapendi waafrika tufanikiwe, hata wahindi hawapendi weusi tufanikiwe, hata warabu hawapendi weusi tufanikiwe.Watu wote duniani wana roho za kichawi ndio maana yesu na mtume walianzia huko kwenye roho za kichawi.
 
Back
Top Bottom