Ukitaka kufilisika oa mke kutoka familia maskini

uzi Bora,
wanawake wanawake wanawake.
namshukuru Mungu nna mke sahihi kwangu,
hela zangu ni kwa ajili ya mke wangu na wanangu.
basi.
michepuko mingine ni dudu tu ns kusepa mbele.
nayachukia yanayoniomba hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana mnaoanza maisha msikurupuke kuowa tu sababu ya kupenda jaribu kuchunguza na familia ya huyo unayetaka kumuowa kiuchumi na kiutamaduni iko vipi la sivyo hamtaisha kuja na nyuzi za kurusha vijembe kwa wakwe zenu wanaohamia kwenu mazima bila taarifa na wale wapiga mizinga.

Kuna familia ukioa unaweza kujuta vizinga vinaanzia kwa mashemeji, mama mkwe, baba mkwe, hadi unaweza kujikuta umechanganyikiwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuzaliwa maskini sio kosa,kosa kushindwa kupambana kutafuta pesa na swala la Ndoa na pesa Ni vitu viwili Tofauti.

Babe pujo njoo useme machache.
 
Love, nilishamsahihisha huyo. Mapenzi Hawaangalii kipato cha mtu katika familia yao. Kwani pesa inatafutwa. Akifatilia icho kitu ndiyo aoe, basi hakumpenda huyo mtu bali alimtamani tu. Mpende kwanza, ndipo utajua nini uwezo wa mapenzi.
 
Hata umaskini wa familia zenu binafsi unawafilisi; baba, mama, kaka/dada na watoto wao; mjomba/shangazi na watoto wao etc; wote wanakutolea macho wewe. Wengine mna nyota tu za umaskini
Mimi naweza kuku unga mkono kwa asilimia 100%. Umasikini ni nyota ya mtu au uzembe wakukusudia. Mfano mtu kama Mchelle Obama hakutoka familia tajiri baba yake alikuwa anaunga unga kama fundi bomba ili wasome kweli mtoto wakike akawa na akili na uchungu kuikombowa familia yao leo nimke wa Rais. Same to Obama ndie pekee ktk Familia ya Obama alie toka. Mwangalie kaka yake yule wa mama wa Kenya nimasikin mpaka ananuka umasikin. Umasikini ni nyota ya mtu au uzembe wake. Wapo watu wamekuwa na nyadhifa kubwa sana ktk taifa au makampuni ila nimasikini wakutupwa. Ask why
 
Vijana mnaoanza maisha msikurupuke kuowa tu sababu ya kupenda jaribu kuchunguza na familia ya huyo unayetaka kumuowa kiuchumi na kiutamaduni iko vipi la sivyo hamtaisha kuja na nyuzi za kurusha vijembe kwa wakwe zenu wanaohamia kwenu mazima bila taarifa na wale wapiga mizinga.

Kuna familia ukioa unaweza kujuta vizinga vinaanzia kwa mashemeji, mama mkwe, baba mkwe, hadi unaweza kujikuta umechanganyikiwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inatokana nanyota kuna wanawake wananyota mbaya ukiowa tu unapotea ktk anga ya kupata pesa na mara nyingi hawa huwa niwazuri sana. Au waongaji wazuri ila niwaharibifu wa nyota za wanaume. Ndio maana wanaume malaya maisha yao huanguka ghafla ukashanga kumbe amekutana na mchepuko mwenye nyota mbaya same kuna malaya ukikutana nao utataka tena ukutane naye maana wananyota ya pesa. Ndio maana kuna watu hawaachi aina ya michepuko. Anampenda huyo huyo mpakaanaweza amisha makaz
 
Hii ni kweli kabisa. Mimi kuna mwanamke nilikuwa nae kwa muda mrefu sana. Alikuwa ananilazimishia kumpa ujauzito nikawa nachomoa maana nilikuwa bado nipo chuo. Nilipomaliza akawa anakomaa, nikamwambia asubiri tupate sehemu nzuri ya kuishi kwanza.

Nikashangaa analeta hoja ya kutafuta sehemu kubwa ya vyumba zaidi ya vitatu, nikamuuliza yote hiyo ya nini, akanambia wageni wakija tutawaweka wapi, nikamwambia wewe ni mkubwa sawa ila kwa hali ya uchumi wa sasa acha kufosi kuishi maisha ya kijamaa ya miaka ya 1990's maana hali ni tofauti kwa sasa.

Nikaona kuwa hajaridhika na lile jibu maana ndicho kitu alikuwa anataka kitokee. Nikawa nafanya mpango wa kumsaidia kupata kazi maana alikuwa anajitolea, akafanikiwa kupata kazi nzuri weee yenye viposho posho, weeeee si akaanza kuleta dharau. Akawa anapanga vitu kisiri na mama yake.

