50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,091
- 4,063
Wanabodi
Nianze kwa kuwatakia heri nyingi za mwaka 2014,
Mwaka 2013 tulishuhudia masuala mengi kwenye siasa za Tanzania, yapo yaliyofurahisha, yapo yaliyoliza, yapo yaliyoshtua na yapo yaliyoogofya. Katika mkusanyiko wa yote hayo nitajadili masuala mawili ambayo tulimaliza nayo mwaka 2013 na tunaanza nayo tena mwaka 2014 katika sura tofauti kidogo. Ukistaajabu ya Zitto Kabwe ni suala moja na utayaona ya Chadema ni suala lingine nitakalojadili japo kwa kifupi
Nianze na Mh Zitto Zuberi Kabwe (MB) ambaye amepambana kwa miaka mingi kwenye medani ya siasa na kujipambanua kuwa ni miongoni mwa viongozi makini, asiyeyumba wala kuyumbushwa kiasi kwamba ilipata kuandikwa kuwa Mh Zitto hanunuliki na hana bei. Uwezo wa Zitto ulivutia Watanzania wengi toka kwenye maeneo tofauti, bila shaka kuna vijana wengi wanaomwona Zitto kama 'model of excellence' hili halipingiki maana kwa mujibu wa Zitto mwenyewe ni kuwa ameishi kwenye siasa za ushindani kwa takribani miaka ishirini sasa. Na hapo ndipo inashangaza, inakuwaje Zitto ashiriki kwenye siasa kwa miaka 20, muda ambao amejijenga binafsi na amechangia kwa kiasi kikubwa kujenga upinzani unaoichachafya CCM awe ndio chanzo cha kuubomoa upinzani? Haiingii akilini kuona harakati za Zitto katika nusu ya pili ya mwaka 2013 zinaelekeza kuivuruga kabisa Chadema, chama ambacho anakiri ya kwamba ametumia jasho, machozi na damu kukijenga hata kifike hapo kilipo? Ni vigumu pia kukiri ya kuwa mchango wa Zitto kwa Chadema kuwa ni mchango wa kipekee, kwa mfano zipo taarifa kuwa huko jimboni kwake, sio madiwani wa Chadema wanaounda halmashauri, sasa umahiri wa Zitto kujenga chama uko wapi? Ama umahiri wa Zitto hauegemei kwenye kauli mbiu ya chama kuwa Chadema ni msingi? Well, mchango wa Mh Zitto bungeni umesaidia kwa kiasi fulani kuiinua chadema, lakini bungeni ni hatua ya pili muhimu baada ya hatua ya kwanza muhimu ya kuimarisha chama chake jimboni. Yapo mengi ya kushangaa kuhusu na kumhusu Mh Zitto kabwe, itoshe kushangaa namna Zitto anavyojinasibu kwa uhodari kuwa bila Zitto hakuna Chadema, kwamba bila Zitto hakuna Chadema madhubuti wala upinzani makini, kwamba bila Zitto, Chadema ni chama cha kaskazini,chama cha kidini na chama cha kikabila, kwamba bila Zitto hakuna wasomi wala wanademokrasia wa kweli huko Chadema...hakika kuna mengi ya kushangaa. Wakati nashangaa ya Zitto, niwakosoe wale wanaomshabikia Zitto bila kukosoa mitazamo na mienendo ya Zitto kwani kumtukuza Zitto ni aina moja ya utumwa wa fikra. Hivyo, niwatahadhalishe kwa roho safi kuwa ifike mahala tuyashangae ya Zitto Kabwe pengine itakuwa ni fursa nzuri kumfahamu kiongozi wetu huyu.
