Ukitaka kuhama dunia kwa muda, au ukitaka kuwajua watu wazima wenye akili za kitoto, ingia Facebook

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Ukitaka kuhama dunia kwa muda, we usipate shida. Ingia Facebook. Au ukitaka kurudi utotoni pia, hakuna gharama we nenda tu. Ukitaka sifa pia, wala usipate shida. We nenda huko. Ukitaka kuwajua watu wazima wenye akili za kitoto we tumbukia tu huko. Hata yanapotokea matukio makubwa ambayo watu wanatakiwa wajulishwe mapema. Huko huwa wa mwisho kupokea taarifa. Hakuna ladha, ni sawa na chapati ya unga wa muhogo. Mambo yote JF, BIG UP JF
 
poopy.gif
Watu wa Facebook uwa wanafanya hayo hapo juu mkuu...wala usiumize kichwa....
 
Mimi nadhani ukitaka kuhama hii dunia,ni kuwa mbali kabisa na simu na mtandao.....Pia watu wazima wenye akili za kitoto wanapatikana Bar na kwenye guest house na kwenye ma-lodge wakiwa wameacha wake zao,watoto zao na waume zao huku wakifanya mambo ya kijinga.....
FREEDOM OF SPEECH!!
 
Wakuu nilishawahi kuuliza nawezaje kujiDelete kabisa kwenye FacePumba naomba mwenye msaada anisaidie tafadhali! nimeshadelete picha zangu zote sasa limebaki jina tu hii ndio shida nataka nisiwepo kabisa! Nitashukuru asanteni kwa msaada wenu.
 
Tabia inayoni-bore zaidi ni ya mademu mbalimbali wenye tabia ya ku-post picha zao kule sura kitabu wakisubiri likes na kupewa sifa wasizostahili,kama we mzuri ni mzuri tu!
 
FACeBoOk KuNa miCHezO mITamU sANa kULE HatA Mkw.ERe aNAliTaMbuA HiLo.
 
Ahaaaa nimeshajua namna yakujitoa kwenye FacePumba very easy nenda kule Google halafu anadika - how can i delete my facebook account! BASI UTAPATA MAELEKEZO YOTE NAMNA YA KUJITOA! kwa wale mademu mliokua mnanimendea na kuleta hadithi zenu zisizokua na nyuma wale mbele hamtaniona tena pumbaffffff mambo yote mnanipata hapa JF!
 
Ukitaka kuhama dunia kwa muda, we usipate shida. Ingia Facebook. Au ukitaka kurudi utotoni pia, hakuna gharama we nenda tu. Ukitaka sifa pia, wala usipate shida. We nenda huko. Ukitaka kuwajua watu wazima wenye akili za kitoto we tumbukia tu huko. Hata yanapotokea matukio makubwa ambayo watu wanatakiwa wajulishwe mapema. Huko huwa wa mwisho kupokea taarifa. Hakuna ladha, ni sawa na chapati ya unga wa muhogo. Mambo yote JF, BIG UP JF
Hayo ni mawazo na mitazamo yako, chadema wana ukurasa ndani ya facebook na wanautumia ipasavyo kuwapasha wafuasi wao habari!!
 
Hulazimishwi kuwa na rafiki,si lazima kuperuzi wall za watu, unaweza kuzuia kurasa yako baadhiya watu wasione halafu jiulize nini madhumuni ya facebook na wewe unachangia kiasi gani kuzuia mis-use.vile hata humu jf kuna watu na post zao utoto mtupu!
@ wote wanaokandia mitandao ya kijamii
 
Back
Top Bottom