Ukitaka kudanganywa sikiliza zaidi wabunge wa CCM kuliko wa upinzani.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,365
2,000
Kama Ukitaka kudanganywa sikiliza wabunge wa CCM, lakini kama Ukitaka ukweli sikiliza wabunge wa upinzani.

Utafiti unaonyesha hivyo. Yanayomhangaisha Rais wetu Magufuli hivi sasa ni yaleeee yaleee kabisa yaliyokuwa yanapingwa na wabunge wa kambi ya upinzani bungeni na kushangiliwa na wabunge wa CCM. Wabunge wengi wa CCM wakisimama na kutoa hoja bungeni wanazungunza utadhani wanasema ukweli na kumaanisha kile wanachokisema na kutetea, lakini sivyo hivyo kabisa kabisa kabisa, na kama una sigara yako huo ndio wakati unaopaswa kutoka nje ukaivute ili kuepuka kudanganywa. Namna mambo alivyoyakuta Rais Magufuli alivyoshika madaraka huwezi kuamini kama kulikuwa na wabunge majority wenye akili na utashi. Hii ni tofauti kabisa kabisa na mabunge yote makini duniani. Wabunge wa hivi ni rahisi sana kwa mtu yeyote kuwakamata na kuwasweka rumande bila hata ya kijiuliza mara mbilimbili. Heshima ya mtu haitatokana kamwe na cheo, elimu, jinsia au nafasi yake kwenye jamii bali huduma yake iliyotuka kwa wanajamii. Ndiyo maana sio kazi ngumu sana kumheshimu Rais Magufuli kutokana na huduma yake anayopatia watanzania wenzake, anathubutu aone itakuwaje. Hili ni somo kwetu sisi wananchi na hata kwa Rais Dr. Magufuli. Ningekuwa mimi Dr. Magufuli ningemkumbatia kikwelikweli Zitto, Kafulila, Lissu, Mdee, Mnyika, Slaa, Bulaya, Mbatia, na baadhi ya wabunge wa CCM ambao sio ndiyoooo kama madodoki.
 

Targaryen

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
627
500
wabunge wa CCM uwa kama maroboti yanaendeshewa kwa remote ndio maana hata uyu anayepiga kelele sasa ivi hakuna ata siku moja bungeni kapingana na maamuzi ya wenzake afu leo hii anashangaa utazani kama vile ndio leo kajiunga CCM
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom