Ukitaka kufuta upinzani fanya yafuatayo

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
597
2,225
1. Boresha elimu na pia toa elimu bure bila michango kuanzia chekechekea mpaka chuo kikuu.

2. Fanyeni mabadiliko na kutafutaa masoko ya ndani na kimataifa kwa wakulima na wavuvi.

3. Toa mikopo kwa wanafunzi wa chuo kikuuu kwa wakati na siyo kuwanyima mikopo au kuwapatia pungufu.

4. Boresha sekta ya Afya ili Watanzania wapate matibabu bora nchini ikiwemo viongozi wetu badala ya kwenda kutibiwa nje ya nchi. Mpaka hapo inaonesha jinsi gani viongozi wetu wenyewe walivyo hawaziamini huduma na hospitali zetu.

5. Toa ajira kwa kushirikiana na sekta binafisi hata millioni moja kwa mwaka au tengeneza mazingira rafiki kwa vijana wanaotoka vyuo vikuu waweze kupata mikopo rahisi na kujiajiri wenyewe.

6. Tengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wenye biashara zao tayari na wafanyabiashara ambao wanataka kuwekeza nchini.

7. Ongezea wafanyakazi mishahara ili waendane na mahitaji. Jiulize mtu kama mwalimu analipwa 350,000 kwa mwezi kabla ya kodi na akikatwa inabaki kama 270,000, hapo sasa jiulize hajalipa nyumba wala hajanunua nyanya kwa bei ya sasa Dar es salaam ambapo nyanya moja ni 400.

Hajalipa nauli, hajalipa umeme, pia hajalipa maji, hajanunua mafuta ya kupakaa au ya kula. Na hao walimu nimtolea mfano. Pia kuna manesi, nao hawana tofauti na walimu upande wa mishahara na maisha yao.

8. Boresha miundombinu nchi nzima na siyo kikanda au upande ambao ni wenu. Huo unaitwa ukabila, pia umimi.

9. Wape watu uhuru wa mawazo na kutoa maoni yao bila kuwasumbua au kutishia maisha yao.

Ukifanya hivyo vyote utafanikiwa kufuta upinzani usoni, lakini siyo mioyoni mwa watu maana mnachokifanya sio kwamba mnakomoa wapinzani, bali mnakomoa maisha ya Watanzania.

Hata mauaji ya kimbari Rwanda yalianza kwasababu ya wanasiasa uchwara na ambao walikuwa wanaona kuwa wenzao hawafai bali wao kundi dogo ndiyo bora. Hapo ndipo shida huwa zinaanzia.

Kingine, tujifundishe kupitia uchumi wa Zimbabwe umeathirika kwasababu ya mtu mmoja kujiona yeye ni Bora kuliko wengine na jamii ya kimataifa haikuwaacha ikawachapa vikwazo Tanzania tumenyimwa tu mkopo kutoka WB tumeanza kulia mpaka sasa kuna nchi zaidi ya kumi na mbili ambazo zimepunguza misaada kwa Tanzania ndio maana mnaona Mambo yanaenda ovyo ovyo.

Nina maswali mawili:

1. Je, Watanzania mnatakaa tuwe na maisha kama ya watu wa Zimbabwe wanayoishi Sasa hivi?

2. Au munataka yatokee kama yalitokea Rwanda, Sierra Leone, Liberia, Burundi, Uganda, Kenya 2008, au Ivory Coast, Watanzania au wanaCCM mnaopengeza kila kitu mnataka hayo yatokee?

Mzee Mangula, Dr Bashiru, Polepole, kiongozi mkuu wa malaika, Musiba, na Makonda msisahau kuhusu kifo cha Samuel Doe.
 
Utaitwa mchochezi mpinga maendeleo na asiye na uzalendo. Siku hizi Mwl. Bashiru na yule Mzee mstaafu Mangula kipaumbele chao ni kuufuta upinzani ili wasiweze kuhojiwa kama unavyowahoji sasa.
 
