Ukistaajanu ya Musa Utayaona ya Mkapa Kumtunuku Kikwete Udaktari wa Heshima!!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wakuu,
Mnaionaje hiyo ya mkapa kumtunuku udaktari wa heshima kikwete kwenye uzinduzi wa UDOM?? Naona kama ilikuwa kama FUTUHI vile!!!
 
wamekosa uelewa kajamaa kana GPA 2 hata masters hana sifa,mpaka apitie postgraduate,sasa hako kaudaktari si kubaka elimu huhu
 
Kura za urais za kuchakachua, degree ya kuchakachua. huyu siwezi kumwelewa kabasa. Hivi Jk anacho kitu gani ambacho amepata kwa jitihada zake na kipi anastahili? Urais wa heshima, degree za heshima mhh!
 
pia sio ze comedy ni vituko vya uswahilini

Me nilikumbuka kili kipindi cha Channel 5 (EATV) cha kutoka uswazi, kucheki TV yangu naona na mkwere na Ben Dom sikuamini nikataka nitafutie TV yangu panadol
 
Hata mwaka jana kwenye graduu Mzumbe walimpa nilishangaa sana, nikagundua kuwa wsomi wetu ni wanafiki sana wanahubiri ujamaa huku wakipractice ubebari
 
Duuuh!!Hii ndo Tanzania zaidi ya uijuavyo huyo ndo Rais aliyempa kijiti Rais wa Sasa na yeye akapewa Ukuu wa Chuo cha UDOM leo analipa fadhila kwakumuaward mwenzie Doctorate wakati ye mwenyewe hana na naamini hajui kabisa what it takes to have such a stuff.Kwa mtaji huu hatukaa tuendelee hadi tuwapate kina Joseph Kone.Mwenzenu hata hamu yakusoma imeisha kwa Kweli hapa Taaluma imeachwa uchi.
 
Anamshukuru kwa kumlinda ufisadi wake. Mkapa alihusika katika michoto ya EPA, Kiweira Coal Mines , radar na mingine. Mkapa hana shukurani nyingine isipokuwa hiyo tu.
 
Wakuu,
Mnaionaje hiyo ya mkapa kumtunuku udaktari wa heshima kikwete kwenye uzinduzi wa UDOM?? Naona kama ilikuwa kama FUTUHI vile!!!

Si unakumbuka JK alishasema Mkapa aachwe? Hicho alichofanya Mkapa ni kumpooza JK ili yasije yakaamshwa yale ya KIWIRA!:teeth:
 
MpingoMkavu,
Thanks for the post. Nadhani mjadala utakuwa na manufaa sana iwapo wenye utaalamu watatuwekea hapa
i) Honarary Degrees zinatolewa kwa watu wenye vigezo gani?
ii) Honarary Degrees kutolewa mtu anatakiwa kuwa na sifa zipi za msingi?
iii) vyuo vikuu vinavyotoa Honarary Degrees ni kila Chuo kikuu au na vyenyewe viwe na sifa gani kutoa Honorary Degree?
iv) Ili kutoa Honorary Degree Chuo Kikuu kinapaswa kupitia Mchakato gani ili Honorary Degree iwe na hadhi na kutambulika kimataifa kama Honorary Degree? Ninasema hivi kwa kuwa nimeshirikishwa sana wakati Baba wa Taifa alipopewa moja ya Honorary Degrees nikiwa Katibu Mkuu wa TEC. Wanaofahamu ni mchakato gani umetumika kumpata JK kama candidate wa Honorary Degree na candidates wengine ni kina nani na amewashinda kwa merits zipi?
v) Amepewa Honorary Degree baada ya vikao vipi vya Evaluation vya Chuo kikuu cha Dodoma, na hoja za msingi za kupewa Honorary degree zilikuwa nini?
vi) Honorary Degree yenyewe ilikuwa ya nini? Hakuna kitu kinaitwa Daktari wa heshima. Lazima kuna Daktari wa Sheria katika eneo fulani ambapo mhusika kwa vigezo vilivyowekwa na mamlaka ya Chuo husika na baada ya kuwashindanisha candidates katika eneo hilo anapewa Honorary Degree.
vii) Hatimaye je Chuo Kikuu chenyewe kilichotoa Honorary Degree (Udaktari wa heshima) kinachosifa na hadhi ya kutoa Degree hiyo ya Heshima? Ikumbukwe duniani ni vyuo vikuu vichache sana vinatoa Honorary Degrees kwa sababu inayoeleweka na kwa celebrities ambao wamepitia mchakato mkali kweli kweli. Vinginevyo mhusika anaweza kutundika tu Cheti chake ukutani kwa lengo la kujifurahisha lakini haitakuwa na thamani katika ulimwengu wa wasomi wa dunia.
Hivyo Natumaini tutamtendea haki JK, tutaitendea Haki Chuo Kikuu cha Dodoma iwapo wanaofahamu watatutonya misingi, mchakato wa Honorary Degree aliyopewa JK. Bila misingi hiyo tutakuwa tunajadili au kwa sababu tunamchukia tu JK, au ushababiki kwa msingi moja au mwingine na tutakuwa hatuwasaidii sana wale wanaofanya mambo hayo au kwa kujua au kwa kutokujua au kwa kulipa fadhila kama moja alivyosema.

wamekosa uelewa kajamaa kana GPA 2 hata masters hana sifa,mpaka apitie postgraduate,sasa hako kaudaktari si kubaka elimu huhu
 
Back
Top Bottom