Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Hebu nawe wacha mambo ya kujisifa bila ya ushahidi wowote, tuonyeshe ni vipi umekuwa ukitengeneza hizo milioni in 30 seconds na pia itakuwa vizuri zaidi ukitueleza, kama unatengeneza helo sote hizo kwa second 30, ni kwa nini hadi sasa hajulikani kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchi?
Kuna dem mmoja aliniingia hivyo hivyo nijiingize kwenye hiyo biashara ya kupata milioni ndani ya sec 30 baada ya kumsanukia akaniblock kwenye WhatsApp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Mwenye Daladala Dodoma Me Naahid Ntakua Konda Mzuri Anitafute Na Me Natafuta Deleva Mwaminifu Nina Uzoefu Na Hzi Biashara 0769901199
 
Kwa yeyote mwenye utalaam na biashara ya daladala,nataka kununua DCM moja nifanye biashara hapa mjini,naomba kujua changamoto ya hii biashara,mtaji wangu ni 20 million.
 
Umuofia kwenu!

Jamani mimi ni employee katika private sector. Katika kufikiria namna ya kujiongezea kipato nimewaza kukopa pesa benki ili niagize hiace na nianze kupiga ruti za Kasulu-kigoma au kasulu-kibondo. Hii Biashara sijawahi kuifanya ila nategemea kuisimamia baada ya kutafuta dereva anayeweza kuaminika.
Ningependa kujua yafuatayo;

1. Hiace aina gani inayofaa?
2. Kwa mazingira ya Kigoma engine gani inafaa? CC zake pia aina ya mafuta (diesel/petrol)
3. Profit margin ya huku ikoje, katika misimu ya mvua na kiangazi?
4. Ningependa kujua pia kuhusu bima ya gari ya Biashara kama hii ya hiace, especially comprehensive/premium ikoje?
5. Kama nimenunua from Japan, gharama ya kuweka viti vya abiria ikoje?
6. Pia ningependa pia kujua chochote kile kinachohusiana na biashara hii kutoka kwa wazoefu/majongwe wa biashara hii.

NB:
Kasulu-kigoma ni 90 km na nauli ni Tsh. 5,000/= na
Kasulu -Kibondo ni 150 km na nauli ni Tsh. 10,000/=.
Barabara zote ni za vumbi na gari linaweza likaenda na kurudi kwa siku bila shida.

Thanks!
 
Biashara ya Hiace ni biashara nzuri maana Hiace ni gari imara sana. Hiace nzuri ni ile yenye engine ya Diesel. Iwe auto au Manual ulaji wa mafuta hauna tofauti kubwa. Ila kabla ya kuiendesha gari hakikisha kuwa umeikatia bima kubwa ya comprehensive. Nilinunua dala dala ikakaa mwezi mmoja tu bara barani. Dereva akala mzinga. Ningekuwa na bima kubwa ningelipwa. Ile gari niliishia kuiuza kama screpa...
So make sure una bima kubwa. Gari ikifanya kazi pesa inaonekana. Ukipata gari nzuri hata miaka mitano inakaa.
Je bajeti yako ni shi ngapi nikusaidie kuchauga gari?
 
Toyota Hiace Van 1997

Mkuu, kama unataka kufanya biashara ya Hiace, chukua hii gari. Gari bado mbichi kabisa. Nimejaribu kuchek kwenye mitandao mbali mbali, gari nyingi zimetembea kuanzia km 250,000.
Kwa gari hii ukipata dereva mzuri itapiga kazi hata kwa zaidi ya miaka mitano! Ila chonde chonde baba, kumbuka kukata bima kubwa.
Pesa ukiwaomba jamaa wakutumie profoma watakutumia ukalipie pesa benki. Usimpe mtu yeyote pesa mkononi isipokuwa zile clearing fees za kumpa agent. Gari ikifika jitahidi ushuru ukalipe mwenyewe. All in all kila la kheri.
 
Mimi pia wa Kigoma njoo nikuuzie hii yangu iko shinyanga inapiga kazi. Kwa ruti ya kibondo to Is hapo ngoja niifiatilie ili nami niiweke hapo kama sikupata mteja wa haraka maana nahitaji pesa ya haraka na huko iliko nilifuata ubora wa barabara ili gari idumu ila sasa mzunguko sio mzuri. Kama ukiamua kuagiza nje safi hata Mimi nimeagiza mwaka Jana. Sikupenda za Dar huwa wanaleta muozo. Nilishangaa nikiwa Temeke gereji kufunga siti wateja wanaitaka na wakanambia kuwa hii sio ya showroom za hapa, ila uwe makini ukifuaya bei chee Italia alafu petrol ni nzuri injini haichemki na ukipata 2rz utatisha. Kazi njema ukipenda njoo nikuuzie maana hapo kgm wanaiogopa upya wanahisi being akua juu sana. Kgm wananinua used yoka mwanza na kahama zilizo choka. Vinginevyo asante kunionesha ruti ya kibondo hii ndege ndio inamudu izo mambo. Picha hii tukutane road babu.,
 

Attachments

  • IMG-20171014-WA0021.jpg
    IMG-20171014-WA0021.jpg
    65.4 KB · Views: 306
Back
Top Bottom