Samuel die ndio nani ?

Hayo ulisema yanafanyika sana na katika kiwango kikubwa sana sema kwa kuwa umekuwa mpingaji sana unashindwa kuyaona.

Kifo Cha upinzani hakitakuwa Cha ghafla kama Cha ajali ila Cha taratibu sana kama Cha mgonjwa wa kansa tena kitakuwa Cha kawaida "natural death" kwa maana ya kwamba vyama hivyo vitapoteza mvuto kabisa wa kuchagulika na kuuzika.
 
Shida ni kwamba "UPINZANI NI ITIKADI" sio watu. Hata ukinunua watu wa uoinzani ama ukiwaua watu, upinzani utabaki. Ni kama daladala. Akishuka mtu anapanda mwingine na safari inaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na madhara ya kuwanunua wapinzani kuongeza upinzani wa ndani kwenye himaya yako. Yetu macho.
 
Upinzani hauwezi kufutika hata ukiwekea watu mabomba ya maziwa na asali chumbani kwao.

Ikiwa bomba linatoa maziwa ya baridi utaibuka upinzani kuwa kwanini yasiwe maziwa ya moto? Likitoa ya mgando upinzani utaibuka kwanini yasiwe fresh? Yakitoka ya moto bado kutakuwa na upinzani kwanini yasitoke yaliyoganda.

Kiufupi ni kuwa upinzani upo naturally, hata wanaofanya vizuri wanapingwa, hata Chadema ikichukua nchi CCM watakuwa wapinzani hata kama Chadema watafanya maisha ya watu kuwa bora kuliko ilivyo sasa.
 
KARLO MWILAPWA,
Nilijua upinzani umekufa tayari kama mlivyokuwa mnajigamba,kumbe mmeanza kubadilika tena na kusema utakufa taratibu kama kansa inavyomaliza mtu! Daah
 
Hukuona jeshi la polisi walivyoandama mwezi mzima kama wao ndo walioitisha hayo maandamano? Kweli Inno hukuliona hilo? Kiukweli Ukuta uliwin sana kwa wanaoelewa maana ya siasa.
Kama kweli mnapenda hivyo vyama vya upinzani mbona mlishindwa kuandamana?
 
Samuel die ndio nani ?

Hayo ulisema yanafanyika sana na katika kiwango kikubwa sana sema kwa kuwa umekuwa mpingaji sana unashindwa kuyaona.

Kifo Cha upinzani hakitakuwa Cha ghafla kama Cha ajali ila Cha taratibu sana kama Cha mgonjwa wa kansa tena kitakuwa Cha kawaida "natural death" kwa maana ya kwamba vyama hivyo vitapoteza mvuto kabisa wa kuchagulika na kuuzika.

Ni hivi, tume huru ya uchaguzi ndio pekee inayoweza kuonyesha ni chama gani kinastahili kuwepo madarakani, sio tume hii inayotii maagizo ya rais.
 
Nasikitika kuona hutambui maana ya tume huru. Tume hata ikiwa haiwajibiki kwa Rais bado na itaendelea kuwa idara ya Serikali ambayo Rais ndio mkuu wa idara hiyo. Hii inatokana na muundo wa dola yetu kuwa na vyombo 3 ambavyo ni Serikali, bunge na mahakama na taasisi na mashirika na asasi zote zinaangukia hapo.

Unless kama unamaanisha time iwe mhimili wanne wa dola?
 
1. Boresha elimu na pia toa elimu bure bila michango kuanzia chekechekea mpaka chuo kikuu.

2. Fanyeni mabadiliko na kutafutaa masoko ya ndani na kimataifa kwa wakulima na wavuvi.

3. Toa mikopo kwa wanafunzi wa chuo kikuuu kwa wakati na siyo kuwanyima mikopo au kuwapatia pungufu.

4. Boresha sekta ya Afya ili Watanzania wapate matibabu bora nchini ikiwemo viongozi wetu badala ya kwenda kutibiwa nje ya nchi. Mpaka hapo inaonesha jinsi gani viongozi wetu wenyewe walivyo hawaziamini huduma na hospitali zetu.

