Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Hapo kwenye red............. nakubaliana na wewe ni kweli kuwa mfanyakazi ofisini lets say PPF tower ndo ofisi yake............AKANUNUE GUTA............HATAKUBALI SIMPLY BECAUSE GUTA NA PPF TOWER ''WHERE AND WHERE'' I mean wapi na wapi...???
Lakini tunasahahu yafuatayo....
1. hata kama kama guta litagongwa leo to right off, hiyo laki tano uliyoitumia kununua guta haitakuuma sana kama 10M za hicho kikorola ulichokinunua showroom ya used vehicles
2. spea za guta bei rahisi sana ukilinganisha na za korola
3. kuirudisha hiyo 10M kwa 10,000/= ya kila siku ya teksi takes longer than laki tano kwa 15,000/=
4. Ukiona simu yako inapigiwa na ya dereva wa guta yako presure remains the same, lakini simu ya kutoka kwenye kikorola chako ina uwezo wa kukuharibia siku.
5. Guta haina traffic police, kikorola traffic nje nje
6. Guta haina kulipa kodi, bima, manispaa, etc.............hivyo hiyo 15,000/= inakuwa yako peke yako lakini ile 10,000/= ya teksi juwa kuwa unagawana na TRA, MANISPAA, BIMA...............kwa hiyo effectively hupati 10,000/= but may be 6,000/= ambayo italiwa na service ya gari na kulipia presure zote za simu ya dereva wako.....................

JAMANI SIFA NDO ZINAZOTUUWA.......... STUKENI...........SIFA HAZIKUBALIKI
Mkuu umetishaje sasa.. misifa mwenzie ujinga
 
Mimi binafsi napenda biashara ya Daladala lakini changamoto ninazozipata ni kama ifuatavyo - (1)Kulipa rushwa- mimi magari yangu hayatoi rushwa kwa namna yoyote hile - Msimamo huu umeleta uhasama mkubwa sana kati yangu na Polisi.(2) kutokuwa na business stability - kwamba kuna mambo kama polisi wanapoteza muda sana- kwenye biashara yangu napoteza at least siku mbili kwa wiki za hesabu - polisi kaamua tu kukupiga faini kutokana na sababu namba moja (3) Kuna baadhi ya ruote, wamiliki wezangu wa mabasi hawataki gari zangu ziende zifanye biashara kwenye hiyo route (Mbaya zaidi aliyekuwa anaendesha kampeni hiyo ) ni Polisi traffic (ambaye nae ni mmiliki wa daladala).(4) Spare part-hii imekuwa changamoto kubwa sana (5) Mafundi-hawa sasa kila mmoja anajua jinsi ilivyokuwa shida.
 
Tatizo kubwa watu wengi wananunua gari mbovu,utaona ata hapa JF mtu ana tsh 7ml anatafuta hiace super roof!!!pindi dereva atapoleta taarifa ya kwamba gari imeharibika anasema dereva mbaya/mwizi nk.
Kibiashara gari nzuri ni manual ambayo ni disel ambalo ni expensive kuliko petroli automatic,hiyo biz ni nzuri maana kila dakika watu utoka sehemu moja kwenda nyingine sasa kama una gari nzuri na msimamizi mzuri utaipenda..hesabu ya daladala kwa Kigamboni Dar ni 60,000/siku.Ukinunua gari nzuri ukalipia kila kitu ili dereva asipate mwanya wa kusema amekamatwa hana kibali cha sumatra au sababu nyingine yoyote faida ni kubwa kuliko hasara,hasara kama umenunua mbovumbovu maana kila siku ni spare na fundi.
Lucku Sabasaba za Ramadhan(Ramadhan Kareem)
Hembu niambie bei ya Super roof kwa huko Dubai kwa sasa ni bei gani na estimated cost ya kuifikisha Bongoland
-Halafu kwakuwa wewe ni mdau,hembu nipe hesabu ya siku kwa sasa
 
mwakani january naianza hii biashara, ni wapi nitapata gari nzuri manual dezeli kwa bei nafuu? mimi nitaendesha mwenyewe
 
Wakuu habari! Hivi kwa 15M naweza kupata Nissan civilian ambayo iko vizuri nikaiweka barabarani na nikapiga hera vizuri?
 
Biashara ya usafirishaji ni ngumu sana.,usipoielewa na ukaingia kichwa kichwa..,
Vitu vilivyowafanya watu weng kukwama katika hii biashara ni
1. Dereva makini
2.usimamizi wako katika gari lako
3. Services
4. Kula yako na maisha yako kutegemea kipande cha siku....
Niliiogopa sana hii biashara but namshukuru mungu nilikwenda Zanzibar nikapata Nissan Carvan used safi.,nikaiweka barabara leo ni mwaka wa 3.,cjagusa engine wala gear box,wala diff,na imeshanipa gari nyingine Nissan carvan ya pili na najiandaa kutoa ya 3 mwezi may mwaka huu 2016.
Mkuu ulinunua kwa bei gani umenitamanisha kazi Mimi mjasilia Mali.
 