Kumbe mkakati ulikuwa ni apate pa kuishi halafu aje kukaa na wadogo zake na mama yake awe na pakufikia mjini plus ndugu wanaokuja mara kwa mara. Akatafuta sehemu, akapanga sijui kwa pesa gani maana me sikushiriki chochote nilianza kufanya maisha yangu kibaharia.

Nikawa naona tu post za maisha yake anayoishi huko na wadogo zake, nikajisemea kimoyo moyo, Tanzania jamii ya sasa isipokuwa makini, huu umasikini kuupiga vita itakuwa ngumu sana......

Maana watu wanaishi kimazoea sana hawatazamii uhalisia. Nikaona isiwe shida ila ukweli ni kuwa usipokuwa makini umasikini ni kama ukimwi, una ambukizika kirahisi kama mtu hayupo makini na mtu anaekuwa nao. Hawa mabinti siku hizi wamekuwa carrier wazuri sana wa umasikini kiasi kwamba ukithubutu kuingia nae katika maisha hautaelewa pesa inakwenda wapi na mfumo wako wa maisha utabadilika hautaelewa unaishi maisha ya namna gani.

Sisi wanaume huwa tunatarajia kuingia katika mahusiano tupate kale kamuda ka kuishi watu wawili tu yaani mimi na mke wangu tusiingiliane na ndugu wala familia zetu. Katika wakati huo twende kasi sana kujenga nyumba yetu na kujiwekeza kiuchumi na kujiendeleza. Familia zetu tunazisaidia ila tusizipe kipaumbele sana kwenye mambo yasiyo ya lazima.

Leo wanawake wanajikuta wanahuruma sana na familia zao kushinda sehemu alipo. Wewe unapambana unaleta ndani yeye akitafuta visingizio haviishi. Tena kuna muda anapanga na wazazi wake kuwa mzazi anaumwa aidha baba au mama ili tu apate kisingizio cha kutuma pesa kwa wazazi wao. Nilikuta ujumbe anachat na mwenzake anamwambia yaani wazazi wanisomeshe halafu wasipate matunda ya kunisomesha hapo ndipo nikajua napanga maisha na taahira....... Nikaachana nalo jinga moja lile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umefikiri saaaana mkuu, big up!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Love, nilishamsahihisha huyo. Mapenzi Hawaangalii kipato cha mtu katika familia yao. Kwani pesa inatafutwa. Akifatilia icho kitu ndiyo aoe, basi hakumpenda huyo mtu bali alimtamani tu. Mpende kwanza, ndipo utajua nini uwezo wa mapenzi.
Kuna wataalamu wa Mapenz wanasema kwamba Amani ndani ya nyumba huo ndio utajili,Maana yake,Hata nnchi ya Tanzania inaweza kuendelea Kwa sababu ya Amani sasa kama nnchi haina Amani kama Sudani kusini huo utajili au Kupata Mali ni kitu kisichowezekana ndo maana hadi leo Sudan Kusini Wanannchi wake wamategemea misaada Kutoka nnchi za nnje (jumuiya ya kimataifa) ili watu waweze kuishi, watu huuana Sk na Mapenz ni hivyo hivyo hamna Amani hamna maendeleo hamna utajili.

pujo
 
Hii ni kweli kabisa. Mimi kuna mwanamke nilikuwa nae kwa muda mrefu sana. Alikuwa ananilazimishia kumpa ujauzito nikawa nachomoa maana nilikuwa bado nipo chuo. Nilipomaliza akawa anakomaa, nikamwambia asubiri tupate sehemu nzuri ya kuishi kwanza.

Nikashangaa analeta hoja ya kutafuta sehemu kubwa ya vyumba zaidi ya vitatu, nikamuuliza yote hiyo ya nini, akanambia wageni wakija tutawaweka wapi, nikamwambia wewe ni mkubwa sawa ila kwa hali ya uchumi wa sasa acha kufosi kuishi maisha ya kijamaa ya miaka ya 1990's maana hali ni tofauti kwa sasa.

Nikaona kuwa hajaridhika na lile jibu maana ndicho kitu alikuwa anataka kitokee. Nikawa nafanya mpango wa kumsaidia kupata kazi maana alikuwa anajitolea, akafanikiwa kupata kazi nzuri weee yenye viposho posho, weeeee si akaanza kuleta dharau. Akawa anapanga vitu kisiri na mama yake.

Kumbe mkakati ulikuwa ni apate pa kuishi halafu aje kukaa na wadogo zake na mama yake awe na pakufikia mjini plus ndugu wanaokuja mara kwa mara. Akatafuta sehemu, akapanga sijui kwa pesa gani maana me sikushiriki chochote nilianza kufanya maisha yangu kibaharia.