5. Toa ajira kwa kushirikiana na sekta binafisi hata millioni moja kwa mwaka au tengeneza mazingira rafiki kwa vijana wanaotoka vyuo vikuu waweze kupata mikopo rahisi na kujiajiri wenyewe.

6. Tengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wenye biashara zao tayari na wafanyabiashara ambao wanataka kuwekeza nchini.

7. Ongezea wafanyakazi mishahara ili waendane na mahitaji. Jiulize mtu kama mwalimu analipwa 350,000 kwa mwezi kabla ya kodi na akikatwa inabaki kama 270,000, hapo sasa jiulize hajalipa nyumba wala hajanunua nyanya kwa bei ya sasa Dar es salaam ambapo nyanya moja ni 400.

Hajalipa nauli, hajalipa umeme, pia hajalipa maji, hajanunua mafuta ya kupakaa au ya kula. Na hao walimu nimtolea mfano. Pia kuna manesi, nao hawana tofauti na walimu upande wa mishahara na maisha yao.

8. Boresha miundombinu nchi nzima na siyo kikanda au upande ambao ni wenu. Huo unaitwa ukabila, pia umimi.

9. Wape watu uhuru wa mawazo na kutoa maoni yao bila kuwasumbua au kutishia maisha yao.

Ukifanya hivyo vyote utafanikiwa kufuta upinzani usoni, lakini siyo mioyoni mwa watu maana mnachokifanya sio kwamba mnakomoa wapinzani, bali mnakomoa maisha ya Watanzania.

Hata mauaji ya kimbari Rwanda yalianza kwasababu ya wanasiasa uchwara na ambao walikuwa wanaona kuwa wenzao hawafai bali wao kundi dogo ndiyo bora. Hapo ndipo shida huwa zinaanzia.

Kingine, tujifundishe kupitia uchumi wa Zimbabwe umeathirika kwasababu ya mtu mmoja kujiona yeye ni Bora kuliko wengine na jamii ya kimataifa haikuwaacha ikawachapa vikwazo Tanzania tumenyimwa tu mkopo kutoka WB tumeanza kulia mpaka sasa kuna nchi zaidi ya kumi na mbili ambazo zimepunguza misaada kwa Tanzania ndio maana mnaona Mambo yanaenda ovyo ovyo.

Nina maswali mawili:

1. Je, Watanzania mnatakaa tuwe na maisha kama ya watu wa Zimbabwe wanayoishi Sasa hivi?

2. Au munataka yatokee kama yalitokea Rwanda, Sierra Leone, Liberia, Burundi, Uganda, Kenya 2008, au Ivory Coast, Watanzania au wanaCCM mnaopengeza kila kitu mnataka hayo yatokee?

Mzee Mangula, Dr Bashiru, Polepole, kiongozi mkuu wa malaika, Musiba, na Makonda msisahau kuhusu kifo cha Samuel Doe.
Hapo namba 3 umezingua.
 
Nasikitika kuona hutambui maana ya tume huru. Tume hata ikiwa haiwajibiki kwa Rais bado na itaendelea kuwa idara ya Serikali ambayo Rais ndio mkuu wa idara hiyo. Hii inatokana na muundo wa dola yetu kuwa na vyombo 3 ambavyo ni Serikali, bunge na mahakama na taasisi na mashirika na asasi zote zinaangukia hapo.

Unless kama unamaanisha time iwe mhimili wanne wa dola?

Hatuhitaji tume inayowajibika kwa rais, tunahitaji tume huru itakayomtangaza mgombea aliyechaguliwa na wengi, na sio tume inayomtangaza mgombea anayetakiwa na rais.
 
Back
Top Bottom