Dala dala uwe nayo mpya ndio utaona raha na ikiwezekana unakomaa ndani... hadi urejeshe pesa zako ndio uwaachie watu maana madereva ni pasua sana unawez ukalia
 
Nimejaribu kuwa nayo over the week end malipo yanakuwa mazuri hasa... wao wanakwambia ni kawaida kuwa na abilia wengi week end na siku za sikukuu (Ambazo ndizo siku mi nipo nyumbani)

Kwa upande wa pili ni vigumu mimi kumalizana na majembe na matrafiki maana nakuwa kazini. Na wao wanatake advantege hiyo!
unapo anza biashara kama hii unahitaji konda kama wewe mwenyewe,ambaye yupo tayari kulinda pesa zako. pia hakikisha matengenezo yote yanafanyika kwa fundi unaye mwamini na malipo hayapitii kwa dereva.

Tatu pandisha fedha ya makusanyo kutoka 50 kwenda 50 na hiyo 10 in akiba ya dereva na anaipata mwisho wa mwezi kama hakuna matatizo ambayo hayatokani na uzembe wake kama makosa ya barabarani ambayo hayahusiani na vibali.
 
Hiyo ni biashara nzuri tu kama ukikomaa!
Hawa madereva ndivyo walivyo, hawaishi sababu ila unatakiwa kuwa mkali. Kama umeshazoeana na hao madereva badilisha ruti kisha tafuta dereva mwingine na usimchekee, inaelelekea wewe mpole sana, hutapata hela ukiwa mpole na ndo maana wenye madaladala wengi ni wanaume kwani ndo wenye roho ngumu, komaa baba, kama ukishindwa mpe mtu akusaidie kusimamia, hata mimi naweza ila ukibadili ruti,
ni kweli, kama unaona biashara hii in ngumu, jiulize kwa nini watu wanaingiza magari kila siku.. wengi humu sio wafanyabiashara
 
ESSENCE CONDULT LTD.
Kwa wale waliopo ndani na nje ya Tanzania wenye Nia ya kuanzisha makampuni na biashara ndogo na kubwa lakini hawajuj waanzie wapi essence consult ndio jibu lako.
Na wale walioko kwenye biashara na hawana mchanganuo wa biashara (business plan) na hawajui waanzie wapi basi essence consult itakupatia jibu.

Na wale wanaotafuta ushauri wa biashara, wawekezaji na mikopo ya biashara na usajiri wa makampuni basi essence ipo kwa ajiri yako.
Kwa maelezo zaidi na huduma zetu:-

Essence Consult ltd
NHC Building,1st floor,
makunganya street,
Near Askari Manument ,
Dar es salaam.
0655 204 666
e.consult16@gmail.com.
 
Mi nashauri watakaopenda kuanzisha hii industry tufungue group la whatsaap ili tukutane huko
 
A
Nakuonea huruma sana kwa ufinyu wa fikra na uelewa wako. Nakuombea ili vizazi vyako visije kurithi uwezo wako wa kufikiri kwani ni dhahiri umeishia hapo ulipo na una tatizo kubwa la mental rut ambalo humzuia mtu kujifunza kitu kipya.

Rifaro sio biashara ya mtu mwingine. Ni yangu binafsi na nitaweza kuwarithisha warithi wangu baada ya kifo changu ili waiendeleze pale nilipoishia. Kwa mtaji wangu wa TZS 128,500 tu niliyowekeza kwenye biashara hii, nina fursa ya kutengeneza kipato cha mwezi kadri siku zinavyoenda ambacho hata ukiwa na madaladala 10 huwezi kuthubutu kunifikia.

Wewe ndio unafanya biashara ya DEIWAKA kwani kila siku lazima uwe na presha na biashara yako - traffic kakamata daladala, tairi limepasuka, dereva anaumwa, daladala limegongwa, dereva kanyonya mafuta, n.k. Mimi sina presha hizo kwani sihitaji kumuajiri mtu anifanyie biashara hii, siitaji kuisimamia kwani anaeisimamia ni kampuni ya Rifaro yenyewe kwa kunipatia ofisi yangu ndani ya mtandao yenye ripoti ya mapato yangu, wanachama waliopo kwenye mtandao wangu na mambo mengine mengi. Dakika mbili tatu kwa siku za kuongea na watu kama ninavyofanya hapa zinanitosha sana kufanya biashara hii kwa sababu hii ni Smart Business na sio biashara ya mitulinga kama ya Daladala na biashara zingine za karne ya 20.

Kwa wale ambao ni open minded na wangependa ku diversify business portfolio yao, mnakaribishwa kuangalia kuhusu mfumo na fursa iliyopo kwenye kufanya biashara hii ya Rifaro

Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?[/QUOT

Acha kuwa mvivu wa kufikiria wewe....mtt wa kiume usipende biashara za mteremko
 
Back
Top Bottom