Nikawa naona tu post za maisha yake anayoishi huko na wadogo zake, nikajisemea kimoyo moyo, Tanzania jamii ya sasa isipokuwa makini, huu umasikini kuupiga vita itakuwa ngumu sana......

Maana watu wanaishi kimazoea sana hawatazamii uhalisia. Nikaona isiwe shida ila ukweli ni kuwa usipokuwa makini umasikini ni kama ukimwi, una ambukizika kirahisi kama mtu hayupo makini na mtu anaekuwa nao. Hawa mabinti siku hizi wamekuwa carrier wazuri sana wa umasikini kiasi kwamba ukithubutu kuingia nae katika maisha hautaelewa pesa inakwenda wapi na mfumo wako wa maisha utabadilika hautaelewa unaishi maisha ya namna gani.

Sisi wanaume huwa tunatarajia kuingia katika mahusiano tupate kale kamuda ka kuishi watu wawili tu yaani mimi na mke wangu tusiingiliane na ndugu wala familia zetu. Katika wakati huo twende kasi sana kujenga nyumba yetu na kujiwekeza kiuchumi na kujiendeleza. Familia zetu tunazisaidia ila tusizipe kipaumbele sana kwenye mambo yasiyo ya lazima.

Leo wanawake wanajikuta wanahuruma sana na familia zao kushinda sehemu alipo. Wewe unapambana unaleta ndani yeye akitafuta visingizio haviishi. Tena kuna muda anapanga na wazazi wake kuwa mzazi anaumwa aidha baba au mama ili tu apate kisingizio cha kutuma pesa kwa wazazi wao. Nilikuta ujumbe anachat na mwenzake anamwambia yaani wazazi wanisomeshe halafu wasipate matunda ya kunisomesha hapo ndipo nikajua napanga maisha na taahira....... Nikaachana nalo jinga moja lile.

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂 ujamaa ndio umetufikisha hapa.... hapa ndio mtajua kwamba siasa zina mchango mkubwa sana wa kuijenga nchi nawananchi wake au kuibomoa.... wakati siasa zaujamaa zinaletwa nchini slogan ilikuwa ni siasa za ujamaa na kujitegemea..ila sisi tulivyokuwa maandazi tuka apply ujamaa peke yake kujitegemea tukawaachia wachina..cuba na Russia.
 
Baba mkwe samahani mwanangu shemeji yako mdogo anasumbuliwa na vichomi na kifua kinamsumbua sana yaani anakonda tu,niliongea na baba yake akasema nijitahidi nitafute nauli nimpeleke huko(kwa baba mkwe)maana walishaachana"- akajaribu na mitishamba baba yenu(baba mkwe wangu)amesema hivyo.Nimeparangana kila namna lakini nimeshindwa kabisa naomba unisaidie mwanangu samahani sina namna.

Mimi:Mama ni kama shilingi ngapi inahitajika ya nauli?
Mama mkwe:ni elfu 65,000/= tu hela ya kurudi na wao wataparangana huko nikishafika.

Kumbuka hii ni January mambo mengi wanafunzi, kodi za ofisi na mahitaji ya shule mfukoni nilikuwa na 15,000/=tu kwa ajili ya mboga kifamilia nikajisemea moyoni "angekuwa ni mama yangu mzazi ningemshauri huu mpango austishe ili nimatafutie hela taratibu au anye alternative nyingine, lakini yule ni mkwe pengine ataona nimemyima tu,nikapambana kesho yake nikamuagiza wife akampelekea hiyo hela,leo wiki ya pili mama mkwe yupo tu,na dogo (shemeji yangu)yupo tu anaenda shule kila siku,hazipiti siku mbili kaagizwa dogo kuijia chochote, mara mboga,unga,mkaa
Dada mama anakuita,dada mama anasema hivi.....

Dada mama yule pale amesema uende,
Dada (mke wangu) ameshaanza kuchoka kuna wakati anawajibu vibaya mpaka naona aibu,kila siku wanakuja na shida haziwezi kupita siku mbili mama hajamuita binti yake,(tupo mtaa mmoja)
Asipoenda kwa mama yake asubuhi, basi jioni atasubiri haupo ataenda,asipoenda hiyo siku basi kesho bado mmelala asubuhi asubuhi wadogo zake watagonga mlango wameagizwa na mama.

Nina miezi mitatu tu kwenye ndoa hii mpya lakini nahisi ni kama miaka mitano,kumsaidia mama au ndugu yeyote ni swala lisiloepukika ila kwa upande wangu naona imevuka viwango vya kawaida,hapa sijaoa bali nimeachiwa familia,kwa sasa nina familia mbili.