Utayaona ya Chadema ni suala la pili ambalo ningependa tulifikiri kwa pamoja. Yapo maandiko mengi humu jukwaani yaliyosadifu sio tu historia ya Chadema, bali pia migogoro na changamoto zinazokabili chama hiki cha upinzani hapa nchini. Vilevile, kuna masuala mengi ambayo tunayaona kwenye utendaji wa kila siku wa chama hiki, binafsi naona masuala mengi ya Chadema kwa maana ya ideas, mipango na utekelezaji wa mipango ya chama hiki imejielekeza zaidi kwenye ku-confront status quo ya Chama Cha Mapinduzi kushika hatamu. Tumeona harakati za Chadema kwenye kushambulia taasisi za utawala ikiwamo Mahakama, Dola na Serikali yenyewe. Kwa kiasi kikubwa Chadema imefanikiwa sio tu kufikisha elimu ya uraia kwa Watanzania walio wengi, pia kwa kiasi kikubwa Chadema imeilazimisha serikali na vyombo vyake vya utawala kuzingatia taratibu za utawala wa sheria japo kwa kiasi kidogo. Sitarajii ati harakati za Chadema kwa miaka 10 iliyopita ati zingeibadilisha kabisa serikali yetu ambayo utawala wa sheria upo kwenye maandiko zaidi ya utekelezaji. Ukiendelea kuitazama chadema utapa kuona kwamba migogoro inayoisumbua ni migogoro inayotengenezwa na wapinzani wake hasahasa CCM, kwa mgogoro unaoendelea hivi sasa kati ya Chadema na Zitto utapata kuona kwamba shutuma za Chadema kwa Zitto kuwa Zitto anahujumu chama zinaakisi uwepo wa CCM kwenye kambi ya Zitto. Kimsingi sidhani kama ni vibaya CCM kupambana na Chadema kupitia kwa Zitto, isipokuwa kama kijana najisikia aibu kuona kijana mwenzangu Zitto Kabwe anakwenda kinyume na tambo zake anapokubali kutumiwa na CCM ili kuidhoofisha Chadema. Ni aibu kwa vijana kutokuwa na msimamo madhubuti kiasi cha kukubali kutumika. Ijapokuwa ushahidi sisisi wa namna Zitto anavyotumiwa na CCM haujawekwa hadharani, lakini inapofikia hatua Naibu Katibu Mkuu wa Chadema anashutumiwa hadharani kuhujumu chama inatosha kabisa kwa vijana kuona aibu kwani inaashiria kuwa vijana hatuaminiki kupewa nafasi nyeti za uongozi. Hapa pia tunayaona ya Chadema kuwaamini vijana kwenye nafasi za juu za uongozi. Ukitafakari kwa umakini utaona kuwa Chadema ilikuwa inamuandaa Zitto aje kuwa ama katibu mkuu wa chama kama sio mwenyekiti kabisa baada ya kipindi fulani, sasa namshangaa tena Mh Zitto kwa kukosa uvumilivu kujipa muda kabla Chama hakijamuomba rasmi kugombea ama Uenyekiti ama Ukatibu Mkuu, na ndipo tunayaona ya Chadema kwa kuamua kumwondosha kabisa kwenye daftari la Wanachama. Swali linabakia, je, Chadema hawaogopi nini kitatokea baada ya kumwondosha Zitto kwenye daftari la wanachama?
Kwa kifupi, yapo mengi ya kushangaa kuhusu Zitto na yapo mengi ya kuona kuhusu Chadema. Ukipenda unaweza kushangaa mengi kuhusu Chadema na kuona mengi kuhusu Zitto. Hata hivyo itoshe kusema kuwa Mh Zitto na kauli zake anashangaza, misimamo yake na mitazamo yake inashangaza na hata harakati zake za siasa zinashangaza, yote tisa kumi ni washabiki na wafuasi wake nao wanashangaza kiasi kwamba hawajui kuwa Zitto aliyepambana na kufika alipo ni vile alilelewa kwenye misingi ya Chadema, leo hii tunaona Chama kinamwondosha kwa vile amekiuka misingi ya Chama, wafuasi na washabiki wa Zitto hawaoni hilo la Zitto kukengeuka misingi ya Chama kilichomlea, badala yake wanaona Chama kinakwenda mrama. Pia, tunaendelea kuona Chadema ikifanya difficult and painful decisions bila kujali hatma ya chama, ujasiri huu wa Chadema unaniweka kwenye wakati wa kujifunza kitu kipya toka Chadema. Tusubiri tuone