Sent using Jamii Forums mobile app
😃😃 hizi tabia zinakera mnooo...ndio maana sisi wengine hatuoi
 
Vijana mnaoanza maisha msikurupuke kuowa tu sababu ya kupenda jaribu kuchunguza na familia ya huyo unayetaka kumuowa kiuchumi na kiutamaduni iko vipi la sivyo hamtaisha kuja na nyuzi za kurusha vijembe kwa wakwe zenu wanaohamia kwenu mazima bila taarifa na wale wapiga mizinga.

Kuna familia ukioa unaweza kujuta vizinga vinaanzia kwa mashemeji, mama mkwe, baba mkwe, hadi unaweza kujikuta umechanganyikiwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa . True

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wataalamu wa Mapenz wanasema kwamba Amani ndani ya nyumba huo ndio utajili,Maana yake,Hata nnchi ya Tanzania inaweza kuendelea Kwa sababu ya Amani sasa kama nnchi haina Amani kama Sudani kusini huo utajili au Kupata Mali ni kitu kisichowezekana ndo maana hadi leo Sudan Kusini Wanannchi wake wamategemea misaada Kutoka nnchi za nnje (jumuiya ya kimataifa) ili watu waweze kuishi, watu huuana Sk na Mapenz ni hivyo hivyo hamna Amani hamna maendeleo hamna utajili.

pujo
Ni kweli usemacho
 
Baba mkwe samahani mwanangu shemeji yako mdogo anasumbuliwa na vichomi na kifua kinamsumbua sana yaani anakonda tu,niliongea na baba yake akasema nijitahidi nitafute nauli nimpeleke huko(kwa baba mkwe)maana walishaachana"- akajaribu na mitishamba baba yenu(baba mkwe wangu)amesema hivyo.Nimeparangana kila namna lakini nimeshindwa kabisa naomba unisaidie mwanangu samahani sina namna.

Mimi:Mama ni kama shilingi ngapi inahitajika ya nauli?
Mama mkwe:ni elfu 65,000/= tu hela ya kurudi na wao wataparangana huko nikishafika.

Kumbuka hii ni January mambo mengi wanafunzi, kodi za ofisi na mahitaji ya shule mfukoni nilikuwa na 15,000/=tu kwa ajili ya mboga kifamilia nikajisemea moyoni "angekuwa ni mama yangu mzazi ningemshauri huu mpango austishe ili nimatafutie hela taratibu au anye alternative nyingine, lakini yule ni mkwe pengine ataona nimemyima tu,nikapambana kesho yake nikamuagiza wife akampelekea hiyo hela,leo wiki ya pili mama mkwe yupo tu,na dogo (shemeji yangu)yupo tu anaenda shule kila siku,hazipiti siku mbili kaagizwa dogo kuijia chochote, mara mboga,unga,mkaa
Dada mama anakuita,dada mama anasema hivi.....

Dada mama yule pale amesema uende,
Dada (mke wangu) ameshaanza kuchoka kuna wakati anawajibu vibaya mpaka naona aibu,kila siku wanakuja na shida haziwezi kupita siku mbili mama hajamuita binti yake,(tupo mtaa mmoja)
Asipoenda kwa mama yake asubuhi, basi jioni atasubiri haupo ataenda,asipoenda hiyo siku basi kesho bado mmelala asubuhi asubuhi wadogo zake watagonga mlango wameagizwa na mama.

Nina miezi mitatu tu kwenye ndoa hii mpya lakini nahisi ni kama miaka mitano,kumsaidia mama au ndugu yeyote ni swala lisiloepukika ila kwa upande wangu naona imevuka viwango vya kawaida,hapa sijaoa bali nimeachiwa familia,kwa sasa nina familia mbili.

Sent using Jamii Forums mobile app
😂 😂 😂 😂 😂 😂 now ni two Years.
 
Vijana mnaoanza maisha msikurupuke kuowa tu sababu ya kupenda jaribu kuchunguza na familia ya huyo unayetaka kumuowa kiuchumi na kiutamaduni iko vipi la sivyo hamtaisha kuja na nyuzi za kurusha vijembe kwa wakwe zenu wanaohamia kwenu mazima bila taarifa na wale wapiga mizinga.

Kuna familia ukioa unaweza kujuta vizinga vinaanzia kwa mashemeji, mama mkwe, baba mkwe, hadi unaweza kujikuta umechanganyikiwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app

Mie hata wanangu nitawaambia usiolewe na mwanaume maskini wanakuaga wajinga sana wakishapata wanabadilika mnoo! Mwanamke utanyanyasika hadi unakufa au unaacha hiyo ndoa!

Na mwanaume nawe tafuta hela kwanza ndipo uoe siyo unaoa kuja kutesa mtoto wa watu!

Nyie ndio mnasababisha watu wanakua na michepulo ndani ya ndoa!

Kama hujapata hela usioe wala kuolewa shwainiii kabisa!
 
Back
Top Bottom